Ngoja nikwambie sasa, sisi wahuni wa miaka ya 90 na tulivyo sasa


Hapohapo kiwanda cha unga cha Nyati nyuma kulikuwa na uwanja na timu flani nimeisahau jina, jioni ni mwendo wa wahuni kuvuta bangi huku wakicheki mazoezi, sasa pita kuanzia saa 12 na nusu jioni uone utakavyokabwa
 
unenikumbusha tuliokuwa tunakaa kurasini
uwanja wa Ugimbi
na pia hapa kanisani ambako sasa kuna ofisi za Radio ya wapo
lakini pia keko uwanja wa KJ
hatari tupuuuuuu
kuna timu ilikua inaitwa Cyborg wanatokea keko
hatari tupuuu haoooo
ngumi mkononiii
 
Tupe mikasa yao....
 
R.I.P uncle jombi.
Mpwa wake nimehamishia ubabe kwenye Kusaka mapesa.
 
Oy uwanja wa Ugimbi bdo upo masta.?
Ni ile bar pale ndani uwanjani tulikuwa tunacheza disco toto back then bado ipo..?
 
Binafsi mm nlishakutana na jombi uso kwa uso mitaa ya soweto pale garage kwake wkt huo nlikuwa chali sanaa
Alafu mbeya mitaa ya nzovwe kulikuwa na jamaa mmja anaitwa Mike maisumbe alikuwa nunda sana makesi kibao vp yupo au maana kama akiwa Hai mpaka leo basi atakuwa kaokoka 😂

Ova
 
Kulikuwa na mbabe mmja hko anaitwa santana sjui yupo bd au uzee tayari

Ova
Yap Santana alikuwa na nyumba yake pale kwa mfuga mbwa,nami nimetoka muda mrefu sijui anaendeleaje,ila tulishawahi kukutana kwenye vurugu kati ya wavete wa pale manzese kwa wachonga visu dhidi ya Chicago ya manzese kwa mfuga mbwa ila timbwili halikutokea kwa kuwa wavete tulikuwa na support ya wahuni mpaka Mabibo na Mburahati ikabidi Santana na Chicago yake watulie tukayamaliza kwa makaratasi na wao kwenda kufuta kesi polisi Urafiki.
Nalog off
 
kwa mtazamo wangu, pamoja na yote, hapo (kwenye nyekundu) ndipo ilipo hoja kuu ya mtoa mada......nikitumia maarifa ya o'level ya uchambuzi wa kazi za kifasihi naona kabisa mtoa mada anasumbuliwa na aina ya maisha iliyopo sasa kwa vijana wetu;

mifumo ya maisha imebadilika badilika, imevurugwa vurugwa! hakuna ukakamavu wala kugangamala....vijana wamekuwa lainiiiiii, wanashindana na dada zao kutembea na vioo vya kujirembea kwenye vipochi na hatimae ushoga umetapakaa.....wajanja wa siku hizi ni wale wanaoweza kucheza video games vizuri au kuyaelezea mavazi ya kina diamonds vizuri, lakini si wale tena wanaofanya, angalau, mambo ya kishujaa.

watoto wa kiume sasa wanalindwa kama wanavyolindwa watoto wa kike maana ukishangaa tu utakuta wameraruliwa malinda, hawawezi hata kujitetea.....wako lainiiiiii. kijana wa kidato cha nne anagoma kwenda shule eti kisa mama yake hajamtumia hela ya kutumia shuleni.

kijana wa kidato cha nne anaomba ruhusa shule aende kwa mama yake ili akamshonee suruali yake iliyotatuka kidogo mapajani.


mnaokejeli uzi huu mmenishangaza sana!

ahsante sana mtoa mada, umenitafakarisha sana kuhusu yajayo ya vijana wetu hawa!!
 
Kj wavurana bango au si wavuta bangi ukuta wa kanisani apo.
 
Kipindi hicho chugaa kulikuwa na makonseti...cresto aka shimoni....Metropol...Arusha bye night...risk club....mechii za mashule naboishuu vs Arusha sec,soweto.bondeni na ilboru....makumira na Arusha day.achaa kabisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…