SoC02 Ngiri Maji Mawasiliano (Elimu kwa Wazazi kutatua ugonjwa mapema kwa watoto)

SoC02 Ngiri Maji Mawasiliano (Elimu kwa Wazazi kutatua ugonjwa mapema kwa watoto)

Stories of Change - 2022 Competition

Ked zee

Member
Joined
Aug 20, 2022
Posts
14
Reaction score
17
Naitwa Emmanuel ni kijana wa miaka 28,nilizaliwa na tatizo la ngiri maji mawasiliano.Ni ugonjwa ambao ungetibika nikiwa bado mtoto mdogo,lakini kutokana na kutopata elimu sahihi,Wazazi wangu walishindwa kulivalia njuga swala hili.Mpaka leo hii naishi na tatizo hili .Napenda kuchukua nafasi hii kutoka elimu kuhusu ngiri maji mawasiliano.

Ngiri maji mawasiliano ni nini?
Ngiri maji ni kujaa kwa maji kwenye kifuko cha kubeba korodani kwa wanaume.Ngiri maji huwa mawasiliano pale yale maji hutoka na kuingia kupitia uwazi uliopo kwenye kinena kuingia kwenye Kuta za tumboni.Uwazi huo huruhusu majimaji kutoka tumboni kuingia kwenye kifuko kinachobeba korodani.Ngiri maji isiyo mawasiliano hubaki saizi ileile kwa sababu haitoi na kuingiza maji.Ngiri maji mawasiliano huwatokea watoto wa kiume.Na 1 kati ya watoto 10 wakiume wanaozaliwa huwa na ngiri maji mawasiliano.


92601f1f-052f-476c-8401-68281e8be7b5(0).jpg


Nini kinasababisha ngiri maji mawasiliano?
Mtoto wa kiume korodani zake huwa tumboni mwake kabla hazijashuka kwenye kifuko kinachobeba korodani.Ngiri maji hutokea pale mtoto akiwa Bado yupo tumboni,kwenye kifuko cha uzazi wa mama yake. Utando (membrane) hupita kwenye mfereji wa inguinal, kwenye Kuta za tumboni mpaka kwenye kifuko cha korodani,uwazi huo wa utando kitaalamu huitwa (processus vaginalis). Ambao huzipitisha korodani kutoka tumboni kuingia kwenye kifuko cha korodani (scortum). Uwazi huo ukibaki wazi mtoto azaliwapo ndio husababisha majimaji kupitia na kutoka kwenye cavity ya tumbo na kifuko cha kubeba korodani.

Mzazi utatambuaje hili tatizo?
Kabla ya yote daktari au mtaalamu wa magonjwa ya watoto hutambua alionapo na kumuambia mzazi.Daktari hulitambua tatizo hili kwa kumulika mwanga kwenye kifuko cha korodani kuona kama maji yamelizunguka korodani.

Pia ultrasound hufanyika katika kifuko cha korodani kuangalia uvimbe au tatizo jingine liwezalo kujitokeza.

Ikitokea madaktari wakashindwa kuliona hilo tatizo mtoto akiwa bado yupo hospitali au alizaliwa nyumbani.

Mzazi unaweza pia kuligundua tatizo Hilo mwenyewe.Kwa kuangalia na kushika vifuko vya korodani.Mtoto mwenye ngiri maji mawasiliano huwa na kifuko kimoja kuwa kikubwa kuliko kingine, kutokana na kimoja kujawaa maji.

Pia ukishikapo hubonyea na kupungia kuashiria kujaa kwa maji
Saizi ya kifuko hubadilika mtoto akilala kwa sababu,maji hurudi tumboni na saizi huongezeka mtoto akiwa amekaa au kusimama sababu maji hushuka.

Kutoliona korodani moja kwakuwa hurudi ndani kupitia uwazi unaopitisha maji,kwa kukandamizwa au kulalia

Mzazi ni muhimu kwenda kumona daktari ugunduapo hizi dalili, kujua kwa kina nini kina msibu mtoto wako.

