Ni mafuta gani ya mgando unayotumia?
Kama Ni baby care , rays na yanayofanana na hayo hayatakusaidia,
Ukiwa sehemu au kwenye nyakati za baridi na hewa kavu kama nyanda za huko ni vizuri kutumia vipako vizito ambavyo vitakuletea joto pamoja na kutunza unyevu nyevu wa ngozi yako usipotee na kusababisha kukakamaa na kubabuka kwa ngozi.
Tumia vaseline na glycerin tena upake ukishatoka kuoga/kunawa kabla mwili haujakauka ili yashikane vizuri na ngozi, vitakusaidia kukinga kwa kiasi kikubwa dhidi ya uharibifu wa ngozi yako.