Nguvu inawezaje kutengeneza object?

Nguvu inawezaje kutengeneza object?

NILICHOGUNDUA NI KUWA HUWEZA LETA THREAD HAPA HATA KAMA IMEPINDA IKOSE WACHANGIAJI
 
Upepo huvuma,hatuuoni ila tunaona matokeo yake.Vilevile Mungu hatumwoni kwa macho lakini uwepo wake unadhihirika katika mpangilio wa umbaji mfano solar systems,galaxies na kadhalika zilivyopangilika.Hata wewe mwili wako unavyofanya kazi.
 
Kutembea juu ya maji nguvu imeundaje object..? vilevile na kupaa kwa mtume nguvu imeundaje..? object
Kwa kuanzia Soma biblia Takatifu kitabu cha Yoh. 1:1,5.(nguvu kiimani ni neno litokalo kwa Mungu).
 
oel200e
mkuu asante kwa udadavuzi wako lkn kama wewe unaamini ktk Mungu kwanini usinipe majibu tu..?

Majibu ya Mungu kiukweli ni suala la theolojia na imani. Kwanza dini yeyote inakutaka kuiikiri imani ya kwanza kuna "kitu" au "nguvu" yenye akili na intelijensia iitwayo "MUNGU".....bila kukiri hivi, haina maana ya kukueleza hiyo "nguvu" inaundaje vitu. Inakubidi ukubali kwanza uwepo wa hii "nguvu" iitwayo mungu ndio tuendelee.

Mimi binanfsi naamini katika mungu, haina maana siamini katika sayansi pia, lakini najaribu kutokuchanganya kati ya hivi viwili, maana haviendani.

Kwa mfano, Kiimani; uwepo wa mungu unatosha kuelezea kila kitu. Mungu aliumba vitu kwa neno lake tena kwa siku sita.Japo biblia haiendi kina zaidi ya hapo, unaweza kuona kwamba, hata mungu alifanya kazi (sio maneno tu) la sivyo kwa nini asiseme vyote kwa pamoja? au siyo??..kwa hivyo, hata vitabu vya dini havisemi sana lakini vinatupa tumaini la kwamba vitu vyote tunavyoviona ni matokeo ya "nguvu" fulani iliyovipanga kwa pamoja hivyo HAKUNA KITU KILICHOTOKEA KWA AJALI. Kwangu mimi, haya ndio maudhui makubwa zaidi ya vitabu vya dini.

Wakati huo huo, sayansi haijaweza bado kueleza nini chanzo cha maisha au ulimwengu. Theory iliyopo sasa, ambayo wengi wanaiamini (inachekesha kiasi fulani) ni "big bang theory" amabayo inaeleza uumbwaji wa ulimwengu kwa kutokea kwa mlipuko wa nguvu, ambao ulizalisha "nguvu" tunazoziona yaani maada (matter=liquid, gas, solid, plasma) na tusizoziona (dark matter)...hata hivyo bado hatujui nini kilisababisha big bang au kilianza nini kabisa. Na kuhusu maisha, ni kwamba yalitokea tu kwa ajali, tunaishi ili tuishi an baada ya kufa hakuna kingine, hata jua na dunia kuna siku vitakufa.

Mfano mwingine ni ukiangalia DNA na mfumo wake. Wakati wanasayansi wengi wameweza kutengeneza elements ndogo zinazoweza kutengeneza DNA, na hata kufanya experiment zinazofanana na kuubwa kwa dunia (volcanic eruption and lighting) ambazo ndio zilisababisha kutengenezwa kwa DNA..hakuna anayeweza kuelezea kivipi hizo element ndogo ziliungana kutengeneza uhai wa cell za mwanzo kabisa za maisha.

Kwa kifupi, sayansi haijaweza mpaka leo kujibu swali la "uhai" ni nini..mfano kisayansi; virus ni kundi la viumbe visivyo hai sawasawa na jiwe, ndoo n.k japo akiingia mwilini unaumwa kama vile una bakteria ambae ni kiumbe hai.

Hapa ndio wengi wanarudi katika suala la Mungu wa kidini.Lakini pia, zaidi ya hapo tusubiri tu kwa maana sayansi inakua na inajibu maswali mengi sana ambayo hata mwanzo watu wa vitabu vya dini walisema ni Mungu tu, lakini sasa tunajua tofauti. Ndio maana mimi nafikiri Mungu anabaki kuwa ni suala la Imani tu yale mambo yenye kuelekea kwenye utashi na fikra, wala asihusishwe na sababu za kidunia ambazo kwa wakati fulani tumeshindwa kuzifafanua.
 
