Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli

Na umethibitisha kwamba huijui Ngorongoro inayoongelewa hapa.

Wewe mjanja unafikiria....

Ngorongoro(Highlands).

Maeneo yanayojumuisha, ukanda wa mlima lemagurut, kakesio na kuzunguka Ngorongoro crater kwenye msitu wa tropical.

Mimi mjinga ninaiongelea......

Ngorongoro (Lowlands).

Bonde la olduvai kwenda mpaka Malambo,Naiyobi, Lake Natron na ukanda wa Oldoinyo Lengai.

Hizo ni kanda mbili tofauti na uelewa wako mdogo

Midimay.

Kiwango cha mvua kinachopatikana Olduvai na Ukanda huo mpaka Malambo ni cha chini zaidi.

Kulinganisha na maeneo ya Makao,Kimba,Ole misgiyo,Ole kepusi,Nainokanoka, Olmoti na Empakai.

Na ndio sababu huwa siku zote mgogoro uko kwenye kuzuia wafugaji kuja kuchungia ng'ombe zao kwenye huo ukanda wa msitu kuizunguka Crater.
Sababu pana uoto mzuri na vyanzo vikuu vya maji.

Vyanzo vya maji ya Ngorongoro ni msingi wa uhai na matumizi ya ukanda mzima wa Ngorongoro,Karatu,Lake eyasi.


Pamoja na kuwa chanzo kikuu cha Underground water forest ya uoto wa hifadhi ya ziwa
#Manyara.

Hatukurupuki kuandika humu bali tunaandika kile tulichokiishi na kukifanyia kazi.

Karibu sana Midimay [emoji22]
 
Well said [emoji736] mkuu!
Huo ndio uhalisia uliopo.
 
A man himself !!

wewe Ni mtu muhimu Sana,. Ngorongoro inakuhitaji Ni wakati wako wa kuitetea sasa
Nakubaliana na wewe!
Tunachopaswa kufanya ni kuitaka serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinusuru eneo hilo na viumbe wake.
Lakini ihakikishe katika uendeshaji wa zoezi hilo,haki itendeke bila kufanya uonevu wala upendeleo kutoka kaya moja kwenda nyingine.

Kusitokee upotevu wa mali za wananchi.

Ili kubalance na kubakiza idadi ya wafugaji wanaoendana na uhifadhi kusudiwa.
 
Conclusion yako inatokana na mijadala ya mitandaoni.

Good.
 
#fundimchundo!
Uko sahihi.

Mambo au matatizo ya Ngorongoro yako mengi sana na niseme ukweli...kwa wale tunaobahatika kuwa karibu na hilo eneo,inatusikitisha sana.

Matatizo au kadhia niliyoamua kuiweka mezani leo ilikuwa hii ya mgogoro wa kimazingira baina ya Ufugaji,Ukazi na Uhifadhi.

Suala la Mismanagement nalo ni la kipekee katika huu mgogoro. Lakini nalo linahitaji tulifungulie topic yake binafsi ili wadau na jamii ipate kujua kinachoendelea.

Lakini pia wananchi na wadau kupitia hiyo topic waweze kuuanika uozo wowote wanaoujua.
Kama upo na unaendelea, ili serikali itusaidie kwa kuwajibika zaidi kwenye eneo hilo.

Kuna wakubwa wengi wataguswa maslahi yao humo,lakini hatupaswi kuliogopa hilo.
Tuendelee kuliokoa taifa kwa kutoogopa kutoa maoni ya kile tunachokiamini, kwa wakati husika na kwa eneo au hoja husika.
Ahsante fundimchundo
 
