Gemini Are Forever
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 1,508
- 2,619
- Thread starter
-
- #21
Asante kwa ushauri mkuu.Ni mafuta gani ya mgando unayotumia?
Kama Ni baby care , rays na yanayofanana na hayo hayatakusaidia,
Ukiwa sehemu au kwenye nyakati za baridi na hewa kavu kama nyanda za huko ni vizuri kutumia vipako vizito ambavyo vitakuletea joto pamoja na kutunza unyevu nyevu wa ngozi yako usipotee na kusababisha kukakamaa na kubabuka kwa ngozi.
Tumia vaseline na glycerin tena upake ukishatoka kuoga/kunawa kabla mwili haujakauka ili yashikane vizuri na ngozi, vitakusaidia kukinga kwa kiasi kikubwa dhidi ya uharibifu wa ngozi yako.
Kiasi hiki cha maji hakina kazi mwilini huku kwetuKuna zile app za kukumbusha wakati wa kunywa maji, itakuwa ya muhimu kwako. Kweli wakati wa baridi, kiu hukatika ila maji hatufai kuacha kunywa, maximun of 8 glasses a day to avoid dehydration.
Inakuwaje shinyanga kuna joto kali lakini ngozi inapauka sana?Baridi ya Iringa, Njombe na Mbeya inababua ngozi kwa sababu ya ukavu wake, humidity iko chini sana huwezi linganisha na mikoa mingine yenye baridi ambayo humidity yake iko juu.
Tafuta mafuta yenye cocoa butter paka au shea butter. Vinginevyo ni mwendo wa kupauka na ngozi kupoteza mvuto(kufubaa).
Asante mkuu, tupo pamoja!Baridi ya Iringa, Njombe na Mbeya inababua ngozi kwa sababu ya ukavu wake, humidity iko chini sana huwezi linganisha na mikoa mingine yenye baridi ambayo humidity yake iko juu.
Tafuta mafuta yenye cocoa butter paka au shea butter. Vinginevyo ni mwendo wa kupauka na ngozi kupoteza mvuto(kufubaa).
Thanks mkuu!Cocoa butter mazito
Salutations kwenu!
Nipo Iringa wakuu baridi ni kali sana. Tangu nifike nimeona ngozi yangu ikiharibika sana sana.
Hapo kabla ya kuja Iringa, nilikuwa naishi Pwani. Nilikuwa sipaki mafuta na ngozi ilikuwa nzuri tu. Sasa baada ya kuja Iringa na kutokana na baridi nimekuwa napaka mafuta ya mgando ili kufanya ngozi isiwe kavu lakini bado haisaidii.
Naweza kupaka mafuta lakini baada ya nusu saa yale mafuta yanakauka na ngozi kuwa kavu kama mwanzo.
Je, ni mafuta au kitu gani kizuri cha kupaka au kutumia ili kuifanya ngozi iwe nzuri?
Rangi;- Maji ya kunde.
Jinsia;- ME
Mbona km mepesi sanaNiliwahi kusikia mafuta ya nazi ndiyo mazuri zaidi. Niliwahi kupita Njombe kikazi nikakaa pale wiki kilikuwa kipindi cha baridi nilipapenda sana.
Mbona km mepesi sana
Na kwenye baridi kali yanaganda
hadi uyeyushe na warm water
Pamoja sana mkuu!Niliwahi kusikia mafuta ya nazi ndiyo mazuri zaidi. Niliwahi kupita Njombe kikazi nikakaa pale wiki kilikuwa kipindi cha baridi nilipapenda sana.
Tafuta mafuta ya mgando ya Nivea pure ukikosa basi chukua mngando vasseline nyeupe. Hayo mafuta ni mazuri sana kwa ngozi na hayana chemicals nyingi.
Asante sana mkuuTafuta mafuta ya mgando ya Nivea pure ukikosa basi chukua mngando vasseline nyeupe. Hayo mafuta ni mazuri sana kwa ngozi na hayana chemicals nyingi.
Pamoja sana mkuuTafuta mafuta ya mnyonyo. The best
Ni noma sana mkuu hasa hii mikoa ya nyanda za juuMimi na baridi NI tofauti kabisa.
Na huu mwezi wa sita uwa siupendi kabisa
Pamoja sana mkuu, nitafuata huu ushauri wako mwenyeji wangu π π π! Lotion ipi pia itafaa mkuu?Nunua glycerin changanya kwenye lotion yako, nunua Vaseline pia paka kwa juu baada ya kupaka lotion yako yenye mchanganyiko wa glycerin, baada ya wiki njoo nishukuru.
Karibu Iringa, Karibu Frelimo