Ngumi za mtaani mmepewa uwanja unaanza vipi kuongea maneno, kijana kaambulia aibu kwa kushushiwa kipigo kikali hadharani, usipende kuongea ikikutokea!

Ngumi za mtaani mmepewa uwanja unaanza vipi kuongea maneno, kijana kaambulia aibu kwa kushushiwa kipigo kikali hadharani, usipende kuongea ikikutokea!

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Nimetoka zangu kazini nikaona niende kununua mahitaji kadhaa sokoni.

Ghafla nikaona tunaambiwa na vijana jamani mpishe hii njia kidogo iwe wazi kwa muda, nilidhani labda kuna emergency nikasimama.

Ghafla wakaingia vijana wawili kumbe ni ugomvi.

Moja wao kavaa vizuri tu sikuweza kumdhania, akaanza kumuongelesha mwenzie huniwezi, hata hajmaliza neno akarushiwa ngumi nzito sana akadondoka chini, hapo alipigwa kipigo cha mbwa koko ikabidi wawaachanishe tu.

kijana kaambulia aibu kubwa mbele ya hadhara, kaondoka uso chini kwa kosa kubwa alilofanya la kuongea kwenye street fight.

Kwa bahati nzuri hakuna silaha zilizotumika, vijana wamemalizana kiume kwa kuzichapa kavu.
 
Back
Top Bottom