Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Withholding tax, kumbe kulikuwa na msamaha kwa wapangaji binafsi. Kwenye biashara tushazoea kulipa hio. Tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa.
Nyingine hii huku.
Screenshot_20220825-140403.jpg
 
Nyumba za kupanga sio biashara rasmi sana ndio maana wengi hatujui...

Lakini kwa watu wenye fremu, apartments zenye leseni ya biashara huwa wanafanya withholding tax kwa niaba ya wapangaji...

Hivyo wewe mpangaji utaona umetoa kodi yako kama kawaida, lakini mwenye nyumba anarejesha 10% ya serikali huko 'tiaraei'...
Hata nyumba za biashara wewe mpangaji ndio unapeleka kodi ya zuio tra. Ndio maana mkataba wa pango lazima uupeleke tra wakakufanyie hesabu za stamp duty na hio withholding tax.
 
Hata nyumba za biashara wewe mpangaji ndio unapeleka kodi ya zuio tra. Ndio maana mkataba wa pango lazima uupeleke tra wakakufanyie hesabu za stamp duty na hio withholding tax.
Wape elimu wape elimu

Lipa kodi kwa maendeleo ya taifa

Ova
 
Sasa nawasilishaje kodi ambayo nimeilipa kabla ya sheria kutungwa?

Yani ni sawa na wewe wakuambie ulipie 10% yq miaka yote ambayo umeishi kwenye nyumba ya kupanga
Utawasilisha ya mwaka husika.
 
Mimi naona hapo wanaopanga watazidi kuumia tu,kitakachofanyika ni hivi,tuseme kodi ya nyumba ilikuwa laki 5 mwenye nyumba atapandisha iwe 5.7 ili ukitoa 10% ile tano yake iendlee kubaki pale pale...
 
Kimfumo na kiuongozi Tanzania kutozesha wananchi ni wizi tu, bado hatuna demokrasia, katiba mbovu na mapungufu chungu nzima, huduma za kijamii ndio vituko, kutozesha watu kiasi hiki ni kufaidisha wachache...
Ni sawa na kuweka maji kwenye tenga, hizi tozo hazitasaidia chochote...
 
Okay, ni jambo zuri. Lakini kwa upande wangu ningemuomba rais akemee kwa wapangishaji kututoza kodi kubwa, nyumba ya laki nne atleast iwe nusu yake, nyumba ya laki tatu atleast iwe nusu yake. Naiomba serikali itufikirie kwenye hili pia.
 
Back
Top Bottom