Midimay, unakosea kutumia lugha isiyofaa wakati unaongea mambo mazuri sana kama uliyoandika.
Watanzania wengi hawajui kwa nini Ngorongoro ina Mamlaka yake, tofauti na Mbuga nyingine za Wanyamapori.
Upekee wa Ngorongoro ni kule kuishi pamoja kwa Wafugaji na Wanyamapori.
Nje ya kuishi pamoja, hakuna hicho kiitwacho Ngorongoro World Heritage.
Wabunge nao wapo wasiolijua hili.
Wafugaji wa Kimasai ndiyo nguzo kuu ya Uhifadhi Ngorongoro.
Tatizo, kama ulivyoligusia, ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, NCAA.
Ni wala rushwa.
Ni wazembe.
Ni watoa rushwa.
Ni wabadhirifu.
Hawafai.
Wanakula rushwa kuruhusu Ujenzi holela mbugani.
Wanazembea kuitunza Hifadhi. Tunaposema kuitunza Hifadhi ni pamoja na kuwahudumia Wafugaji wa Kimasai ambao ni 'integral part of Ngorongoro Conservation Area.
Hifadhi inaingiza zaidi ya Shs. Bilioni 150 kila mwaka kwa sababu ya upekee huu wa Binadamu na Wanyamapori kuishi pamoja.
Mimi siyo mwenyeji wa Ngorongoro, lakini nimelijua hili baada ya kukutana na Mtaalam aliyenielimisha juu ya Ngorongoro.
Na nikajisomea pia taarifa zaidi kwenye Google.
Viongozi wa Hifadhi wanatumia pesa za Umma kuhonga watu mbalimbali ili lawama itoke kwao ielekezwe kwa Wafugaji.
Tukielimishana bila matusi, Watanzania tutaendelea kujua uhalisia wa Ngorongoro.
Tutajua ukweli wa Ngorongoro.
Na daima, 'kweli' itatamalaki.
Kampeni chafu za kuwatuhumu Wafugaji zitashindwa.
Wafugaji na Wanyamapori wataendelea kuishi pamoja na kuneemeka pamoja.
Na wataingiza mabilioni mengi zaidi kuliko Bilioni 170 za mwaka juzi.
 
Asante kwa ushauri kiongozi lakini hatuwezi kuwa na lugha tamu kama waathirika. Kiukweli tunakwaza na tunakasirishwa na hivi vitendo vya NCAA na wizara ya maliasili na utalii kwa ujumla kujitoa akili na kutumia rasilimali fedha za umma kumhonga kila mtu ili wapate uungwaji mkono. Ukiona hivyo ujue kwenye mijadala wameshindwa. Walikuwa wamejipangia hadi Februari hii wawe wamehamisha wamaasai pale kwenda Handeni na Kitwai.
Wameshindwa kwenye meza ya majadiliano, wameopt kutumia waandishi makanjanja kama Kitenge.
Na, je huko wanakotaka kupeleka wamaasai, kuna huduma za jamii, kama wanadai eti kule hakuna huduma za jamii?
Hawa watu ni wajinga sana.
Lazima serikali iwalinde watu wake na sio kuruhusu wachache kuwaumiza watu wake au jamii moja. Ni hatari sana. Ni upaliliaji wa mbegu mbaya.
 
Mkuu kinachogombaniwa ni maeneo ya malisho ya bure.
Hizo flats wala makazi si hoja. Hao nomadic pastoralists watahama tu.
Kama solution ni kuwaondoa kwa kisingizio cha uhifadhi basi ziondolewe hoteli za watalii na ofisi zote za NCAA.
Na mwongozo huo uende hadi maeneo yaliyopo chini ya TANAPA!
Hoteli na ofisi ziwe nje ya hifadhi!
 
... hapo nimeelewa Mkuu; kumbe masai hajawahi kuwa na shida na malazi/nyumba; dhahabu kwake ni green yards kwa ajili ya chakula cha mifugo. Ufafanuzi wako umeeleweka vyema; asante sana.
 
Ni kweli kabisa kuwepo kwa wamasai na wanyama Ngorongoro ilikuwa ni kivutio hapo zamani. Lakini kwa sasa idadi ya Wamasai imezidi mno na baadhi ya tamaduni wamebadili. Njia pekee ya kulinda Ngorongoro ni kuwatoa wamasai! Tanzania ina maeneo mengi mazuri sana kuwaweka.
 
Kwa sasa ipi? Waliongezeka lini? Ni limlni walivuka ile idadi mnayotaka? Nani aliweka hiyo idadi? Walipozidi hiyo idadi kulifanyika nini? Nini ilikuwa plan idadi ua watu ikivuka limit iliyowekwa?
 
Ukiwaondoa Wafugaji, maana yake unaiua Hifadhi ya Ngorongoro.
Mimi napinga kuwahamisha Wafugaji.
Kwa nini, Tanzania kama Nchi, ishindwe kuboresha eneo lenye ukubwa wa kilimita za mraba 8292, lenye uwezo wa kuingiza bilioni 200 kwa kila mwaka?
Kwa nini tunailea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati imethibisha kushindwa kazi?
 
Hakuna kitu tunachoweza kufanya kama nchi. Tuna mapungufu makubwa sana. Kama vile tumelogwa. Inakuwaje mtu anaamini kuwaondo watu ndio kuiokoa na kuitengeneza Ngongoro? Mbona ni upumbavu?
 
