Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Kwa mtindo huu watafanya wapangaji tupandishiwe Kodi. Mana mwenye nyumba hawezi kukubali pesa yake ikatwe asilimia hizo.
 
Acha kulinganisha kondoo na vitu vya kijinga. Kondoo ukimvuruga anakutia pembe/kichwa. Mtanzania hakuna kitu atafanya yeye ataishia kulalamika tu. [emoji1787] Huku anakamuliwa.


Sisi watanzania ni waoga sana, hata mimi ni muoga.
Acha kufananisha uoga na vitu vya kijinga sometimes uoga ni akili watanzania ni mbaazi tu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa mtindo huu watafanya wapangaji tupandishiwe Kodi. Mana mwenye nyumba hawezi kukubali pesa yake ikatwe asilimia hizo.
Pesa inakatwa ila mkataba utasoma elfu 40,000/= ili ikatwe ndogo wakati ni 4m, hii wote wenye leseni huwa wanakatwa wakienda TRA kukadiliwa kodi ya biashara
 
Lakini Ni saws tu chumba TSH 60,000, mwenye nyumba anakula 54000/= TRA wanakula 6000/= very fair, Sasa hiyo Kodi itumike kupunguza (to subside) gharama za vifaa vya ujenzi.
Hapa kuna wajinga wa chadomo wanataka kupotosha..

Kwanza serikali ingefanya tathmini ya nyumba zote za kupangisha ili walipe Kodi maana miaka mingi wamekuwa wakikwepa hii Kodi.
 
Ni vile serikali imezembea kufanya ufuatiliaji maana kuna nyumba nyingi Sana wanapangisha na hawalipi mapato.
 
Wananchi wanasahau kuwa nchi zinaendelea kwasababu ya kodi. Hatutakiwi kugomea kodi, tunatakiwa kupaza sauti kodi zetu zitumike vizuri kwa maendeleo yetu.
Harafu wanadai huduma Bora za jamii nk wanadhani zinaletwa na mvua au? Ni Kodi tuu.
 
Mi nashangaa sana sijui kwa nini watu wanapumua bure hadi sasa, itabidi serikali iweke tozo ya kupumua kwenye hewa ya anga la Tanzania, mama anaupiga mwingi sana
 
Hayo yote hasa la huduma za jamii inahitaji pesa,tulipe Kodi na tozo stahiki mambo yaende,ulalamishi hauwezi kusaidia.
 
Akipandisha kwani anayo nyumba peke yake hapa mjini?

Kwanza Tanzania real estate haijaendelea kivile ila ikikua lazima serikali itaunda regulatory authority..
 
Hivi hii inatekelezekaje?..hiyo asilimia kumi ni kutoka kodi ya mwezi, miezi sita au mwaka?.

Kwamba kama kodi ni elfu hamsini na Mwenye Nyumba anataka ya miezi mitatu, mimi nikate elfu kumi na tano nipeleke TRA kisha nimletee Mwenye nyumba laki moja na thelathini na tano?.

Au la kama kanikubalia nilipe mwezi mmoja nipeleke elfu tano TRA nimpe mwenye nyumba elfu erobaini na tano?.

Na je namtaarifu kwanza Mwenye Nyumba au naenda TRA kinyemela?....na vipi kama nikimpa hiyo pungufu akaikataa na kugoma kunipa mkataba TRA watanirudishia elfu tano yangu au nitatakiwa kuzunguka na hiyo elfu arobaini na tano mpaka nikipata chumba kingine?.
 
Wenye nyumba binafsi walikuwa na msamaha ila sasa wote watalipa..

Natoa wito kwa serikali kuwatafuta wote wenye nyumba za kupangisha mtaani Ili walipe Kodi,saizi watakwepa ila sensa itawaumbua maana hilo swali lilikuwepo.
 
Kulingana na Mkataba wako kama unachaji kwa mwezi au miezi au mwaka..

TRA ikitambua nyumba zote zenye wapangaji itaweza.
 
Hapa wangesema, ukilipa kodi unakata 10% witholding tax na katika hiyo 10 mpangaji unabaki na 4% kama bonus yako ili angalau tuwe mawakala wa faida.

Yaani mimi niwe wakala wa TRA kukusanya hiyo 10% alafu nalipa nauli yangu kuioeleka TRA. Kwa huduma gani nzuri tunazopata kama wananchi?
 
Naomba kujua ile buku ya kila mwezi inayokatwa kupitia luku ni kodi ya nini?
Kodi ya jengo yaani ni kwamba wewe uliyepanga au umejenga unalipia jengo kwenye ardhi ya serikali,pia kuna Kodi ya Ardhi kwa viwanja naashba yote ambayo yanatambulika na yana hati.
 
Mpangaji unakuwa wakala.wa Kodi wa TRA,unakata mwenyewe na unapeleka kuilipa TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…