Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli


Kwa hio kwa sababu tuliharibu selous tuharibu na ngorongoro ?
Kucontrol watu ni kazi ngumu sanaa bora wapewe eneo jingine wahame.
Mbna watu wanapisha ujenzi wa miundombinu kila siku kwani wao maasai ni kina nani hadi wasihame ?
 
Ila nikiisoma hii post ninazidi kuamini kwamba hela inatafutwa haswa
 
Watu ni wa ajabu sana ...yaani wanazungumzia watu wameongezeka sana lakini wanashau na wanyama wameongezeka maradufu na wanaolinda hao wanyama ni jamii ya kifugaji.kama kuna wavamizi ambao siyo jamii ya wafugaji waondolewe...hivi binadamu na wanyama wanaoishi pamoja sio kivutio cha utalii?
 
Wewe unapaelewa vizuri kabisa.
Wapo wengi wanajadili hili suala bila hata kuijuia Ngorongoro wala wakazi wake.
Mimi ni mhifadhi huru. Na eneo tajwa ni miongoni mwa maeneo nimefanya kazi na kupata uzoefu mkubwa na hisia mchanganyiko.
Ni hivi: NGORONGORO inakufa kwa mengi.
Na zisipofanyika jitihada za makusudi kuendeleza uhifadhi mle ndani tutapoteza ikolojia muhimu sana pamoja na kipokwa sifa zote tulizo nazo kwenye utalii.
Tufikirie kuhusu:
  • Kudhibiti idadi ya ng'ombe.
  • Kudhibiti idadi ya watu.
  • Kudhibiti makazi na shughuli za watu.
  • Kudhibiti ujenzi wa hoteli na kambi za kitalii.
Aidha nitoe tu angalizo: kwa tabia zetu hizi za kutokujali uhifadhi wa mazingira huko mbele ya safari tutaendeleza harakati za kugombania access ya maeneo nyeti kwenye uhifadhi.
 
Wewe ni mjinga kama Kitenge. Toka lini Ngorongoro inapata mvua kidogo mwaka mzima? Ngorongoro ni ukanda wa juu unaopata mvua sawia kila mwaka. Tena mvua nyingi kuliko sehemu nyingi nchini.

Hatua ya kwanza iwe ya kuivunja hiyo NCAA mnayoitumia kujitajirisha kwa kufisadi na kujilipa posho kubwa kubwa.
Eneo likabidhiwa kwa TANAPA ili iwe national park. Utalii wa utamaduni umekwisha. Eneo la NCA liwe mbuga ya Taifa chini ya Tanapa kama ilivyo Serengeti, Tarangire au lake Manyara.
 
Kwani wewe wanyama pori wanakusaidia nini. Wapambanieni wazungu kwani kuhifadhi mlipanga mlipangiwa.
 
Wanabodi JF!,

Nawasalimia popote pale mlipo!
Naomba niende kwenye Mada hii kuhusu NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY.(NCAA).
Njoo uchukue teni,wanyama kukaa na binadamu mnaona ajabu wakti wamekaa nao enzi na enzi...tarangire wanyama yanakaa na watu miaka,minjingu pundamilia wanashinda kwenye makazi ya watu na kuku hamshangai...tunajua macho kumchuzi anataka kuwapa OBC eneo zaidi pia yeye na waarabu wa granmelia wanataka kujenga hotel
 
Umeongea point ya msingi sana "ku-control namba ya watu na mifugo" na nadhani hili ndilo litakalofanyika na NCAA wameanza wao kama wao kuchukua hatua ya kuhamisha ofisi na makazi kupeleka karatu. Hatua itakayofuata nadhani ni kupunguza idadi ya wamasai walioko ndani ya hifadhi na siyo kuwahamisha wote maana wamasai wana haki ya asili na kisheria ya kuwa kule.

Hifadhi imeharibika sana na ujenzi wa nyumba za tofali na bati umeongezeka kwa kasi.
 
Hiyo nembo inamaana gani?

View attachment 2113934

Ni sahihi kabisa maoni yako kuhusu nembo.
Lakini mambo yamebadilika, hali zimebadilika, watu wamebadilika n.k. sasa kwa nini na sisi tusiende kulingana na mabadiliko hayo?? Hiyo nembo siyo msaafu (ambayo imeandikwa ukithubutu kubadilisha chochote kwenye hiyo, utapewa mapigo kulingana na ulichofanya) inaweza ikabadilishwa. Ukweli ni kuwa watu wanazaliana na kuongezeka sana. Pia desturi za wanaoishi kule ndani wanaenda kuchukuana hata wengine kutoka nchi jirani. Kuna siku nimeona hapa JF mpaka nyumba za bati zimejengwa kwenye hifadhi.
 
A man himself !!

wewe Ni mtu muhimu Sana,. Ngorongoro inakuhitaji Ni wakati wako wa kuitetea sasa
 
Waacheni masai waishi maeneo yao ya asili bhana, kama vipi hamishieni hao wanyama serengeti, selous au mikumi nchi hii imejaa hifadhi kila mahali............hivi ni nani anatakiwa kupewa kipaumbele kati ya binadamu na mnyama kuishi mahali?
 
Kama wakipatiwa huduma zote za kijamii basi ujue Neno la hifadhi litakufa kabisaa... wakati mnajua toplist ya nchi zinaongiza kwa utalii duniani, tanzania nayo imekuwa ya kwanza kwahyo kwa mimi nachoomba wamasai waendelee kujirecord na tik tok watoboe maisha waache kuwinda wanyama na kugoma kutoka kwenye hifadhi
 
Swala la Ngorongoro liko wazi kabisa.kua jamii ya wafugaji wanapaswa kuondoka eneo la hifadhi .Kinacholeta huu msuguano ni serikali yenyewe kutaka vyote vyote.Serikali inapokosa kauli moja thabiti ndo kunapelekea hizi siasa uchwara zinazoendelea sasa.Na hii danadana imeanza kitambo sasa serikali isipokaa chini nakuchukua hatua sasa hivi kukiwa bado na hili vuguvugu iko siku tutajutia.
 
Waacheni masai waishi maeneo yao ya asili bhana, kama vipi hamishieni hao wanyama serengeti, selous au mikumi nchi hii imejaa hifadhi kila mahali............hivi ni nani anatakiwa kupewa kipaumbele kati ya binadamu na mnyama kuishi mahali?
Kwani ni lazima binadamu aishi porini?.Kila kitu kinategemeana ndo maana vikawepo.Uharibifu wa mazingira utakapokithiri hata binadamu atakua hatarini.kwahiyo kama binadamu anayejielewa lazima tubalance haya mambo.Binadamu ni mhimu ila pia ni mnyama mwaribifu ndo maana tukawekeana sheria.tukisema kwasababu ni binadamu aachwe tu iko siku futatafuta mazingira rafiki yakuishi kwa tochi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nch hii ina mbuga nyingi sana na zenye eneo kubwa sana kuweza kuhamisha kabila ambalo limedumisha mila na tamaduni zake kwenye maeneo yao ya asili na hivyo kuwa kivutio kwa wageni, acheni kuleta maslahi binafsi kwenye hili swala.......
 
Hiyo nembo inamaana gani?

View attachment 2113934
Hii nembo ilitengenezwa miaka hiyo kulipokua na sheria ya matumizi mseto ya ardhi ila haya ni mambo yanayoweza kubadilika muda wowote.kwahiyo hata hii nembo naamini itakuja kubadilika kwasababu sasa hivi wizara ya maliasili iko na mchakato wa mfumo wa jeshi usu la uhifadhi ambalo litabadili mambo mengi yakiutendaji na utambulisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru kwa hilo mkuu,watu hawapendi ukweli.
Umeandika vizuri, lakini ukaweka ukweli nusu. Unatakiwa ukamilishe taarifa yako.
Yapo mambo ambayo hayabishiwi.
La kwanza ni kwamba Ngorongoro ina hali mbaya.
La pili ni kwamba Ngorongoro ni ya kipekee kwa kuhifadhi Wafugaji na Wanyamapori.
Tatu ni kwamba Hifadhi hii ya Wafugaji na Wanyamapori inaingiza pesa za kutosha kila mwaka. Takribani zaidi ya Bilioni 150 kila mwaka.
NNE ni kwamba Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeshindwa kuitunza hiyo Hifadhi, pamoja na makusanyo makubwa sana kila mwaka.
TANO ni kwamba kila anayezungumzia uharibifu wa Ngorongoro anakwepa kumtaja MTUHUMIWA halisi, ambaye ni Ngorongoro Conservation Area Authority, yaani Mamlaka ya Hifadhi hii, badala yake anaelekeza lawama kwa Wafugaji, ambao ni sehemu ya Uhifadhi huu.
Na mwisho tunatakiwa tuungane kuiokoa Ngorongoro kwa kuwaweka Kitimoto Mamlaka ya Hifadhi watueleze wanalofanya katika hiyo Hifadhi wakati mazingira yanaendelea kudorora.
Kuna kila dalili kuwa rushwa inatembea katika hizi harakati.
Viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi wanaweza kuwahonga watu wachache, lakini hawawezi kutuhonga Watanzania wote, tena kwa kutumia pesa zetu za Umma.
Sijaona anayeuliza utaratibu wa kutoa Vibali vya Ujenzi ndani ya Hifadhi na madhara yake kwa Uhifadhi.
Madhara ya Majengo makubwa na Mahoteli yanavuruga 'ecosystem' ya Ngorongoro.
Mamlaka ya Hifadhi ndilo tatizo la Ngorongoro.
 
Iangamie tu, unadhani hao wanaowafurusha wamasai ni kwa maslahi ya Taifa?
 
Ebu tuache porojo maana jamii ya kimasaai haijaanza kuishi huko jana iyo population increase awakuiproject ao watu wa mazingira kwmb baada ya miaka kadhaa wataleta uharibifu kwenye mazingira wafanye namna mapema leo ndo wanaona mazingira yanaharibika, waacheni ao watu waishiiiii acheniiii porojo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…