Hakuna kitu tunachoweza kufanya kama nchi. Tuna mapungufu makubwa sana. Kama vile tumelogwa. Inakuwaje mtu anaamini kuwaondo watu ndio kuiokoa na kuitengeneza Ngongoro? Mbona ni upumbavu?
Kuna taarifa za uhakika kuwa Faru waliokuwepo Ngorongoro waliwindwa na kumalizika baada ya Viongozi wa Hifadhi, NCAA kuwaondoa kwenye ulinzi wa mbuga, u-Game Warden, Wafugaji wa Kimasai. Na ilithibitika kuwa Mhifadhi Mkuu ndiye aliyehusika kumuua huyo Faru.
Propaganda za Viongozi Wabadhirifu, zinataka kuizidi nguvu hoja ya Uhifadhi.
NGO lukuki zilizojaa Ngorongoro nazo zinastahili kubeba lawama kwa kuhodhi Hoja ya UPEKEE wa Binadamu kuishi pamoja na Wanyamapori.
NGO zilikosea mara kwa mara kwa kutamka kuwa Ngorongoro ni ya Wamasai, hali inayoleta UKAKASI wa Kikabila.
Matokeo yake, wapo wanaotaka Wafugaji waondolewe kwa sababu tu ya kukerwa na 'tune' ya Ukabila inayotajwa tajwa. NGO zimefanya makusudi kutumia neno Wamasai ili wapate fedha za Wafadhili.
Tufike mahali tuelezane ukweli.
Yote katika yote, tatizo ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Na baada ya kumsikiliza Waziri Mkuu Bungeni, upo uwezekano wa Ufisadi wa Mamlaka kukumbatiwa na Serikali.
Wapigania haki za Uhifadhi wa Ngorongoro, unganeni uje Uzi madhubuti hapa JF kuiokoa Ngorongoro.
Hapa issue siyo kuwaokoa Wanyamapori peke yao wala Wafugaji pekeyao.
Ngorongoro ni mahali pa haya makundi mawili kuishi pamoja.
Ngorongoro ni UNIQUE.
Paendelee kuwa 'unique'.
 
Ngorongoro ni mahali pa Binadamu na Wanyamapori kuishi pamoja.
Watalii wanaofurika kuingia Ngorongoro wanakuja kuona na kushangaa hali hiyo ya kuishi pamoja.
Ukiwaondoa Wafugaji, Ngorongoro inaondolewa kwenye Orodha ya UNESCO World Heritage Sites, maana itakuwa Mbuga tu sawa na Serengeti.
Nashanga kuwa wapo wasioliona hilo.
Jiulize, wakati Ngorongoro inaingiza Bilioni 170 mwaka juzi, hizo Mbuga za Taifa ziliingiza kiasi gani?
Kwa nini?
Kwa nini ishindikane kuboresha eneo linaloingiza hela nyingi, kiasi cha kufikiria kuliua?
Eneo ambalo ukubwa wake ni kama Kilomita 90 kwa kilomita 90.
Tukikubali Ngorongoro ife kwa kuwaondoa Wafugaji, itafuatia Serengeti National Park, ambako hivi sasa Makampuni mengi ya Nchi za Nje wameomba wapewe Leseni za Kuchimba Madini.
Tangu wakati wa Mkoloni mpaka mwaka jana, haikuruhusiwa kuingia kwenye Mbuga ya Serengeti kutafuta madini.
Ngorongoro ikifa, itafuatia Serengeti.
Wafugaji wasiondolewe Ngorongoro.
Badala yake tutumie mapato makubwa yanayopatikana kuboresha mazingira ya Wafugaji na Wanyamapori.
Waendelee kuishi pamoja.
 
... hapo nimeelewa Mkuu; kumbe masai hajawahi kuwa na shida na malazi/nyumba; dhahabu kwake ni green yards kwa ajili ya chakula cha mifugo. Ufafanuzi wako umeeleweka vyema; asante sana.
Hakika! Ki asili ni nomadic pastoralists. Ng'ombe kwao ni kila kitu. Majuzi tu hapa October to December maeneo mengi yalikumbwa na ukame. NCA ikawa kimbilio. Ng'ombe makundi kwa makundi walihamishiwa kutafutiwa malisho.

NB: Wenyeji wanaona kama wageni wananufaika zaidi yao.
 
Safi sana kama wameanza kuhamishwa . Mambo mengine sio ya kukaa kujadili, yanahitaji udikteta.
 
Kweli mkuu unaifaham vizur ngorongoro, naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…