Ngugi wa Thiong'o alikuwaje kiboko ya mabeberu huku akiishi kwa mabeberu badala ya Afrika?

Kama ilivyo kwamba sio kila mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM ni mwana CCM wa ukweli au anaamini sera na siasa za CCM, Hivyo vivyo sio kila muingereza/mmarekani ni beberu au anaamini katika ubeberu. Kuna waingereza wengi tu wanaamini siasa za ujamaa. Vile vile kuna wana CCM wengi tu ni mabeberu wengine wako tayari kutoa roho za watu wasio na hatia kafara za kichawi au kuwapoteza wapinzani wao ili waendeleze ubeberu wao.
 
Kama alikuwa mbaya kwa wazungu kwa nini aliishi kwao?
Wenzetu hawana mikunjo kiivo kama sisi ambao mtu akiwa na akili nyingi tunamhesabu ni adui wa taifa
 
Hauwezi kua mwiba wa mabeberu kama hujawahi kuishi kwao au huishi kwao,maana ukiishi nao unawajua kwa undani na unapata exposure pia. Huwezi kua mwiba wa mabeberu ukawa unaishi africa au bongo, nyie hamuoni wabongo wanavyokuaga tu wakikutana na mabeberu mikia wanaingiza matakoni wanakua wanyonge kuanzia waliosoma hadi hata wasio soma.Wabongo wanaogopa sana ngozi nyeupe sijui tatizo ni lugha ila kwa sisi wabongo tunaoishia downtown New york tunaweza kula sahani moja na mabeberu.. kutembea ni kujifunza.
 
Naona wazungu hawana ujinga wa kuunda "kikundi kisichojulikana " ungekuta wangeshammaliza.
 
Huyu jamaa anayritwa Ngugi wa Thiong'o kama walivyo activist wengi ambao nawaona fake, alikuwa akijinadi na kuitwa pia mkosoaji wa mabeberu, akijidai kukosoa mifumo ya elimu na lugha ya Kiingereza eti ni kutukuza mabeberu
Hadi akaamua kuandika kwa Kikuyu vitabu vyake badala ya English lengo eti ni ku resist ubeberu.!

Cha ajabu huyu mtu alikuwa akiishi kwa mabeberu, yaani nchi yake na nchi zote 54 za Africa kaziona ni kama takataka akaamua kulowea kwa mabeberu huku aki promote lugha ya kabila lake la Kikuyu.

Contradiction moja kubwa sana
Hakua kiboko ya mabeberu
 
Hauwezi kua mwiba wa mabeberu kama hujawahi kuishi kwao au huishi kwao,maana ukiishi nao unawajua kwa undani na unapata exposure pia. Huwezi kua mwiba wa mabeberu ukawa unaishi africa au bongo, nyie hamuoni wabongo wanavyokuaga tu wakikutana na mabeberu mikia wanaingiza matakoni wanakua wanyonge kuanzia waliosoma hadi hata wasio soma.Wabongo wanaogopa sana ngozi nyeupe sijui tatizo ni lugha ila kwa sisi wabongo tunaoishia downtown New york tunaweza kula sahani moja na mabeberu.. kutembea ni kujifunza.
Angekuwa mwiba kweli wangeshamuondoa, kama alikuwa anakaa huko na bado akawa salama basi alikuwa hana effect yoyote kwao ama alikuwa feki
 
Ubeberu ni Nini labda tuanzie hapo ?

Pili kwa yeye kuishi huko huenda ndio kulimfanya kuweza kuona a different and full picture kuliko vinginevyo...; Kwahio Ulitaka awe Mbaguzi na kuwachukia hao mabwana au afanye alichofanya kwa kuelezea vitu katika difference perceptions kwa kupinga Imperialism ?

Kwamba alipinga their way of life au alinga imperialism wanayofanya na marginalization as well as kuwaambiwa watu kwamba vyao ni vya kipuuzi (If its all white then its All right)!!!!!
Jamaa hakuenda huko kwa kwenda kuchunguza sijui kupata perspective, ni kuwa alifukizwa nchini kwao, akaenda kuomba ukimbizi huko Ulaya
Jamaa anachukia sana mambo ya Ulaya na utamaduni wake hadi anasema Waafrika hawafai kujifunza Kiingereza sababu ni lugha ya kikoloni, (japokuwa vitabu vyake aliandika kwa Kiingereza!) lakini yeye alienda kuweka makazi kwa hao wakoloni badala hata ya nchi mojawapo ya Africa
 
Je alikuwa anapinga Ulaya au sehemu yoyote kupokea wakimbizi au anapinga Imperialism ? Are the two the same ?

Imperialism is the maintaining and extending of power over foreign nations, particularly through expansionism, employing both hard power (military and economic power) and soft power (diplomatic power and cultural imperialism). Hapo kwenye utamaduni ndio kuna mpaka lugha

Jamaa anachukia forcing one over the other angesema wasijufunze na yeye asingejifunza ila alichopinga ni watu kuambiwa lugha zenu zinaleta utanganisho (division) na English ndio inawaunganisha..., Sasa kwa mtu aliyekuwa na kuona mambo ya MauMau unategemea angekuwa na fikra zipi ?

Ngugi wa Thiong'o strongly advocates for the use of African languages in literature, particularly in the context of post-colonial Africa. He argues that English, while useful, should not be the sole language of African expression, as it is a language of the colonizer and can perpetuate colonial power structures. He believes that African languages are crucial for preserving cultural identity and fostering a sense of self-determination.
 
Wanaijeria na wakenya ni watu vichwani mwao wanawazaga wazungu na ulaya. Cha ajabu huko waendako hawawi matajiri kama hao wazungu. Mambo ya kukimbilia ulaya ufanikiwe ilikuwa ni scum kwa watu weusi wawaze ulaya waaache kuijenga Afrika ili wazungu waje wakute upinzani mdogo. Imagine mtu kama Chinua angekuwa hajawahi enda ulaya halafu ni mbunge au kiongozi yoyote yule.
Maelfu ya wasomi kama Chinua walikimbilia ulaya na kujikuta wajakazi wa wazungu hivyo hawana mchango wowote ktk kulijenga bara la Africa kazi yao kukosoa wakiwa huko.
Nduguyangu kabla ya kuwadharau jiulize kitugani kiliwakimbiza? Kumbuka wengi wao walikuwa wapiganiahaki na mageuzi kipindi chao na vipindi hivyohivyo serikali nyingi ziliongozwa kwa mikono ya chuma mfano Nigeria na Kenya kwa kipindi cha harakati zao.
 
Kwamba literary works walizoandika hao Mabwana kina Chinua, Bwana Ngugi n.k. hayana mchango wowote ? Really ?!!!!

Unataka binadamu afanye nini ili uone mchango wake ? Yaani muunganiko wa fikra zao kwenye karatasi zimeweza kuchangamsha fikra na mawazo ya wengi huko mashuleni na majumbani sasa sijui wewe neno mchango ni nini ?
 
Je alikuwa anapinga Ulaya au sehemu yoyote kupokea wakimbizi au anapinga Imperialism ? Are the two the same ?

Imperialism is the maintaining and extending of power over foreign nations, particularly through expansionism, employing both hard power (military and economic power) and soft power (diplomatic power and cultural imperialism). Hapo kwenye utamaduni ndio kuna mpaka lugha

Jamaa anachukia forcing one over the other angesema wasijufunze na yeye asingejifunza ila alichopinga ni watu kuambiwa lugha zenu zinaleta utanganisho (division) na English ndio inawaunganisha..., Sasa kwa mtu aliyekuwa na kuona mambo ya MauMau unategemea angekuwa na fikra zipi ?

Ngugi wa Thiong'o strongly advocates for the use of African languages in literature, particularly in the context of post-colonial Africa. He argues that English, while useful, should not be the sole language of African expression, as it is a language of the colonizer and can perpetuate colonial power structures. He believes that African languages are crucial for preserving cultural identity and fostering a sense of self-determination.
Mzee kila kabila likoanza ku promote lugha yake kama huyo jamaa alivyokuwa akifanya itakuaje kwenye umoja na utanagamano, hasa ukizingatia matatizo mengi Africa sasa hivi yanaletwa na ukabila?