Hutibika vipi?
Mara nyingi ngiri maji mawasiliano hupotea na kujirekebisha yenyewe ndani ya miezi 6 au mwaka 1 mtoto azaliwapo bila tiba yote Ile.Lakini inaweza kutokea tatizo Hilo lisijirekebishe kwa kujifunga na mtoto akabaki nalo baada ya huo mwaka mmoja.Ikitokea hivyo itabidi mtoto afanyiwe upasuaji, kurekebisha Hilo tatizo.Mzazi hutakiwi kuwa na wasiwasi maana upasuaji wake ni rahisi na hauna changamoto nyingi .

Mtoto hupewa ganzi ili alale, Kisha mchano wa sentimeta mbili hufanyika katika ngozi iliyopo kwenye kinena,Kisha daktari mpasuaji hutoa maji yaliyomo kwenye kifuko cha korodani na kufunga uwazi wa utando (processus vaginalis) unaopitisha maji, Kisha kushona na kumaliza.

Mtoto hujiskia vizuri siku Moja baada ya upasuaji na daktari humpa vidonge vya kutuliza maimivu.Mzazi hushauriwa kumuangalia mtoto kwa karibu,maana mtoto huruhusiwa kula na kucheza mapema awezapo baada ya upasuaji. Ndani ya wiki 4 Mtoto haruhisiwi kupanda juu ya vitu na kufanya shughuli zinazo husisha nguvu na mvutano mkubwa wa misuli.Zinaweza kuumiza Sehemu ya kinena.Muogeshe baada ya siku mbili kutoka kwenye upasuaji.

Mtoto kuwa na uvimbe Sehemu ya upasuaji ni kawaida, Ila inabidi mzazi amuone daktari endapo mtoto atakuwa na homa, kuvuja damu na maimivu makali.Maana hizo ni changamoto za upasuaji.

Changamoto na madhara ya kuishi na ugonjwa bila tiba
Mtoto aneishi na ugonjwa wa ngiri maji mawasiliano bila kutibiwa,akiwa mtoto na mtu mzima kwa baadae kutokana na changamoto zinazoletwa na ugonjwa huo.

Madhara ya kimwili
Ngiri maji mawasiliano huweza kusababisha saratani ya korodani kwa baadae awapo mtu mzima.Kutokana na changamoto za neva katika cell za korodani.Inayo hatarisha uwezo uzazi kwa mwanaume.

Pia inasababisha kupata mshipa wa ngiri.Kwa sababu uwazi kwenye kinena unaweza kupitisha kiungo kama utumbo mdogo na kusababisha ngiri kutokea.Shughuli kama kunyanyua vitu vizito,kujikamua kwa nguvu wakati wa kujisaidia na kucheka kupitiliza kunapelekea msukumo kwenye uwazi huo.Na kupitisha viungo.

Madhara ya kisaikologia
Hata nitayahushisha Moja kwa Moja kupitia kwangu,kwa sababu nimezipitia. Kutaniwa na kucheka na watoto wenzake.Humsabisha mtoto kukosa amani na kujiskia chino.kutokana na utofauti uliopo kwenye mwili.kitu kinachoweza kuasili masomo yake shuleni.

Aibu ya kuingia kwenye mahusiano,akifikia umri sahihi unaoruhusu mahusiano na jinsi tofauti .Kwa sababu ya kuogopa mwenzi wake kugundua na kumkatilia.

Wasiwasi wa magonjwa mengine.Kama saratani,kwa sababu ngiri maji mawasiliano huhusishwa na saratani. Na katika haya ni muhimu mwanasaikologia kuhusika kuepusha msongo wa mawazo.

Kwa kumaliza ni kifanyike?
Wazazi wapewe elimu sahihi kuhusu ugonjwa huu.Ili Mama mjamzito aendapo kujifungua akikutana na tatizo Hilo kwa mtoto wake wa kiume.Ajue ni nini kinatakiwa kufanyika.Kuliko kuficha na kupuuzia.

Watu wazima kama Mimi tunao ishi na ugonjwa huu tupewe semina jinsi ya kupata tiba bila uwoga.Na kujua madhara katika uzazi kwa kujaa bila kupata tiba.

Serikali pia ifanye urahisi wa gharama na wataalamu kufanikisha matibabu ya ngiri maji mawasiliano na ngiri zingine zote.kuwapa Wazazi moyo wa kuwapeleka watoto kwa ajili ya upasuaji.

Tatizo Hilo halizuiliki, ila linatibika mzazi chukua hatua.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom