Uamuzi wa serikali wa kuhamisha jamii ya Wamasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomera ni hatua yenye msingi wa kisheria na kisiasa, inayolenga kulinda maslahi ya taifa pamoja na kuhifadhi mazingira. Hatua hii, ingawa imeibua hisia mchanganyiko, inafuata mwelekeo wa matukio mengine yaliyowahi kutokea nchini Tanzania na kwingineko duniani, ambako serikali zimechukua hatua za kulinda maliasili na kuhakikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Katika historia ya Tanzania, serikali imewahi kuchukua hatua kama hii katika maeneo mengine kwa lengo la kuhifadhi mazingira au kuwezesha maendeleo. Mfano wa kwanza ni kuundwa kwa Hifadhi ya Selous miaka ya (1950-1970), ambapo jamii za Wadengereko na Wamatumbi zilihamishwa ili kupisha eneo hilo kuwa hifadhi ya wanyamapori.
Hifadhi hii ni mojawapo ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyoko chini ya uangalizi wa UNESCO. Pia, mwaka 1988, jamii ya Waparakuyo wa Kimasai walihamishwa ili kupisha kuundwa kwa Hifadhi ya Mkomazi. Hifadhi hii inajulikana kwa juhudi zake za kulinda wanyamapori, hasa faru weusi. Aidha, uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire mwaka 1970 ulipelekea kuhamishwa kwa jamii nyingine ya Wamasai kutoka eneo hilo ili kuwezesha utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa wanyamapori. Sambamba na hayo, sera ya Ujamaa na Kujitegemea iliyotekelezwa kati ya mwaka 1967 na 1973 ilisababisha kuhamishwa kwa mamilioni ya watu kutoka maeneo yao ya asili kwenda kwenye vijiji vya Ujamaa. Lengo lilikuwa ni kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii kama vile elimu, afya na maji, pamoja na kuongeza uzalishaji wa kilimo. Matukio haya yameonyesha kuwa, wakati mwingine, serikali inalazimika kuchukua hatua za kipekee kwa maslahi ya taifa na maendeleo endelevu. Kuhamishwa kwa jamii ya Wamasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomera ni mwendelezo wa juhudi hizi za kuhakikisha kuwa maeneo ya urithi wa dunia yanahifadhiwa ipasavyo, wakati huo huo kuwapa wananchi nafasi ya kuishi kwenye maeneo yanayofaa kwa makazi na maendeleo.
Uamuzi wa kuhamisha jamii kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira au maendeleo si jambo geni duniani. Nchini Canada kwa mfano, jamii ya Sayisi Dene ilihamishwa katika miaka ya 1950 kwa madai ya kulinda wanyamapori. Huko Brazil, ujenzi wa Bwawa la Belo Monte katika miaka ya 2010 ulipelekea kuhamishwa kwa maelfu ya watu wa jamii za asili ili kupisha mradi huo mkubwa wa nishati. Nchini Lesotho, mradi wa Maji wa Lesotho Highlands ulioanza mwaka 1986 ulisababisha kuhamishwa kwa jamii kadhaa ili kupisha ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na usambazaji wa maji kwa nchi jirani. Vilevile, nchini India, mradi wa Bwawa la Narmada uliosababisha kuhamishwa kwa maelfu ya watu ili kupisha ujenzi wa bwawa kubwa kwa ajili ya umwagiliaji na uzalishaji wa umeme. Uamuzi kama huo umetokea China n kwingineko.
Kisheria, uamuzi wa serikali kuhamisha Wamasai unazingatia sheria za kitaifa zinazohusu uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya kijamii. Sheria ya Ardhi ya Tanzania na Sheria ya Uhifadhi wa Mazingira zinatoa mamlaka kwa serikali kuchukua hatua za kulinda maeneo ya urithi wa dunia na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali. Zaidi ya hayo, Katiba ya Tanzania inatoa haki kwa serikali kuchukua ardhi kwa maslahi ya umma, kwa sharti la kutoa fidia stahiki. Kisiasa, uamuzi huu unalenga kulinda maslahi ya taifa kwa ujumla, kwa kuhakikisha kuwa maeneo yenye thamani kubwa ya kiasili kama Ngorongoro yanahifadhiwa ipasavyo. Pia, unatoa fursa kwa jamii za Wamasai kupata maeneo mbadala yenye huduma bora zaidi za kijamii, kama vile afya, elimu, na maji, ambazo zimekuwa changamoto kubwa katika eneo la Ngorongoro. Wamasai wanamilikishwa ardhi kubwa wanazopewa ili kuwapatia uhakika wa makazi ya kudumu, malisho ya mifugo yao na usalama wa chakula. Mila na tamaduni zao zinalindwa na wataziendeleza.
Kwa ujumla, uamuzi wa kuhamisha Wamasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomera ni hatua yenye msingi imara wa kisheria na kisiasa. Ingawa kuna changamoto zinazohusiana na utekelezaji wa hatua hii, Lakini zinafanyiwa kazi ili zoezi liweze kuwa na manufaa makubwa.
Sorry, the Ngorongoro case is distinguished in that it entails the elevation of foreign companies sovereingty above constitutionally guaranteed People' Sovereignty over their natural resources, and hence the commission of a crime against the state through the instrumentality of the incumbent government.
In the present case, where, the government is forcibly relocating the Masai Community, to create space for the company called OBS, which is owned by an Arab Dynasty, the government is in effect, creating an Arab satellite state.
The owner of the OBC company is Major General Mohammed Abdulrahim al Ali, the deputy defense Minister of the UAE.
The company has been in Ngorongoro since 1995, trying to covertly lobby for the creation of an Arab satellite state in Tanzania.
This secretive project has been easily concluded, through a government order, and under President Samia, and who is genetically linked to the Arab world.
So, this is a pure case of state sovereignty mutilation under foreign influence from the Middle East Arabic World.
I shall have more to say on this after a careful analysis of the available evidence.
For now, let me clarify the terms. Satellite States, also known as client states or vassal states, are separate nation states which espouse the same method of governance as the master state controlling them. The master state is under full or partial control of other states which are “revolving” around it, where the control is hidden or behind the scenes.
In this sense, "Ngorongoro" has been an Arab satellite state in the making for some years now, since the time when Mizengo Pinda wa still our Prime Minister. And now, the government's order to evict the indigenous Masai residents, and deregister the villages, while abandoning the resistant residents leaving them without any key social services has concluded the Arab satellite state creation project.
In short What the government is doing to the Masai community is akin to what the government of Nigeria did to the Biafra community where thousands died because of government imposed hunger.
It is the only evidence needed to prove that the sixth phase government under President Samia has lost legitimacy.