Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walalamike kwamba hawataki kulipa Kodi kwa kipato Chao au?Mtalalamika tu, na hakuna mtakacho wafanya.
Tunakumbushana tu, Hakuna mtu muoga kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana. 🤣🤣
Acha kufananisha uoga na vitu vya kijinga sometimes uoga ni akili watanzania ni mbaazi tu[emoji23][emoji23][emoji23]Acha kulinganisha kondoo na vitu vya kijinga. Kondoo ukimvuruga anakutia pembe/kichwa. Mtanzania hakuna kitu atafanya yeye ataishia kulalamika tu. [emoji1787] Huku anakamuliwa.
Sisi watanzania ni waoga sana, hata mimi ni muoga.
Pesa inakatwa ila mkataba utasoma elfu 40,000/= ili ikatwe ndogo wakati ni 4m, hii wote wenye leseni huwa wanakatwa wakienda TRA kukadiliwa kodi ya biasharaKwa mtindo huu watafanya wapangaji tupandishiwe Kodi. Mana mwenye nyumba hawezi kukubali pesa yake ikatwe asilimia hizo.
Hapa kuna wajinga wa chadomo wanataka kupotosha..Lakini Ni saws tu chumba TSH 60,000, mwenye nyumba anakula 54000/= TRA wanakula 6000/= very fair, Sasa hiyo Kodi itumike kupunguza (to subside) gharama za vifaa vya ujenzi.
Wasilipe kwa sababu wao ni kina nani hasa?Hiyo ni kwa Waswahili walala hoi weusi tu, apartments za Wahindi/Waarabu/Irani Oysterbay Upanga au Masaki hawatalipa hata shilingi, na wakigusa hapo mwisho wao umewadia, …
Ni vile serikali imezembea kufanya ufuatiliaji maana kuna nyumba nyingi Sana wanapangisha na hawalipi mapato.Nyumba za kupanga sio biashara rasmi sana ndio maana wengi hatujui...
Lakini kwa watu wenye fremu, apartments zenye leseni ya biashara huwa wanafanya withholding tax kwa niaba ya wapangaji...
Hivyo wewe mpangaji utaona umetoa kodi yako kama kawaida, lakini mwenye nyumba anarejesha 10% ya serikali huko 'tiaraei'...
Harafu wanadai huduma Bora za jamii nk wanadhani zinaletwa na mvua au? Ni Kodi tuu.Wananchi wanasahau kuwa nchi zinaendelea kwasababu ya kodi. Hatutakiwi kugomea kodi, tunatakiwa kupaza sauti kodi zetu zitumike vizuri kwa maendeleo yetu.
Hayo yote hasa la huduma za jamii inahitaji pesa,tulipe Kodi na tozo stahiki mambo yaende,ulalamishi hauwezi kusaidia.Kimfumo na kiuongozi Tanzania kutozesha wananchi ni wizi tu, bado hatuna demokrasia, katiba mbovu na mapungufu chungu nzima, huduma za kijamii ndio vituko, kutozesha watu kiasi hiki ni kufaidisha wachache...
Ni sawa na kuweka maji kwenye tenga, hizi tozo hazitasaidia chochote...
Sawa ila lipa Kodi ya pango mzeeWewe hata Kiswahili hujui.
Akipandisha kwani anayo nyumba peke yake hapa mjini?Hapo mwenye nyumba lazima apandishe kodi ili kuziba pengo matokeo yake ni maumimivu kwa sisi tusio na nyumba. Ila kwa jicho lenye kuona mbaaali, gharama za maisha zinaenda kupaa tena maana mpangaji nae atapandisha bei ya bidhaa au huduma atoaye kwa wengine ili kufidia ongezeko la pango.
Sauti ya akina nape iliyonaswa na Magufuli ndio inafaa kutumika awamu hii kuwa nchi inatawaliwa na ....
Wenye nyumba binafsi walikuwa na msamaha ila sasa wote watalipa..hiyo ilikuwepo mbona, sema wapangaji wa frem za biashara ndio tulikuwa tunalipa, wenye nyumba walikuwa watata na wengine wanaweka kabisa kwenye mikataba kuwa kodi yoyote inayohusiana na serikari itakuwa ni juu ya mpangaji... bado mpangaji atapigika tu sababu yeye ndo mwenye shida kubwa.
Kulingana na Mkataba wako kama unachaji kwa mwezi au miezi au mwaka..KHivi hii inatekelezekaje?..hiyo asilimia kumi ni kutoka kodi ya mwezi, miezi sita au mwaka?.
Kwamba kama kodi ni elfu hamsini na Mwenye Nyumba anataka miezi mitatu nikate elfu kumi na tano nipeleke TRA kisha nimletee Mwenye nyumba laki moja na thelathini na tano?.
Au la kama kanikubalia nilipe mwezi mmoja nipeleke elfu tano TRA nimpe mwenye nyumba elfu erobaini na tano?.
Na je namtaarifu kwanza Mwenye Nyumba au naenda TRA kinyemela?....na vipi kama nikimpa hiyo pungu akaikataa na kugoma kunipa mkataba TRA watanirudishia au nitatakiwa kuzunguka na hiyo elfu arobaini na tano mpaka nikipata chumba kingine?.
Kodi ya jengo yaani ni kwamba wewe uliyepanga au umejenga unalipia jengo kwenye ardhi ya serikali,pia kuna Kodi ya Ardhi kwa viwanja naashba yote ambayo yanatambulika na yana hati.Naomba kujua ile buku ya kila mwezi inayokatwa kupitia luku ni kodi ya nini?
Mpangaji unakuwa wakala.wa Kodi wa TRA,unakata mwenyewe na unapeleka kuilipa TRA.Hapa wangesema, ukilipa kodi unakata 10% witholding tax na katika hiyo 10 mpangaji unabaki na 4% kama bonus yako ili angalau tuwe mawakala wa faida. Yaani mimi niwe wakala wa TRA kukusanya hiyo 10% alafu nalipa nauli yangu kuioeleka TRA. Kwa huduma gani nzuri tunazopata kama wananchi?
Umeme utakuwa expensive Sana harafu kila nyumba ina Kodi tofauti sasa ukiweka flat sio sawa.Waiweke tena kwenye LUKU ili kuepusha kukimbizana kimbizana barabarani