Ngurumo: Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu

Well prepared ! Mungu akubariki sana.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Hapa kosa kubwa linafanywa na viongozi wetu wa kiimani, sio mara ya kwanza kwa huyu mzee kutumia nyumba za ibada na kueleza mambo yanayo poteza watu kinyume na lengo kuu la nyumba hizo. Kwa kawaida yeyote anae simama ndani ya nyumba ya ibada na kuhutubia/kuhubiri ina maanisha ni miongoni mwa wenye kuendesha ibada husika kwa siku hiyo, sasa huyu mzee anapewa nafasi hiyo kama nani?
Kama anapewa nafasi kama kiongozi wa serikali, basi viongozi wa dini lazima watambue kwamba serikali haina dini hivyo viongozi wake hawana sifa yakuongoza ibada kwa mujibu wa nafasi zao.
Nyumba za ibada zina utaratibu na viongozi wa kiimani katika kuongoza ibada, muumini yeyote anae ingia kwenye za ibada inatakiwa abaki kuwa muumini kama waumini wengine.
 
 

Attachments

  • IMG-20210221-WA0037.jpg
    67.8 KB · Views: 2

Ila Braza una akili sana......basi tu hatuna mfumo mzuri wa kuwapa nafasi wazaliwa wetu wa kwanza, yaani wale ambao bible inawaita malango!
 
Namheshimu sana rais magufuri kama mkuu wa nchi ,kama mkubwa ki umri kunizidi na mm mi kama mtoto wake kwakwe ,lakn hili suala la corona kweli anatupeleka pabaya .kwanin watu wasipimwe? Takwimu za vifo zitangazwe ? Watu wasisitizwe kuchukua tahadhar n.k

Ifahamike binadamu tusipo kumbushwa huwa tunajisahau sanaa ndo maana hata shule ikitangazwa test ndo watu husoma sanaaaa.

Kama viongozi wanajukumu kubwa sanaaaa kutilia mkazo hili suala na sio kuchukulia poa poa,

Tunaweza tusiweke lock down lkn misingi ya usalama ikiimalishwa watu watanusulika .
 
Mzee watampaka matope sana lakini ni genius kwenye hili....halafu naona mnajisahau sana Mzee asingizie barakoa za nje zina walakini ili nn?zile experiment za mapapai mmezisahau? Siyo kila anachosema mzungu ni sahihi,..au anawatakieni mema hivi kule walikokufa makumi na maelfu kwa mzungu kwnn ndio pasifatiliwe sana? Na wewe Mkuu unalalamika ulitaka mzee awe anakuja kukusanitize? Akunawishe mikono na barakoa?tunalalamika sana badala ya kushauri....sijawahi kuona ugonjwa uliopona kwa ulalamishi.
 
Wapumbavu hamuishi duniani
 

Mara kadhaa walinzi wake wamekuwa wanaingilia liturjia na kusababisha vurugu isiyo ya lazima kanisani.

Waamini wanasemea chini chini tu, lakini wanakerwa.
 
Hebu tuondolee huu upumbavu wako. Kama ni mkweli atuwekee huo ushahidi hadharani wa kuonyesha ni nchi ipi iliingiza barakoa ili ituue Watanzania ziliingia Nchini. Na ni nani aliyezigundua kama si salama, zilifanywa nini na kwanini hakuishtaki nchi husika katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kuingiza nchini Barakoa hatarishi.
 
Umeandika vizuri sana sana kongole mkuu BAK
Mwandishi wa hii story na origin yake iko hapa👇🏾...
 
Reactions: BAK
Hana ugenius wowote zaidi ya kukariri tu.
Jiulize n chanjo ngapi umechomwa mpaka unafikia huo umri? Wazungu wangeamua kutumaliza ingekuwa kazi rahisi mno kama kuteleza kwenye ganda la ndizi.
Muelezeni huyo ndugu yenu hana leadership skills zozote.
Mnampamba tu ili muambulie chochote enyi wachumia tumbo.
Hana unyenyevu wowote anajipa utukufu na mamlaka kama Mungu ndo mana anaongea chochote anachojisikia altareni mbele ya yesu wa ekaristi.
Huyu n mpagani tu kanisa limtenge Aache kuitumia mimbari ya kanisa vibaya.
 
Tumeisikiliza hotuba vizuri,hakuna mahala ambapo anawaswaga na kuwapelekesha mapadre na maaskofu katoliki. Rais ametoa tahadhali juu ya kutumia barakoa zinazostahili.

Mtoa mada huna lolote,endelea kuosha vgombo vya wazungu huko ughaibuni.
Kanisa LA Leo mkuu limepotoka sana,unampaje mike Muumini ahutubie siasa kanisani?,

Si aite press conference atoe matamko,angalia sasa amewananga mpaka Maas kofu.
 
Nimeisikiliza, maelezo ya ngurumo yanawakilisha kila alichokuwa akichokisema pamoja na anachokifikiri Jiwe hata jioni hii.
Ngurumo anabadilisha alichoongea Rais kwenda katika mtizamo wake yeye ili kupotosha Jamii. Jiulize kama issue ni Corona ni nchi gani ambayo imeweza kuicontrol kwa kuvaa barakoa na lockdown? Mbona tulivyoacha kuvaa barakoa mwaka jana corona ilipungua sana? Kwann baada ya chanjo tu corona imekuja tena kwa kasi nyingine? Mbona hajajibu hoja ya Rais kwamba mijini ndo kwenye Corona na siyo vijijini? Huyo mwandishi ni mpuuzi na mwenye chuki binafsi na magufuli ndo maana alikimbia nchi hii kwenda kufanya kazi ya kuchamba vizee vya kizungu.
 
Mungu amsaidie huyu mtu sijui ana kichwa cha aina gani, nakubaliana na mwandishi anaposema ukiona wanakufa wakubwa ujue huko chini ndio wamepukutika wakutosha, Mungu atusaidie.
Ndani ya wiki nne zilizopita nimepoteza ndugu, marafiki na jamaa wa karibu zaidi ya watano.
Naturally hasira zinaenda kwa yule mwenye dhamana na afya ya jamii, anayeshindwa kuchukua tahadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…