Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23]utajua tu,ukiona zile lc300 model utajua tu Zina enda wap,we Rudi jukwaa la kimasihara tuburudishe stress zitutoke.hizi tozo kama kuna mtu anajua zinaenda wapi naomba aniambiee
ahahaa.. sensa ni siriii.Wenye nyumba binafsi walikuwa na msamaha ila sasa wote watalipa..
Natoa wito kwa serikali kuwatafuta wote wenye nyumba za kupangisha mtaani Ili walipe Kodi,saizi watakwepa ila sensa itawaumbua maana hilo swali lilikuwepo.
🤣🤣Mkuu usipokuwa makini Unaweza fungwa jela maisha!unapobishana na sirikali lazima uwe umeandaa nauli ya kuvuka mipaka ya nchi.Hahahahah hio TAX mi nikilala nazalisha nini hapo nyumbani? Nawasubiria kwa hamu na nimejiandaa kulala mahabusu safari hii!
Na wakubwa ndio wameshahamisha magoli hivyo,wametuchonganisha tuparurane wenyewe.Kinachoniuma ni kuwa mwenye nyumba hawezi kubali uondoe hio 10% kwenye kodi yake
vitofa vya kichwa vitawahusu🤣🤣🤣🤣🤣Mzee watakula vitofa au?
yajayo yanafurahishakabisa
Kwenye suala la mpangaji bado elimu inahitajika sana, kinachokwenda kutokea ni housing rent to sky rocketMzigo unakwenda kwa mpangaji, kwamfano, mimi nataka mpangaji anilipe 100K kwa mwezi, kwa sheria hii nitalipwa 90K, ili kumentain 100K yangu nitampandishia kodi na kuwa 110K
Wana paswa pia wawajulisbe na wenye nyumba zao piaKwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi kupitia Ukurasa wake wa Instagram, imeeleza kuwa;
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesisitiza wapangaji kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.
Akiwa katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022 wilayani Bariadi, Ofisa huduma na elimu mkuu kutoka TRA, Eugenia Mkumbo amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kodi kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.
"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba" amesema Eugenia.
My take
Awamu ya sita inazidi kuupiga mwingi na kuleta furaha katika mioyo na nyuso za watanzania, ama kwa hakika watanzania Mungu awape nini tena ? manataka Rais wa aina gani nyie? nchi inasonga mbele kwa kasi Tozo zinajenga nchi ,matumizi yamebanwa , pesa haziibiwi, mafisadi yamebanwa, raha sana
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2022, imeanza kusimamia sheria inayowapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.
=======
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesisitiza wapangaji katika nyumba za kapanga kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.
Hayo yamesemwa na Ofisa Huduma na Elimu Mkuu wa TRA, Eugenia Mkumbo katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022, leo Alhamisi Agosti 25, 2022 wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kodi kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi, hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.
"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi, utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba," amesema Eugenia
Aidha, amesema Serikali imefuta kodi kwa wanafunzi wanaokwenda kupata mafunzo ya vitendo kwa lengo la kuwarahisishia waajiri kuwapa nafasi ya kupata uzoefu wa kazi kwa urahisi wanafunzi wanaohitimu masomo.
Akifafanua kuhusu kodi ya pango, Kissa Kyejo, Afisa Mkuu Usimamizi wa Kodi amesema mfanyabiashara ni mbia wa Serikali na anapaswa achangie kipato unachopata kwa kulipa kodi.
"Yule mwenye nyumba anapata kipato kwa sababu analipwa na wapangaji lakini TRA tunaweza tusimfikie mwenye nyumba kwa sababu hana namba ya utambulisho wa mlipa kodi.
“Pengine amejenga nyumba na sio mfanyabiashara sheria, ilichofanya ni kwamba mpangaji ambae ndie anamlipa mwenye nyumba kipato aweke zuio na kulipa kodi ya pango," amesema
Baadhi ya wapangaji katika mji wa Bariadi, wamesema kodi hiyo ni kama mgogoro kati ya wenye nyumba na wapangaji kwa sababu ni kazi ngumu kumlipia kodi mtu ambaye hajaamua kulipa kodi kwa hiari.
"Kabla ya kumpa mamlaka mpangaji kuzuia hela ya pango ili kulipa kodi, wangewaita wenye nyumba na kuwapa elimu ili wawe tayari kukatwa pesa zao lakini saizi itakuwa ni changamoto sana kwa sababu wengi hawajui hata hiyo kodi inahusu nini," amesema John Lucas mkazi wa Kidinda.
Chanzo: Mwananchi
Wanawaambia wapangaji tu,hawa wanataka kugombanisha wapangaji na wenye nyumba[emoji23]Wana paswa pia wawajulisbe na wenye nyumba zao pia