Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Acha kulinganisha kondoo na vitu vya kijinga. Kondoo ukimvuruga anakutia pembe/kichwa. Mtanzania hakuna kitu atafanya yeye ataishia kulalamika tu. 🤣 Huku anakamuliwa.


Sisi watanzania ni waoga sana, hata mimi ni muoga.
Hahahaha kondoo mstarabu kweli kweli ila hapendi kabisaa kitu kinachoitwa upumbavu kwake.
 
Kwwni ile inakatwa kupitia LUKU ni nini?
Ile ni kodi ya jengo ambayo kila mwenye nyumba anatakiwa kulipa na hii ni kodi ya zuio ambayo ni 10% ya kodi anayolipwa mwenye nyumba ya kupangisha.
 
Ile ni kodi ya jengo ambayo kila mwenye nyumba anatakiwa kulipa na hii ni kodi ya zuio ambayo ni 10% ya kodi anayolipwa mwenye nyumba ya kupangisha.
Dah,ngoja nikayajenge na landlord kwanza
 
Okay, ni jambo zuri. Lakini kwa upande wangu ningemuomba rais akemee kwa wapangishaji kututoza kodi kubwa, nyumba ya laki nne atleast iwe nusu yake, nyumba ya laki tatu atleast iwe nusu yake. Naiomba serikali itufikirie kwenye hili pia.
Haiwezekani mkuu na hili swala la kupanda gharama za Maisha ndo balaa kabisa.
 
Hii ndio Taarifa mpya iliyosambazwa na vyombo vya habari vya Tanzania siku ya leo , Kwamba nyie Wapangaji wa majengo ya kuishi ama ya biashara kaeni tayari kwa hiyo Tozo mpya inayokuja hivi karibuni , Kwamba kwenye hicho kitita unachomlipa mwenye nyumba basi piga hesabu ya 10% uipeleke TRA .

Usije kusema hatukukuambia .

Mungu ibariki Tanzania
 
hiyo ilikuwepo mbona, sema wapangaji wa frem za biashara ndio tulikuwa tunalipa, wenye nyumba walikuwa watata na wengine wanaweka kabisa kwenye mikataba kuwa kodi yoyote inayohusiana na serikari itakuwa ni juu ya mpangaji... bado mpangaji atapigika tu sababu yeye ndo mwenye shida kubwa.
 
Back
Top Bottom