Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli

Parody la mshambuliaji hili. Period
 
Umeua mkuu....akirudi nitag
 
Ile semina aliyoagiza waziri mkuu kwa ajili ya wabunge,inawafaa wengine pia kama hawa
Mkuu
Unahitaji kueleweshwa kidogo kuhusiana na hili.

Hapa haiongelewi Ngorongoro ya Loliondo,huko ndio kuna mwarabu.

Bali inaongelewa tarafa ya Ngorongoro ambalo ni eneo linaloihusu Crater ya Ngorongoro na vijiji kadhaa vya kuizunguka hiyo crater.
 
Hata kule selou wapo waliopongeza na wapo wengi waliopinga huo mradi.
 
Kweli Ngorongoro inaangamia kwa kuendekeza siasa za kijinga, Tanzania tuna maeneo mengi ya mapori wanaweza kupelekwa huko kuishi lakini hatuna ngorongoro nyingine.
 
Nimesoma para chache sana nimekuelewa 'naunga mkono hoja' ngorongoro inatoweka real.
Hata mimi pia nimesoma mistari michache tu nimemuelewa. Kusema kweli suala la Ngorongoro wala halihitaji uwe na madigirii kuona kwamba hifadhi inaharibika.
 
Mkuu asante kwa uchambuzi mzuri.
 
Hivi ukimpa mtu offer ya kumhamishia mahali ambapo maisha yake yatakuwa qualitatively better kuliko yalivyo pale alipo sasa atakaa kweli?

Sidhani kama Serikali imenadi mpango wowote wa maana kwa hii jamii ya Wamaasai.
Huu muda ambao wamasai wanaupoteza kwa kubishana na serikali nadhani wangetumia kujadili hayo maana mwisho wa siku watakaoathirika ni wao.
 
Mimi nimekaa siku tatu pale , naafiki masai waondolewe kwa kuwa wanazaana sana uwezi kudhibiti hali hiyo. Ila Tanzania nayo ipunguze idadi ya vipori uchwala watu wapate maeneo ya kuishi na kufuga. Mfano mkoa wa shinyanga na tabora kuna vipori vingi vya hovyo.
 
Mimi nimekaa siku tatu pale , naafiki masai waondolewe kwa kuwa wanazaana sana uwezi kudhibiti hali hiyo. Ila Tanzania nayo ipunguze idadi ya vipori uchwala watu wapate maeneo ya kuishi na kufuga. Mfano mkoa wa shinyanga na tabora kuna vipori vingi vya hovyo.
 
Uko sahihi kabisa. Kwa mfano hawa wafugaji wa kimasaai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Wangepewa mojawapo ya hayo mapori ya akiba na waendelee kuishi na wanyama kama kawaida yao.
Ili kuiokoa ikolojia ya Ngorongoro.
 
Kusema wabaki baadhi itakuwa ngumu,maana baada ya miaka kadhaa watu na mifugo vitaongezeka Tena ....

Wewe unaijua vizuri ngorongoro je kwa nn serikali isiongeze radius kuzunguka mbuga? Hata kilometer kadhaa?
 
Kumbuka Masai hawaka Ghorofani. Ukitaka kuwauwa basi walazimishe kukaa ghorofani mori ukiwapanda mtawakuta wote chini.
 
Hivi vinavyoangamia Tanzania ni Ngorongoro tu? Deni la Taifa mbona pia linatuangamiza.
 
Voicer, kwanza nikiri hapa kuwa wewe ni 'voice of reason' hapa JF katika mjadala huu. Na wewe ni ama Mkazi wa Ngorongoro au unao ukaribu mkubwa na Ngorongoro.

Nimefuatilia yaliyozungumzwa Bungeni nikafahanu kuwa idadi kubwa ya Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliopo Ngorongoro wanamilikiwa na watu walio nje ya Ngorongoro.

Mifugo mingi ni mali ya Watu wenye Landcruiser VX wanaolala katika Nyumba za Maghorofa nje ya Hifadhi.
Wafugaji ndani ya Hifadhi wanamiliki Ng'ombe, Mbuzi, na Kondoo wachache sana.

Wingi wa Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliotoka nje ya Hifadhi ndicho kiini cha mgogoro huu.
Mamlaka ya Ngorongoro ni Watuhumiwa namba moja katika tuhuma hii.

Wameshiriki kuingiza mifugo toka nje ya Hifadhi kwa ama kulifumbia macho jambo hili, au kushiriki moja kwa moja.
Watuhumiwa namba 2 ni NGO zilizojaa Hifadhini ambazo zinaogopa kuwataja Wamiliki wa mifugo wakati wanawajua. Inawezekana Wamiliki wa hizo NGO na wao wameshiriki kuingiza mifugo yao ndani ya Hifadhi.

