Ngoma mpya ya Ali Kiba ''Mvumo wa Radi''; Maoni na ushauri

Ngoma ni nzuri inachezeka. Ila pale alipoweka igizo sijui what is your name kanikera. Ndo uko unacheza sasa unasimama wamalize kuulizana au??
Ile ni video...kwenye audio ndo hakuna hiyokitu...hata wasanii wakubwa huwa wanafanya hivyo...wakina rihanna..rick rose,dj khaleed etc...say my name baby.....!!
 
mi nataka nimfaham yule jamaa aliyebonga kizungu na kucheeeeeekaaa..!
Wale wateja wa dstv tutakuwa tunamjua huyu jamaa kabla ya mechi,mapunziko na mwisho wa game lazima tumuone akiishangilia cha lake la majogoo...
 
Haaha tuiskilize tu "nobody is safe"[emoji445] [emoji445] [emoji445]
Ndio ndio "nobody is safe"

Ali aliwahi kusema yeye ni kipenzi cha watu "Ali ni kipenzi cha watu"

Ila muziki wa bongo unavituko hakyanani...huku Team kiba huku team Mond
 
Nimeisikiliza nyimbo hii zaidi ya mara tano. Ni wimbo wa kawaida sana ila kwasababu umeimbwa na Ali Kiba basi naamini utakuwa mkubwa. CMG wote wamejipanga kuanzia asubuhi kuhakikisha wanamuinua.

Nitarudi badae na maoni yangu...
WASAFI TV WATAUINUA! PROMO WATAPATA KALI!
 
mziki mzuri kabisa ...wameshazoea manyimbo yao ya matusi matusi "" alikiba anawaimbia mziki watu wanaojielewa "" wanaojiheshimu na kuuthamini utu wao "" so kwa sisi ma gentleman ngoma tumeilewa aisee...""
Hata mavazi safi kabisa
Well done king
 
Wimbo Classic kwa watu Classic.... sasa kama unashangilia singeli hapa lazima pawe pazito kwako. lol

Live Long King Kiba.
 
Mwambie Jamaa aionee huruma lugha adhimu ya Kiswahili..
Jamaa linaharibu lugha eti "craudz"
Imagine jama yupo uhamiaji ndo anasajili passport..si anakuharibia jina uyo!
Clouds ni kiswahili!!???


Never knew that. lol
 
Masaa 38 viewers laki 7[emoji10][emoji3][emoji3][emoji3][emoji2] mond tunaomba saport najua ukiamuru virs milion ndan ya dakika tu inakuwa
 
Nyimbo nzuri na kubwa sana ila kizazi cha Instagram hawataielewa.

Alikiba amekua sasa he is a gentleman mziki wake na interviews zake clouds TV and radio zimedhihirisha.

Ila vijana wanaopenda kusikiza udaku na scandles za personal life wanaponda mpaka interviews eti ziliboa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…