Na kama watu ni wabaya, haina haja ya kukaa kwa watu unaoamini ni wabaya wakati nafasi ipo nyingi tu kwa watu unaoamini ni wazuri, otherwise ni unafiki
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Nduguyangu kabla ya kuwadharau jiulize kitugani kiliwakimbiza? Kumbuka wengi wao walikuwa wapiganiahaki na mageuzi kipindi chao na vipindi hivyohivyo serikali nyingi ziliongozwa kwa mikono ya chuma mfano Nigeria na Kenya kwa kipindi cha harakati zao.
Kwa nini wasikimbilie nchi kama China hivi au Tanzania, maana wao wanaona matatizo ya dunia yanaletwa na wazungu halafu wanakimbilia tena kwa wazungu wakipata misukosuko
 
Hauwezi kua mwiba wa mabeberu kama hujawahi kuishi kwao au huishi kwao,maana ukiishi nao unawajua kwa undani na unapata exposure pia. Huwezi kua mwiba wa mabeberu ukawa unaishi africa au bongo, nyie hamuoni wabongo wanavyokuaga tu wakikutana na mabeberu mikia wanaingiza matakoni wanakua wanyonge kuanzia waliosoma hadi hata wasio soma.Wabongo wanaogopa sana ngozi nyeupe sijui tatizo ni lugha ila kwa sisi wabongo tunaoishia downtown New york tunaweza kula sahani moja na mabeberu.. kutembea ni kujifunza.

NI UNAFIQ TU HUU.
 
Kwamba literary works walizoandika hao Mabwana kina Chinua, Bwana Ngugi n.k. hayana mchango wowote ? Really ?!!!!

Unataka binadamu afanye nini ili uone mchango wake ? Yaani muunganiko wa fikra zao kwenye karatasi zimeweza kuchangamsha fikra na mawazo ya wengi huko mashuleni na majumbani sasa sijui wewe neno mchango ni nini ?
The river between imekusaidia nini ?
Wale ambao hawajawahi kusoma the river between na wewe uliesoma mna tofauti gani?
Halafu usome kwenye vizuri kwenye mistari kabla hujanikosoa. Comment yangu imeendana na mtoa mada. Ishu kubwa wao kukimbilia ulaya badala ya kuzijenga nchi zao, sasa uzalendo wao upo wapi au uzalendo ni kuishia kuandika vitabu bila kutekeleza kwa vitendo ?.
 
The river between imekusaidia nini ?
Hujui faida ya Literature ?
Wale ambao hawajawahi kusoma the river between na wewe uliesoma mna tofauti gani?
Huyu na wengine wengi wameongezea idadi ya literary works..., labda swali lingekuwa kuna faida au hasara ya kupoteza kazi za huyu bwana (kuwepo kwake au kutokuwepo kwake).., na fact kwamba hata wewe unatambua kazi zake ni uthibitisho tosha wa impact yake
Halafu usome kwenye vizuri kwenye mistari kabla hujanikosoa. Comment yangu imeendana na mtoa mada. Ishu kubwa wao kukimbilia ulaya badala ya kuzijenga nchi zao, sasa uzalendo wao upo wapi au uzalendo ni kuishia kuandika vitabu bila kutekeleza kwa vitendo ?.
Kwahio sasa tunaongelea uzalendo wao na sio impact yao ? Kutekeleza kwa Vitendo ukimaanisha nini ? Ushasikia msemo wa a pen is mightier than the sword.... Na mtu kama Chinua alikuwa frustrated na kinachoendelea baada ya independence ukizingatia na corruption vitu ambavyo mpaka sasa vinatutafuna.....

Kila mtu na nafasi yake
 
Hujui faida ya Literature ?