Watuhumiwa namba 3 ni Wafugaji wenyewe wa Kimasai waliokubali kutumiwa kuchunga mifugo ambayo siyo mali yao.
Inawezekana walipaza sauti zao lakini zikamezwa na Viongozi wa NGO na Mamlaka ya Ngorongoro ambao wanashirikiana kuiua Ngorongoro kwa kinachoonekana kuwa masilahi binafsi.
Tupe mwanga kuhusu hili tafadhali.
 
Kusema wabaki baadhi itakuwa ngumu,maana baada ya miaka kadhaa watu na mifugo vitaongezeka Tena ....

Wewe unaijua vizuri ngorongoro je kwa nn serikali isiongeze radius kuzunguka mbuga? Hata kilometer kadhaa?
Mkuu!



[emoji871]Tatizo kubwa hapa ni kwamba hata kama radius itaongezwa bado source kuu ya maji na malisho iko huku juu Ngorongoro Highlands.

[emoji871]Na hiki ndio kiini cha mgogoro,maana kila inapofika majira ya kiangazi,ukame unawalazimisha wafugaji kuileta na kuiingiza mifugo yao ndani msitu kwa malisho.kinyume na sheria.

[emoji871]Kwa hiyo eneo la square km 8200.
Sio dogo kwao.

[emoji871]Ila eneo lenye neema ni kama 30% ya eneo lote latarafa hiyo ya Ngorongoro.Na kila kundi lina uhitaji wa eneo hili.

Na ugomvi unaanzia hapo.
 
fundimchundo!

[emoji871]Umeongea mambo mengi kuihusu Ngorongoro kwa ujumla wake.
Ila nitofautishe hapa.....

[emoji871]Kuna migogoro miwili ya ardhi katika wilaya ya Ngorongoro.Nayo ni kama ifuatavyo.

[emoji871]Kuna mgogoro wa ardhi unaoihusu tarafa ya Ngorongoro yenye ukubwa wa Square kilometres 8200.

[emoji871]Ambapo wafugaji wanatakiwa kuhamishwa ili kupunguza idadi ya shughuli za kibinadamu na ongezeko kubwa la idadi ya mifugo.
Hali
inayotishia uwepo wa uhifadhi mseto baina ya Binadamu na mifugo yao,pamoja na wanyama pori asilia na ikolojia ya mimea.

[emoji871]Kuna mgogoro wa ardhi unaoihusu tarafa ya Loliondo yenye ukubwa wa square kilometres 1500.
Ambapo shughuli za makazi ya binadamu na mifugo yao inatakiwa kukoma.

[emoji871]Ili kuweza kubadili matumizi ya eneo hilo kuwa pori tengefu au Game reserved area.

[emoji871]Hapa tunajadili eneo moja kati ya hayo mawili.
Ambalo ni tarafa ya Ngorongoero.

[emoji871]Kuhusu umiliki wa mifugo kwa watu wasioishi ndani ya hifadhi au eneo la Ngorongoro,ni jambo lenye utata.

[emoji871]Sababu ni ukweli usiopingika kwamba,maisha ya kaya nyingi unazozikuta na idadi kubwa ya mifugo.
Bado haireflect maisha unayowakuta nayo kwenye maboma hayo.

[emoji871]Mimi binafsi sijalifanyia kazi suala hilo kwa sababu liko mbali tofauti na majukumu yangu ya kikazi yanayoniwezesha kufikia maeneo hayo.

[emoji871]Nimewahi kuona mfumo huu katika nchi ya Rwanda[emoji1206].

Kwamba!

[emoji871]Kuna eneo linaitwa #Kayonza.eneo hilo maarufu nchini #Rwanda[emoji1206].sababu ndiko mji wa nyumbani alikozaliwa rais #Kagame wa nchi hiyo.Kayonza pia inapakana na hifadhi maarufu ya wanyama nchini humo ya #Akagera National Park.

[emoji871]Lakini hapa nimelitaja kwa sababu niliona tukio linalofanana na hili la Ngorongoro.

[emoji871]Kuna idadi kubwa sana tena kupindukia ya mifugo inayotunzwa hapo ili kufaidi malisho katika bonde la Akagera. (Kagera).

[emoji871]Na ukiulizia wamiliki wa Ng'ombe wale utapewa jibu kwamba baadhi ni wa familia za mawaziri pamoja na matajiri walioko #Kigali.

[emoji871]Hivyo sintanshangaa mtindo huo kuwezekana ndani ya Ngorongoro.
 
Utalii wa utamaduni kwa namna unavofanyika sasa NCA ni greenwashing ya nguvu.
Watu wanaigiza maisha ya Maasai pale "Kanjiro" (staged cultural experience).
Kingine utitiri wa lodge na camps unaathiri biashara ya utalii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…