Ngorongoro wakiifunga Morocco leo, wanatinga robo fainali

Ngorongoro wakiifunga Morocco leo, wanatinga robo fainali

Dakika 12'
Pasi ndefu ya kichwa inapokewa kwa kichwa na kuunganishwa vyema kwa mguu, Morocco wanapata goli jingine
Tanzanie 0 - 3 Maroc

[emoji1][emoji1][emoji1] wanamzuka wa kwenda ulaya, talent zipo za kutosha..

Unacho kisema ni kweli kwa sababu wangekua wanampa pasi Kelvin John ambaye anaonekana kuzurura tuu pale mbele bila mpira saizi wangekua wamesha qualify kitambo.

Team work na preority ndio shida ya hawa watoto.
Mwalimu hajawapa muunganiko mzuri uwanjani
 
Dakika 17'
Counter attack ya Morocco inasababisha faulo nje kidogo ya penati box ya Ngorogoro Heroes . Adhabu kuelekea Tanzania. Kipa Daniel Mgore wa Tanzania anaunyaka mpira huo wa adhabu bila wasiwasi.
 
Tatizo ni mfumo wa soka Tanzania, hawa wangekuwa tayari wanachezea klabu za ligi kuu ya Tanzania, mapungufu haya hayangekuwepo. Tunawachelewesha sana kuwaita "madogo" wakati walitakiwa wameshacheza mechi ktk ligi kuu yetu zaidi ya michezo 60 .

Tufumue mawazo mgando na kuwaamini wawechezee Namungo, Azam, Simba, Kagera, Coastal Union, Ruvu katika mechi za ligi kuu hata wakiwa na miaka 16, 17 na wakifika miaka 19 na 20 wanakuwa wachezaji hatari tajwa siyo ndani ya Tanzania tu bali hata Afrika na Ulaya.
Mbona karibu wote wanacheza ligi kuu ?
 
22 February 2021
Stade Olympique

Dakika 4'
Adhabu ya peneti kuelekea goli la Tanzania. GOAL !
Tanzanie 0 - Maroc 1 (pen)

c.c tabutupu

Haya madudu yote ya timu zetu za Taifq kuwa kichwa cha mwendawazimu, yanasababishwa na CCM! Wameiba viwanja vyetu mpira wa miguu, hawana sera nzuri ya kukuza vipaji vya watoto zaidi tu ya kuwalazimisha kusoma elimu ya kukaririshwa mpaka kidato cha nne!

Hawataki kutoka madarakani! Ona sasa tunavyo fungwa hovyo hovyo! Hivi hao vijana hawatoki kwenye klabu za simba na yanga kweli? Maana yule atakasirika kweli.
 
Umesema kweli kabisa.. vilabu vianze kusajili u20, na wapewe nafasi..

Pia vilabu havijui tuu kuwa u17 ni biashara nzuri sana kwa sababu akinunuliwa kuna mgao wa timu iliyo mlea kabla ya miaka 18, mgao huo huodelea miaka yote ya mchezaji.

Imagine kama simba ingekua imemsajili samatta toka akiwa 18, kwa sheria za fifa wangepiga mpunga hadi leo.
Hao watoto karibu wote wanacheza ligi kuu hapa Tanzania.

Wengine wanacheza ligi daraja la kwanza.

Sijajua mnataka wacheze simba na Yanga ndiyo waonekane wanacheza ligi kuu.
1 Daniel Mgore ni golikipa namba moja wa Biashara United ya Mara.
2.David kameta amecheza Ligi kuu Lipuli na Simba.
3. Abdul Selemani Sopu anacheza Ndanda Fc ligi daraja la kwanza.
4. Rajab Athuman anacheza Gwambina Fc ligi kuu.

Yule beki namba tatu Paschal anacheza KMC sema hapati namba kwa sababu ya uwepo wa Ramadhani Ally Oviedo.
5.Tepsy Evan's anacheza Ihefu Fc ligi kuu.

Hao ni baadhi tu ya wanacheza timu za ligi kuu.
 
Dakika 31'

Khatari kubwa golini mwa Tanzania lakini kipa anafanya makubwa na kuokoa jahazi la Ngorongoro lisizidi kujaa maji likapata ajali

Tanzania 0 - 3 Morocco
 
Dakika ya 34'
Morocco tena wanaingia kwa kasi ndani ya box lakini shuti linapaa na mpira ni goal kick kuelekea Morocco.

Tanzania 0 - 3 Morocco
 
Dakika ya 39'
Bado Ngorongoro wanapata shida sana kuingia eneo la 18 upande wa Morocco. Tanzania sinia Morocco 3.
Tanzania 0 - 3 Morocco
 
Dakika 41'
Kuelekea kipindi cha kwanza kuisha Ngorongoro heroes wanaonesha kuanza kutulia kidogo ball possession na gonga one-two pasi baina ya wachezaji wa Tanzania kibao na kuonesha matumaini kuelekea kipindi cha pili chs mchezo mambo yatakuwa tofauti.
Tanzania 0 - 3 Morocco
 
Dakika 45 '

Tanzania 0 - 3 Maroc

Timu zinaenda mapumziko,
 
Hao watoto karibu wote wanacheza ligi kuu hapa Tanzania.

Wengine wanacheza ligi daraja la kwanza.

Sijajua mnataka wacheze simba na Yanga ndiyo waonekane wanacheza ligi kuu.
1 Daniel Mgore ni golikipa namba moja wa Biashara United ya Mara.
2.David kameta amecheza Ligi kuu Lipuli na Simba.
3. Abdul Selemani Sopu anacheza Ndanda Fc ligi daraja la kwanza.
4. Rajab Athuman anacheza Gwambina Fc ligi kuu.

Yule beki namba tatu Paschal anacheza KMC sema hapati namba kwa sababu ya uwepo wa Ramadhani Ally Oviedo.
5.Tepsy Evan's anacheza Ihefu Fc ligi kuu.

Hao ni baadhi tu ya wanacheza timu za ligi kuu.
Safi sana data zako ziko vizuri, tatizo ni nini wachezaji nyota Azam, Namungo, Yanga, Simba n.k wanatoka Ghana, Congo, Burundi, Zimbabwe, Uganda ?

Hawa madogo na mafaza wa kiTanzania kwanini wanafunikwa ktk timu zao za kiTanzania?

Bado tupo Mauritania U20 CAF timu za Tanzania na Morocco zipo mapumziko

Highlights kipindi cha kwanza

Safi sana data zako ziko vizuri, tatizo ni nini wachezaji nyota Azam, Namungo, Yanga, Simba n.k wanatoka Ghana, Congo, Burundi, Zimbabwe, Uganda ?
Hizo timu zinahitaji wachezaji wanaoshindana kwa sababu wachezaji wetu wengi hawana ndoto binafsi za kufika popote ndiyo maana hawajitumi uwanjani.

Lakini tuseme ukweli timu ya Ngorongoro heroes haina kocha.

Jinsi inavyocheza unaona wazi timu haijaunganishwa vizuri kiuchezaji siyo ubora wa wachezaji.
 
Back
Top Bottom