Ngozi kufubaa na kuwa kavu. Ni mafuta gani mazuri ya kupaka sehemu za baridi?

Salutations kwenu!

Nipo Iringa wakuu baridi ni kali sana. Tangu nifike nimeona ngozi yangu ikiharibika sana sana.

Hapo kabla ya kuja Iringa, nilikuwa naishi Pwani. Nilikuwa sipaki mafuta na ngozi ilikuwa nzuri tu. Sasa baada ya kuja Iringa na kutokana na baridi nimekuwa napaka mafuta ya mgando ili kufanya ngozi isiwe kavu lakini bado haisaidii.

Naweza kupaka mafuta lakini baada ya nusu saa yale mafuta yanakauka na ngozi kuwa kavu kama mwanzo.

Je, ni mafuta au kitu gani kizuri cha kupaka au kutumia ili kuifanya ngozi iwe nzuri?

Rangi;- Maji ya kunde.
Jinsia;- ME

Piga mkorogo mkuu fanya kum DM mukoko Tonombe
 
Kuna mikoa ukikaa unachakaa kama tako la nyani sema kwa sisi watafutaji tunajikuta tunatulia sehemu yeyote kwa mazingira yeyote ila Dodoma na Singida kuna baridi na vumbi la kutosha yaani utatoka ukurutu kama wote
 
Bora vyote viwepo mkuu, lakini isiwe tu vumbi/udongo mwekundu. Nahisi nina phobia nayo!
 
Ili upate mafuta mazuri inabid kwanza ujue ngozi yako je niya mafuta au kavu? Sasa kwakua wewe ni mwanaume najua hili zoez ni gumu kwako cha kufanya tengeneza mwenyewe nyumban mafuta ya karoti halaf yachanganye na grisil ngozi yako utaipenda sana na bila shaka yatakua ndiyo mafuta yako! (Jinsi ya kutengeneza mafuta ya karoti ingia youtube siyo kazi ngumu kabisa ni kitendo cha dakika kumi tu utakua ushapata mafuta yatakayokupa furaha!
 
Shukuran mkuu! I think ngozi yangu ni ya mafuta coz huwa nikipaka mafuta usoni huwa natokwa na chunusi, ila nikiacha kupaka chunusi hupotea.

Vipi kuhusu Grisil? Umemaanisha Grisi ama..? Sijakupata hapo!
 
Yes ni grisi hii ya kulainisha vyuma [emoji28][emoji28][emoji28]sijui kama alikuwa anamaanisha grasiline
 
Salutations kwenu!

Nipo Iringa wakuu baridi ni kali sana. Tangu nifike nimeona ngozi yangu ikiharibika sana sana.

Hapo kabla ya kuja Iringa, nilikuwa naishi Pwani. Nilikuwa sipaki mafuta na ngozi ilikuwa nzuri tu. Sasa baada ya kuja Iringa na kutokana na baridi nimekuwa napaka mafuta ya mgando ili kufanya ngozi isiwe kavu lakini bado haisaidii.

Naweza kupaka mafuta lakini baada ya nusu saa yale mafuta yanakauka na ngozi kuwa kavu kama mwanzo.

Je, ni mafuta au kitu gani kizuri cha kupaka au kutumia ili kuifanya ngozi iwe nzuri?

Rangi;- Maji ya kunde.
Jinsia;- ME
Ngozi yako ni aina gani??
 
Jitahidi ununue Vitamin E all over body cream naamini haitakuangusha, itaipa ngozi yako moisture kwa masaa 24
Nimekuwa nikiitumia kila nnapokuwa kwenye baridi kali, na matokeo yake ni mazuri sana
Asante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom