Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

sasa kwenye sensa jidai unataka sifa ukiulizwa nyumba unataja zote ulizo nazo utanyonywa hadi mavi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nani kama mama jamani[emoji23][emoji23][emoji23], hakika Magufuli alikuwa raisi wa hovyo sana kuwaita wanyonge!!! Hakukusanya hata buku kwa wanyonge ila mama kaweza
Sukuma gang inakomeshwa!

Tunapumua..
 
Hahahahah hio TAX mi nikilala nazalisha nini hapo nyumbani? Nawasubiria kwa hamu na nimejiandaa kulala mahabusu safari hii!
We mkorofi tu, kujimwambafai ndio zako!
Umeambiwa ukate asilimia 10%kutoka kwenye pesa unayomlipa mwenye nyumba, sasa wewe mpangaji kinachokuuma ni kipi hapo!?
 
KODI NYINGI HULIPWA JANUARI NA JULY, KWA KIPINDI HIKI ELIMU ITOLEWE KWANZA.
::ushauri::
NASHAURI IPUNGUZWE IWE 7%.
 
With holding tax hulipwa na anayefanya malipo, yaani kwa lugha nyingine ni kama anakuwa wakala wa TRA...

Anazuia hiyo 10% ya malipo ya pango, na anapaswa kuireturn TRA...
Hata PAYE ni withholding tax , mwajiri anakukata halafu anaiwasilisha TRA.
 
Hivi afisa wa TRA akitamka jambo ndiyo linakuwa tamko la TRA na serikali kwa ujumla? au anayepaswa kutampa tamko mpaka ikaonekana ni TRA/serikali si kamishna mkuu wa TRA?
 
Hahahahah hio TAX mi nikilala nazalisha nini hapo nyumbani? Nawasubiria kwa hamu na nimejiandaa kulala mahabusu safari hii!
Usiseme hivo jirani kwani ukilipa kwa kutengeneza hiyo mikanda utapata shida gani wewe toa tu.Nchi ni yetu sote na Maendeleo ni yetu
 
Hiyo kodi mpangaji ndiye atakayeumia. Mwenyenyumba anakuongezea kodi tu ili ipatikane ya TRA chake kinabaki palepale
 
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi kupitia Ukurasa wake wa Instagram, imeeleza kuwa;

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesisitiza wapangaji kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.

Akiwa katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022 wilayani Bariadi, Ofisa huduma na elimu mkuu kutoka TRA, Eugenia Mkumbo amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kodi kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba" amesema Eugenia.

My take
Awamu ya sita inazidi kuupiga mwingi na kuleta furaha katika mioyo na nyuso za watanzania, ama kwa hakika watanzania Mungu awape nini tena ? manataka Rais wa aina gani nyie? nchi inasonga mbele kwa kasi Tozo zinajenga nchi ,matumizi yamebanwa , pesa haziibiwi, mafisadi yamebanwa, raha sana

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2022, imeanza kusimamia sheria inayowapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

=======
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesisitiza wapangaji katika nyumba za kapanga kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.

Hayo yamesemwa na Ofisa Huduma na Elimu Mkuu wa TRA, Eugenia Mkumbo katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022, leo Alhamisi Agosti 25, 2022 wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kodi kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi, hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi, utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba," amesema Eugenia

Aidha, amesema Serikali imefuta kodi kwa wanafunzi wanaokwenda kupata mafunzo ya vitendo kwa lengo la kuwarahisishia waajiri kuwapa nafasi ya kupata uzoefu wa kazi kwa urahisi wanafunzi wanaohitimu masomo.

Akifafanua kuhusu kodi ya pango, Kissa Kyejo, Afisa Mkuu Usimamizi wa Kodi amesema mfanyabiashara ni mbia wa Serikali na anapaswa achangie kipato unachopata kwa kulipa kodi.

"Yule mwenye nyumba anapata kipato kwa sababu analipwa na wapangaji lakini TRA tunaweza tusimfikie mwenye nyumba kwa sababu hana namba ya utambulisho wa mlipa kodi.

“Pengine amejenga nyumba na sio mfanyabiashara sheria, ilichofanya ni kwamba mpangaji ambae ndie anamlipa mwenye nyumba kipato aweke zuio na kulipa kodi ya pango," amesema

Baadhi ya wapangaji katika mji wa Bariadi, wamesema kodi hiyo ni kama mgogoro kati ya wenye nyumba na wapangaji kwa sababu ni kazi ngumu kumlipia kodi mtu ambaye hajaamua kulipa kodi kwa hiari.

"Kabla ya kumpa mamlaka mpangaji kuzuia hela ya pango ili kulipa kodi, wangewaita wenye nyumba na kuwapa elimu ili wawe tayari kukatwa pesa zao lakini saizi itakuwa ni changamoto sana kwa sababu wengi hawajui hata hiyo kodi inahusu nini," amesema John Lucas mkazi wa Kidinda.

Chanzo: Mwananchi
Hapa itatafutwa kila namna watu wakatwe pesa bila kujari umepanga au haujapanga!
 
We mkorofi tu, kujimwambafai ndio zako!
Umeambiwa ukate asilimia 10%kutoka kwenye pesa unayomlipa mwenye nyumba, sasa wewe mpangaji kinachokuuma ni kipi hapo!?
Kinachoniuma ni kuwa mwenye nyumba hawezi kubali uondoe hio 10% kwenye kodi yake
 
Mtanzania hakuna kitu atafanya yeye ataishia kulalamika tu. 🤣 Huku anakamuliwa.
🐄
images (95).jpeg
 
Back
Top Bottom