Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Naomba kujua ile buku ya kila mwezi inayokatwa kupitia luku ni kodi ya nini?
Ile ni kodi ya kuisaidia serikali katika shughuli zake ama kwa jina lingine inaitwa kodi ya uzalendo kwa wananchi
 
Nadhani kwanza viwanja vingepimwa bure na kutolewa hati bure ndipo kodi zirudi kwa mfumo huo, nyumba zenyewe hazijabainishwa Zipi na ziko wapi nani mmiliki kisha zoezi ndio lianze
 
Mfano Chumba cha 30,000 ikatwe 3,000 ibaki 27,000. Duh, sasa wapangaji watakuwa mabosi kuwakata wenye nyumba hela.

Ila ili ibaki hela anayotaka mwenye nyumba, itabidi kodi zipande mpaka 33,500.

Tutaelewana tu, mwenye nyumba hatakubali apate pungufu na kiwango alichopanga.
 
Mwenye nyumba ndio mwenye jukumu la kulipa maana hapo kwenye kiasi cha Kodi unachomlipa mwenye nyumba inakatwa 10% na Kwa msingi huo lazima kuwe na makubaliano ya kwenye Mkataba wa upangishaji..
Makubaliano yapo wazi, aailimia kadhaa zitaongezeka kwenye kodi ili mwwnye nyumba apate kodi aliyoipanga.
 
Vifaa wakati wa kujenga nyumba vililipiwa kodi,nyumba baada ya kukamilika nakatwa elfu moja kila mwezi kila nikinunua umeme.

Umepata mpangaji nikwatwe 10% ya pango. Nasema huo ukhanithi sifanyi wanajua nilipo pata pesa ya kujengea hiyo nyumba?
 
Jengeni nch yenu acheni kulia lia
Wao wanaozikupokea ndiyo wajenge nchi kwa kuzisimamia fedha vizuri
Waache matumiz mabovu,matumizi ya anasa....wafanye vitu mwananchi akiona , mwisho wa siku anasema kweli kodi znatumika vizuri

Ova
 
Hahahahah hio TAX mi nikilala nazalisha nini hapo nyumbani? Nawasubiria kwa hamu na nimejiandaa kulala mahabusu safari hii!
Nilivyoelewa Mimi ni Kodi anayopaswa kulipa mwenye nyumba lakini wewe wakati unalipia Kodi ya nyumba unapaswa kukata asilimia kumi uiwasilishe TRA.

Kwa hiyo anayelipa ni mwenye nyumba si mpangaji
 
Nilivyoelewa Mimi ni Kodi anayopaswa kulipa mwenye nyumba lakini wewe wakati unalipia Kodi ya nyumba unapaswa kukata asilimia kumi uiwasilishe TRA.
Kwa hiyo anayelipa ni mwenye nyumba si mpangaji
Hapo sawa
 
Back
Top Bottom