NGO'S na upatikanaji wake wakazi

NGO'S na upatikanaji wake wakazi

Nimefanya kazi shirika.

Nasubiri mradi pia katika shirika.

Muda wote niljokuwa katika shirika nimejifunza connection ni kitu kikubwa sana.

Pia shirika halipendi kufanya kazi na mtu asiyemzoefu na kazi.

Mara nyingi hata wakitangaza ajira wanakuwa na watu wao.

Kwenye shirika langu hata leo ikitangazwa ajira mimi nampgia Dr naitwa kazini na wala sio kwa interview
Hold on Mkuu, hivi nimekuona kwenye uzi fulani ume jiajiri unaingiza 1m au nimekufananisha?
 
NGOs zote ambazo DONOR ni mmoja, lets say USAID Mara nyingi nafasi za kazi huwa wanatangaziana NDANI ya taasisi Kwanza.

Wakikosa mtu ndio wanatangaziana NJE.

PILI, NGOs siku hizi HAZILIPI vizuri, UHUNI mwingi labda uwe nafasi za JUU.
Shida ni unaingia vipi hapo kwao ili wakupe nafasi hata ukitolee
 
Shida ni unaingia vipi hapo kwao ili wakupe nafasi hata ukitolee
Kuna ukweli fulani...mara nyingi "kamlete approach" na head hunting ndio hutumika. Pia wengi wao huwa wana God fathers above...kuna mfano wa shirika fulani limejaa mashemeji..ndugu wa viongozi wa juu plus dotted lines. Ila nafasi chache ndio hua zinaachwa mpiganie waombaji wa nje
 
Connection ndio kila kitu mkuu, nakumbuka kipindi Mkwere ndio anamalizia awamu ya pili kuna shirika moja wapo juu nilipiga nao Interview hadi kwenye Oral ikaishia hapo.

Baada ya kama mwaka hivi nikapata Connection ya shirika lingine toka juu hapo hapo, hiyo sikufanya hata interview nikaambiwa tu nika report ofisini kwao hapa Dar, nilivoenda kuna maelezo nikapewa then kuna vitu nikakabidhiwa then nikaambiwa Jumapili safari nikareport kwenye kituo changu cha kazi.

Mradi wa kwanza ukaja kuisha nikarudi town, ukaja mradi wa pili nao nikapigiwa simu tu na jamaa alonipa hiyo connection, safari hii nikapelekwa mkoa mwingine kabisa huo mradi ukaisha ndio nikarudi town.

Nakubaliana na wewe kazi nyingi za NGO ni mwendo wa connection tu mkuu.
Basi tupe connection mkuu okoa kizazi Mungu atakubariki
 
Basi tupe connection mkuu okoa kizazi Mungu atakubariki
Mkuu naona watu wengi wananifuata PM niwape connection. Ila naomba muelewe kuwa ipo hivi yule jamaa alienipaga connection mimi yupo nje ya nchi kama miaka mitatu sasa.

Mimi baada ya kuitwa kipindi kile nilitumikia mkataba wangu mikoa kadhaa, mkataba ulivyoisha sikuongeza nikaanza mishe zangu binafsi, so watu ninaofahamiana nao ni wa level ya chini huku mkoani huko so hawana impact yoyote maana recruitment inafanyikia HQ na sio mikoani.

Nadhani nimeeleweka.
 
Back
Top Bottom