Huyu na wengine wengi wameongezea idadi ya literary works..., labda swali lingekuwa kuna faida au hasara ya kupoteza kazi za huyu bwana (kuwepo kwake au kutokuwepo kwake).., na fact kwamba hata wewe unatambua kazi zake ni uthibitisho tosha wa impact yake

Kwahio sasa tunaongelea uzalendo wao na sio impact yao ? Kutekeleza kwa Vitendo ukimaanisha nini ? Ushasikia msemo wa a pen is mightier than the sword.... Na mtu kama Chinua alikuwa frustrated na kinachoendelea baada ya independence ukizingatia na corruption vitu ambavyo mpaka sasa vinatutafuna.....

Kila mtu na nafasi yake
Mkuu ningefundishwa kufuga vizuri mifugo ningekuwa bora zaidi kuliko kusoma zile hadithi. Zilinipotezea mda sikujua nilikuwa mtoto, siku hizi sifanyi ujinga wa kusoma hekaya kama zile. Hizo ndio ilimu zilizodumaza waafrika wengi.
Kama unaendelea kujazua watoto wako vitabu vya aina hio, basi nakupa pole sana.
Sasa kama hivyo vitabu viliamsha akili yetu mbona bado tuna abudu wazungu na lugha zao, tena rika la hao kina ngugi ndio wazungu kama mungu wao.
Wazungu wachina wanafundisha watoto wao teknolojia sisi tumejaza literature. Sikubaliani na hayo mavitabu, yalitakiwa yasomwe kwa hoby sio lazima. YAMETUANGAMIZA ndio maana tumekuwa watumwa wa wazungu, wachina, warabu na wahindi. Tuna babaisha babaisha tu mambo hatuna maarifa ya maana.
 
Mkuu ningefundishwa kufuga vizuri mifugo ningekuwa bora zaidi kuliko kusoma zile hadithi. Zilinipotezea mda sikujua nilikuwa mtoto, siku hizi sifanyi ujinga wa kusoma hekaya kama zile. Hizo ndio ilimu zilizodumaza waafrika wengi.
Kufuga ulikatazwa kujifunza ? Kwahio kesho utasema hata Pele asingecheza mpira bali angekufundisha kulima mihogo !!!; Huyu bwana na wengine kama yeye wali play their part (hata kina Agoro Anduru) kwa tanzania kwahio hata kutoa entertainment kwa watu kama wewe mkitoka kufuga mifugo vizuri mpate cha kusoma.., au ukishafuga hata entertainment haipo tena ?
Kama unaendelea kujazua watoto wako vitabu vya aina hio, basi nakupa pole sana. Sasa kama hivyo vitabu viliamsha akili yetu mbona bado tuna abudu wazungu na lugha zao, tena rika la hao kina ngugi ndio wazungu kama mungu wao.
Nina mashaka sana na uelewa wako, Moja vitabu hivi havikwambii ufanye hiki wala kile au ukubaliane na chochote kwenye kitabu kama hicho bali inakuongezea uwezo wa kuangalia mambo katika different perspective na hata kupinga kwamba fulani hapa na pale alikosea....

Vitabu hivi vinatumia (allegory) mfano animal farm kuelezea jinsi ya watu wanavyonyonya wengine (walamba asali) kwa justification ya kwamba wao ni viongozi..., kwahio havikupi solution pale vinaonyesha umbwe fulani sehemu fulani kwa macho ya mwandishi (ofcourse angeweza kutumia muda wake kunywa mbege lakini alimua kuutumia kuandika) sasa je asingeandika ndio wewe ungebadilika ? Au alichoandika ndio kimekufanya usijifunze kufuga ?!!!;
Wazungu wachina wanafundisha watoto wao teknolojia sisi tumejaza literature. Sikubaliani na hayo mavitabu, yalitakiwa yasomwe kwa hoby sio lazima. YAMETUANGAMIZA ndio maana tumekuwa watumwa wa wazungu, wachina, warabu na wahindi. Tuna babaisha babaisha tu mambo hatuna maarifa ya maana.
Kwamba wazungu na wachina hawana literature ?!!!!!! Sasa niambie nani kati yangu mimi na wewe anaabudu wazungu..., kwamba kabla ya wazungu Afrika kulikuwa hakuna teknolojia ? Unajua kuna parts of Afrika Civilization ilianza hata kabla ya huko Western ?
 
Back
Top Bottom