Ngoja niseme nanyi vijana wa leo

Ngoja niseme nanyi vijana wa leo

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Kwanza sio lazima niwasalimie maana nitapoteza muda tu...🤨

Ipo hivi.

Jukumu la mzazi wako ni kuhakikisha unakua na afya njema, unapata malazi na mavazi mazuri na kisha unapata elimu na maarifa ili ukawe mtu mbele za watu duniani.

Kazi ya mzazi wako sio kukutafutia mali na sio jukumu la mzazi kukupeleka kwenye mafanikio ambayo ni jukumu lako wewe mwenyewe na ndio maana alikuhudumia tangu utoto hadi umejifaham.

Lakini kwa fikra zako hizi wewe kijana, ipo siku utaiba then utawaachia wazazi wako msala kwamba wakafungwe jela badala yako kwasababu wao ndio walikuzaa..😂

Anywas,

Mimi hua nawaambia wanangu kwamba, mkimuona mwizi anauwawa tambueni huyo anawazazi wake na wakati wanamzaa hawakupanga mtoto wao aje kuwa mwizi.🤨

I'm done...☹️
 
Nini kimetokea aposto?
FB_IMG_17141612739174511.jpg
 
Mzazi mzuri huachia urithi watoto wake.
Mithali 13:22
Nb :elimu sio urithi

Pia mlee mtoto katika njia ifaayo naye hataicha kamwe.

So hapa tunaona ukimpa urithi yaani kianzio kinachoshikika mfano shamba, baiskeli nk huku ana maadili ya elimu na miiko uliyompatia lazima mtoto atafanikiwa.
 
"""Kazi ya mzazi wako sio kukutafutia mali na sio jukumu la mzazi kukupeleka kwenye mafanikio ambayo ni jukumu lako wewe mwenyewe na ndio maana alikuhudumia tangu utoto hadi umejifaham."""

Mkuu Ushimen mbona kuna wengine kila kukicha ni kutafutia nyumbani tu mpaka unajuta kwanini ni wa kwanza.

Maana wadogo zako wote macho kwako wewe.

Bado mzee

Bado bi mkubwa.

Halafu hapo hapo naambiwa kuwa kazi ya mzazi sio kukutafutia how ..?
 
Mzazi mzuri huachia urithi watoto wake.
Mithali 13:22
Nb :elimu sio urithi

Pia mlee mtoto katika njia ifaayo naye hataicha kamwe .

So hapa tunaona ukimpa urithi yaani kianzio kinachoshikika mfano shamba,baiskeli nk huku ana maadili ya elimu na miiko uliyompatia lazima mtoto atafanikiwa.
Daah kweli mkuu elimu sio urithi et
 
Kazi ya mzazi wako sio kukutafutia mali na sio jukumu la mzazi kukupeleka kwenye mafanikio ambayo ni jukumu lako wewe mwenyewe
Mimi naona kama mzazi anatakiwa afanye kadri ya uwezo wake,

Yawezekana mzazi ana uwezo wa kumpa mtoto mtaji mkubwa au kumrithisha mali nyingi....

Ni jambo jema.

Mtoto akishindwa kujiongeza akawa mwizi au mlevi na vitu kama hivyo, mzazi hatolaumiwa kwasababu amefanya kadri ya uwezo wake.
 
Back
Top Bottom