Ngasa kwenda Afrika ya Kusini ni sahihi

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
942
Reaction score
168
nimesoma gazeti moja kuwa kuna habari ngasa ameenda afrika kusini kufanya majaribio.
mimi nampa tano lakini uongozi wa yanga unadai kuwa hauna habari eti ikibainika kama kweli itampa adhabu.
nyie vikaragosi wa yanga acheni ujinga huo wa kumng'ang'ania mchezaji kama mmemzaa nyinyi.
 
Hata mimi nimesikia hiyo. Binasfi nampongeza sana japo clabuni kwake kuna mizengwe sana. Huwa hawataki mchezaji ahame mpaka kiwango chake kishuke
 
Labda kama ni mchezaji mwingine, ila kama ni mpuuzi Ngassa achukuliwe hatua stahiki. Huyu kijana mnayemtetea leo si ndo ambae alipata deal la kuchezea El Mereikh ya Sudan, tena Azam na Simba walishakubaliana kwa pamoja kumuuza kule na hiyo team ikatuma viongozi waje Dsm kuzungumza na mchezaji. Jamaa akawazimia simu ili asipatikane na kuzungumza na wale viongozi. Inasemekana kuna team ilimficha ili badae aje kusaini hiyo team, na kweli yalitokea. Sasa leo kashtuka nini?
 
Kuna haja ya kufahamu mambo mawili muhimu kwenye swala hili, ambayo inaonekana tumeyaweka kando hadi sasa kwenye mjadala huu: (1) haki ya mchezaji na ya klabu katika kuhamia timu nyengine (2) taratibu zinazohitajika ili mchezaji ajiunge na timu nuengine. Kwa hili la kwanza, itoshe tu kusema kwamba Ngasa ana haki ya kutafuta maslahi zaidi kwenye timu anayoona inamuhitaji, lakini na klabu nayo ina haki ya kupatiwa taarifa na, inapobidi, kutoa idhini kwa mchezaji huyo kufanya hivyo. Kwa hili la pili, ni wazi kwamba mchezaji aliye kwenye mkataba anakatazwa na sheria za FIFA kuwasiliana na timu nyengine isipokuwa kama atakuwa amebakisha miezi sita kwenye mkataba huo.
Kuliko kutapika jazba na kucheua ushabiki, ni vyema kuangalia maswala hayo kwanza.
 
Kama taarifa hii ni sahihi, all the best Ngasa.. maana pale jangwani Msuva kashatake over status yako.. Bora ukajaribu kutengeneza ufalme kwingine.
 

Ngasa alishachezea Azam na Simba lakini hawakumpeleka South Afrika. Kunya anye kuku, bata anaharisha.
 
Ngasa mwenyewe ni mjinga tu

Muda wote anawaza chupi

Alipokua simba alipata nafasi ya kwenda nje

Akaona Yanga ndio dili sana.

Wakamrubuni kuvunja mkataba kinyemela.Sasahivi analipa deni na linamgharimu
 

nasikie eti ngassa ana miaka 19?
 
Ngasa alishachezea Azam na Simba lakini hawakumpeleka South Afrika. Kunya anye kuku, bata anaharisha.

Kama kumbukumbu zako ziko sawa...simba walimtafutia ngassa nafasi kwenda kucheza El Merekh

Ila yeye kwa sababu ya kupenda sana chupi akagoma

Akadanganywa na matapeli wa Yanga...akavunja mkataba na simba ...sasa hivi kila mwezi anakatwa milion kuilipa simba...

Yanga walimuahidi watamsaidia kulipa laki tano kila mwezi...wamemtelekeza ...hawataki tena

