Tatizo lako unaandika habari nusu nusu, unasema Samata alikataa kucheza kwa sababu hakupewa gari hapo hapo unasema kwamba ilibidi auzwe kwa sababu alikataa kucheza kwa hiyo unataka kuniambia TP Mazembe walimununua Samata bila kumwona akicheza? Ukweli ni kwamba ni kweli Simba walimwahidi kumpa gari lakini hawakumpa kwa wakati naye akafanya mgomo lakini baadaye wakampa gari na mechi ya kwanza tu kucheza alifunga goli mbili sikumbuki ilikuwa ni mechi dhidi ya timu gani.
TP Mazembe walimwona Samata kwenye match mbili ambazo hizi timu mbili zilikutana na Samata akiwa uwanjani ndo TP Mazembe wakavutiwa naye pamoja na Ochan na kuwasajili wote wawili sasa kama alikuwa hachezi TP Mazembe wangemsajili vipi bila kumwona kumbuka Samata hakuwahi kufanya majaribio TP Mazembe ili asajiliwe.
Na kuhusu Ngasa hata kama ni kweli Simba walijua kwamba Ngasa hatacheza Simba ingawa alikuwa ameshasaini mkataba tayari sasa kulikuwa na ubaya gani kumpeleka timu kubwa kama El Mereikh na hiyo ingekuwa ni kwa faida yake mwenyewe na kwa timu yake ya Simba pia.
Kuhusu huyo mchezaji unayemsema naye hakuondoka kwa ruhusa kutoka kwa uongozi wa Yanga, alichofanya ni kutoroka na kwenda South Afrika na timu ya huko South Afrika ndo ilifaidika naye wakati alipouzwa Ulaya, Yanga haijawahi kufaidika naye zaidi ya nyie kujisifia tu kwamba alichezea Jangwani. Kwa sababu yule alifanikiwa baada ya kutoroka mwacheni Ngasa naye huenda akafanikiwa ingawa ametoroka.