Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Mimi naona hapo wanaopanga watazidi kuumia tu,kitakachofanyika ni hivi,tuseme kodi ya nyumba ilikuwa laki 5 mwenye nyumba atapandisha iwe 5.7 ili ukitoa 10% ile tano yake iendlee kubaki pale pale...

Mimi sioni faida yoyote kwa mpangaji ukizingatia anaefaidika hapo ni mpangishaji na serikali tu. Wa kufurahia hapo ni serikali na sio mpangaji 😁
 
Okay, ni jambo zuri. Lakini kwa upande wangu ningemuomba rais akemee kwa wapangishaji kututoza kodi kubwa, nyumba ya laki nne atleast iwe nusu yake, nyumba ya laki tatu atleast iwe nusu yake. Naiomba serikali itufikirie kwenye hili pia.
Namuoombaaaa waziriiiiii aliaaangalieee na hiloooo
 
Withholding tax, kumbe kulikuwa na msamaha kwa wapangaji binafsi. Kwenye biashara tushazoea kulipa hio. Tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa.
Hii ni kweli lakini mwenye nyumba gani atakubali umkate hiyo 10%? Kwenye biashara tunafanya sababu tunaingiza na kuogopa notes. Huu mzigo mwingine kwa raia.
 
Ni kuwapa wapangaji mizigo ya ziada.
Hela ya dalali ya mwezi mmoja analipa mpangaji na hela anayotakiwa kukatwa TRA mwenye nyumba analipa mpangaji, hela ya Kodi ya nyumba analipa mpangaji.
Tusio na nyumba tunapitia wakati mgumu sana ( Tunaomba MUNGU atusaidie kwa namna ya pekee).
 
PAYE--inaenda Benki inakwatwa Service charge za Bank- Bank nayo inakulima VAT- unaenda kuchukuwa benki kwa matumizi yako unakutana na Tozo aka Goverment Levy, unanuna vocha unalimwa Tozo, unaenda kulipa kodi ya pango unalimwa Withholding Tax ... Haki ya Mungu kilimo ndiyo kazi nzuri ambayo mkulima ukivuna unakula direct bila kupitia TRA kujipendekeza kwetu kwenda kuuza ndiyo kinachotuponza... Ila tukirudi kwenye biashara ya kubadirishana kitu kwa kitu hatutakuwa tunalalamika hivi
 
Mwenye nyumba ndio alipe sio mpangaji! Hizo sheria kandamizi wanazojitungia tungia tu zitawafikisha mahali fulani maana hazitekelezeki
Eti mpangaji atoke nyumbani, alipie usafiri hadi TRA, aunge foleni kulipa withholding tax. Hizo gharama zake atalipwa na Nani,?!

Kama ni uzalendo na wao waache kutumia Ma-vieit mjini wapande Harrier!
 
PAYE--inaenda Benki inakwatwa Service charge za Bank- Bank nayo inakulima VAT- unaenda kuchukuwa benki kwa matumizi yako unakutana na Tozo aka Goverment Levy, unanuna vocha unalimwa Tozo, unaenda kulipa kodi ya pango unalimwa Withholding Tax ... Haki ya Mungu kilimo ndiyo kazi nzuri ambayo mkulima ukivuna unakula direct bila kupitia TRA kujipendekeza kwetu kwenda kuuza ndiyo kinachotuponza... Ila tukirudi kwenye biashara ya kubadirishana kitu kwa kitu hatutakuwa tunalalamika hivi
Bado ukienda kanisani kuna

Kodi ya Sadaka
Kodi ya Kujimaliza
Kodi ya kueneza Injili
Kodi ya Ujenzi
Kodi ya Ukombozi
Kodi ya Fungu la kumi
Kodi ya mafuta ya upako
Kodi ya shukrani
 
Anakatwa mwenye nyumba ila wewe mpangaji ndio mkusanyaji, ila kiuhalisia mwenye nyumba anakupandishia kodi tu kufidia.
Hivi Ile Kodi ya jengo kwenye luku nayo naona Kama Kodi zinakua Mara mbili mbili
 
Hapo mwenye nyumba lazima apandishe kodi ili kuziba pengo matokeo yake ni maumimivu kwa sisi tusio na nyumba. Ila kwa jicho lenye kuona mbaaali, gharama za maisha zinaenda kupaa tena maana mpangaji nae atapandisha bei ya bidhaa au huduma atoaye kwa wengine ili kufidia ongezeko la pango.

Sauti ya akina nape iliyonaswa na Magufuli ndio inafaa kutumika awamu hii kuwa nchi inatawaliwa na ....
 
Hivi Ile Kodi ya jengo kwenye luku nayo naona Kama Kodi zinakua Mara mbili mbili
Kodi ni nyingi sana, lakini bila kodi maendeleo yatatoka wapi? Tupambane tu kuhakikisha kodi zetu zinatumika vizuri.
 
Back
Top Bottom