Yanga ni timu ya hovyo sana
 

Yanga wana kosa gani? Yeye Ngassa aliwadanganya Yanga kuwa hakuwa na mkataba wowote na Simba ndiyo maana wakamchukua. Sasa ilipothibitishwa kuwa Ngassa alikuwa na mkataba halali Yanga wangekeua apuuzi kama wangemlipia hilo deni wakati hiyo haikuwa kwenye mkataba wakati Yanga wanamchukua. Tatizo Ngassa alifikiri ni bora sana na chochote ambacho angewaambia Yanga wangemfanyia bila kujali mkataba wao ulisemaje. Hiyo isingewezekana kwa Timu inayoendeshwa kwa kanuni. Halafu huyu Ngassa akalia eti wanachama na wapenzi wamchangie kulipa deni, akaanika akaunti yake hadharani wapenzi waingize mapesa. Nafikiri alipata mshtuko wa moyo alipoona hata mashabiki wa Yanga nao hawakumkomboa kwa sababu ya ujinga alioifanya. Naamini kabisa huko Afrika Kusini hatafanikiwa ila msishangae akija yeye mwenyewe akaanza kupayuka kuwa amefaulu na Yanga wamekataa kumruhusu aondoke. Movie kama hizo wachezaji wa TZ wamezoea kuzionyesha.
 


Mkuu, weka ushabiki pembeni kwanza. Uhovyo wa Yanga ndio uhovyo wa Mikia. Kumbuka Mbwana Samata alifikaje TP Mazembe. Simba ilishindwa kumpa Mark II waliyoahidi akagoma kucheza. Simba wakawa hawana jinsi lazima auzwe!

Issue ya Simba kumtafutia Ngasa El Mereikh ya Sudan ina siasa ambazo labda huzijui. Walishaona kwa vyovyote Ngasa angeondoka hivyo walitaka kumtumia kupata hela sio kupenda maendeleo yake. Mambo ya wachezaji kupenda chupi si la Ngasa pekee. Huyo Kapombe kwa nini alishindwa France? Hayo ni matitizo binafsi ya wachezaji.

Yanga ni timu pekee Tanzania ambayo mchezaji wake kacheza ulaya kwa mafanikio. Waulize wenzio wakuambie ni nani huyo.
 
Tatizo lako unaandika habari nusu nusu, unasema Samata alikataa kucheza kwa sababu hakupewa gari hapo hapo unasema kwamba ilibidi auzwe kwa sababu alikataa kucheza kwa hiyo unataka kuniambia TP Mazembe walimununua Samata bila kumwona akicheza? Ukweli ni kwamba ni kweli Simba walimwahidi kumpa gari lakini hawakumpa kwa wakati naye akafanya mgomo lakini baadaye wakampa gari na mechi ya kwanza tu kucheza alifunga goli mbili sikumbuki ilikuwa ni mechi dhidi ya timu gani.

TP Mazembe walimwona Samata kwenye match mbili ambazo hizi timu mbili zilikutana na Samata akiwa uwanjani ndo TP Mazembe wakavutiwa naye pamoja na Ochan na kuwasajili wote wawili sasa kama alikuwa hachezi TP Mazembe wangemsajili vipi bila kumwona kumbuka Samata hakuwahi kufanya majaribio TP Mazembe ili asajiliwe.

Na kuhusu Ngasa hata kama ni kweli Simba walijua kwamba Ngasa hatacheza Simba ingawa alikuwa ameshasaini mkataba tayari sasa kulikuwa na ubaya gani kumpeleka timu kubwa kama El Mereikh na hiyo ingekuwa ni kwa faida yake mwenyewe na kwa timu yake ya Simba pia.

Kuhusu huyo mchezaji unayemsema naye hakuondoka kwa ruhusa kutoka kwa uongozi wa Yanga, alichofanya ni kutoroka na kwenda South Afrika na timu ya huko South Afrika ndo ilifaidika naye wakati alipouzwa Ulaya, Yanga haijawahi kufaidika naye zaidi ya nyie kujisifia tu kwamba alichezea Jangwani. Kwa sababu yule alifanikiwa baada ya kutoroka mwacheni Ngasa naye huenda akafanikiwa ingawa ametoroka.
 

Hela za Okwi zimeishafika au bado? Za Kapombe je? Maana Simba ndio inajua kufaidi ikiwauza wachezaji!
 
Hela za Okwi zimeishafika au bado? Za Kapombe je? Maana Simba ndio inajua kufaidi ikiwauza wachezaji!

Naamini una ufahamu na uelewa mkubwa sana wa masuala madogo madogo kama haya, na naamini pia una uwezo mkubwa wa kuweza kutofautisha kati ya mzazi aliyepeleka mwanae shule akashindwa mwenyewe na mzazi ambaye hataki kusikia wanae wakienda shule. Na pia tofautisha kati ya mzazi ambaye anamruhusu mwanae kwenda mbali kujaribu maisha lakini kama atashindwa ni juu yake kuchagua kwingine.

