Connection ndio kila kitu mkuu, nakumbuka kipindi Mkwere ndio anamalizia awamu ya pili kuna shirika moja wapo juu nilipiga nao Interview hadi kwenye Oral ikaishia hapo.
Baada kama ya kama mwaka hivi nikapata Connection ya shirika lingine toka juu hapo hapo, hiyo sikufanya hata interview nikaambiwa tu nika report ofisini kwao hapa Dar, nilivoenda kuna maelezo nikapewa then kuna vitu nikakabidhiwa then nikaambiwa Jumapili safari nikareport kwenye kituo changu cha kazi.
Mradi wa kwanza ukaja kuisha nikarudi town, ukaja mradi wa pili nao nikapigiwa simu tu na jamaa alonipa hiyo connection, safari hii nikapelekwa mkoa mwingine kabisa huo mradi ukaisha ndio nikarudi town.
Nakubaliana na wewe kazi nyingi za NGO ni mwendo wa connection tu mkuu.