Suala la Okwi linafahamika kuvunja kwa makubaliano kwa timu iliyomchukua Okwi ndo kumesababisha imani waliyokuwa nayo viongozi wa Simba kuonekana wajinga na waongo.

Kapombe hata wewe unajua kuna viongozi wa timu mbili walikuwa wanamrubuni Kapombe asirudi Ufaransa na bahati mbaya naye akarubunika ila angalau alipata watu wakamshauri vizuri akaenda timu aliyoenda na angejidanganya tu akaenda ile timu nyingine lazima yangemkuta ya Ngasa na Kaseja, hawataki kukuacha uondoke halafu hawataki ucheze hata dakika 15 za mwisho.
 

To be honest, hayo yapo Yanga peke yake?

La Kaseja lipo wazi. Simba walimwacha kwa kushuka kiwango lakini nakiri viongozi Yanga walifanya makosa kumsajili. Kiwango chake ndio tatizo. Kumbuka mechi ya Yanga na Coast Union kule Tanga. Vinginevyo tuseme aliuza mechi lakini tusifike huko tuseme kiwango kimeshuka.

Ngasa pamoja na mapenzi yake kwa Yanga ni kielelezo cha soka la Tanzania. Si Yanga, Azam wala Simba. Viongozi wa timu zetu kongwe pamoja na Azam ambao ungetegemea wabadilike kutokana na umilika wa Club, bado wapo kwenye ujima wa namna ya kuendesha soka.

Tuone VPL mwaka huu itaisha vipi safari bado ni ndefu
 

To be honest hayo mambo yako Yanga zaidi kuliko timu zingine, angalia Kavumbagu na Domayo walivyoondoka Yanga, mikataba yao imeisha lakini hawaonyeshi kama wanawahitaji au la hadi waliposikia kwamba Azam wamewasajili ndo na wao wakaonyesha kuwataka tena wakati wachezaji muda wote walikuwa nao.

Ile mechi haikuwa Yanga na Coastal, ilikuwa ni Yanga na Mgambo, lile lilikuwa kosa la kimchezo halikuwa kosa la kukusudia hata ile mechi ya Simba na Yanga pia halikuwa kosa la kukusudia lilikuwa ni kosa la kimchezo.

Ni kweli asilimia kubwa ya viongozi wetu wanafanana, wahenga walisema mnyonge mnyongeni haki ya mpeni, mimi nasema mnyonge msimnyonge na haki yake mpeni vile vile; pamoja na ubaya wote wa Rage na udhaifu alionao, huyu Msomali ana huruma kwa wachezaji labda na yeye kwa sababu alicheza mpira, kitendo cha Kapombe kumruhusu kwenda Ufaransa bila malipo yoyote ilikuwa ni faida kubwa kwa Kapombe kuliko kwa team, na kitendo cha kumruhusu Okwi kwenda Tunisia kwa mali Kauli ilikuwa ni faida kubwa kwa Okwi kuliko kwa team. Tofauti ya Viongozi na Simba na Yanga iko hapa: Kwa Simba: Kama uongozi utatotifautiana na mchezaji kwa ama kiwango chake kushuka ama tofauti zingine za kinidhamu mara nyingi watakuacha ukatafute timu na sio kukung'ang'ania, mifano ya hivi karibuni ni Kiemba na Chanongo lakini pia kuna Edward Christopher na Uhuru Selemani bila kumsahau Mwinyi Kazimoto ambaye alitoroka lakini uongozi ulimruhusu na biashara ikafanyika mpaka sasa anakipiga umangani.

Kwa Yanga hali ni tofauti angalia walichotaka kumfanyia Okwi mwaka jana walishaonyesha nia ya kumwacha mapema tu lakini hadi dirisha la usajili linakaribia kufungwa alikuwa hajapewa taarifa ya kuachwa na isingekuwa watu wapenda ukweli walioko pale tff kuamua kumweleza ukweli (bila kujali kwamba watapoteza kibarua chao au la na kweli wengine walipoteza) bila shaka angesubiri dirisha dogo au angeenda kutafuta timu nchi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…