Wanasayansi wameshindwa kuelezea chanzo cha ulimwengu na vilivyomo,zaidi ya kutoa madai.

Mola huumba kwa kusema "Kuwa",basi kitu kinakuwa.
Unaweza kuthibitisha Mola yupo na huumba kwa kusema tu na hizo si hadithi tu?
 
Usije kupoteza muda hata siku moja ukataka kuelezewa chanzo cha ulimwengu kisayansi,wanasayansi wanatumia dhana.

Pia kuna vitu vingine kwa kutumi akili na milango ya fahamu peke yake huwezi kuvidiriki katu.

Hapa inafanya kazi ni IMANI.
Sasa hiyo imani nayo, kujua umani ipi ni nzuri na ipi ni mbaya unatumia nini kujua?

Makalio?
 
Kumbe umeuliza katika post niliyonukuu! sasa iweje uulize swali na hapo hapo useme sijajibu?
Ulitaka niseme hujajibu kabla sijauliza swali?

Una hakika hiyo ni mara ya kwanza?

Ulisoma ulichonukuu kabla ya kujibu au ulijibu tu?
 
Upendo ni nini kwako? Kujua na Kuweza yote ni nini kwako? Msingi wa hoja yako ni dhaifu kwani nilishakuambia Mungu HAWEZI kufanya upumbavu. Pia kama ungekuwa unalenga kujifunza ungekumbuka kuwa nilikuambia, Upendo ni tokeo la Kutii sheria za Mungu, wala si kugawa chakula kwa masikini na wagonjwa ILA TU KAMA UNATII SHERIA YA MUNGU.

Upendo si kumuumba tu binadamu like robot je ni zao la sheria? Ipi ni tofauti ya nafasi ya binadamu na Ujumbe vingine ulimwenguni?
Kwa sheria na nguvu ulimwengu ulifanyika UWEZO JUU YA ULIMWENGU , kwa sheria na nguvu ulimwengu unaishi UPENDO, kwa Upendo ulimwengu unadumu KUSUDIO/KUDRA.
Anaita sasa.
Unafahamu kusema nguvu "hawezi" ni kujichanganya?

Hii nguvu ni personal god?

Inasikiliza maombi ya watu na kuingilia ili kusaidia watu?

Mbona hujibu maswali?
 
Unafahamu maana ya swali ni nini?

Sitegemei ufahamu. Unatumia makalio kufikiri.
Nina fahamu maana ya swali na nina elimu ya vipi nijibu maswali na wakati gani nijibu na wakati gani nisijibu.

Wasomi wetu wanasema "Bora ufanye mazungumzo na wajuzi elfu mtafikia muafaka kuliko kufanya mazungumzo na mjinga mmoja mtakwazana"

Nimekupa haki yako mzee.Kwa hapa nimefunga mazungumza na wewe.

Kisha nimekupa amani.Nimemaliza.
 
Nina fahamu maana ya swali na nina elimu ya vipi nijibu maswali na wakati gani nijibu na wakati gani nisijibu.

Wasomi wetu wanasema "Bora ufanye mazungumzo na wajuzi elfu mtafikia muafaka kuliko kufanya mazungumzo na mjinga mmoja mtakwazana"

Nimekupa haki yako mzee.Kwa hapa nimefunga mazungumza na wewe.

Kisha nimekupa amani.Nimemaliza.
Hujamaliza. Wewe huna haki ya kumaliza mjadala ambao haukuhusu wewe tu.

Sema unakimbia. Kwa sababu huwezi kutetea kuwapo kwa Mungu ambaye hayupo.
 
Mimi sijui ulimwengu umefanyikaje, nataka kuangalia uwezekano wa unachosema, kama ni kitu kinachowezekana kimantiki au hakiwezekani.

Katika kuangalia kama kinawezekana au hakiwezekani, nataka kuijua hiyo asili na nguvu ikoje ili niipime vizuri.

Moja ya kitu kitakachonisaidia kuipima vizuri, ni kujua kama hiyo asili ina upendo au haina.

Ndiyo maana nikakuuliza, hiyo asili ina upendo au haina?

Kwa nini swali hili linakuwa gumu sana kwako kujibu?
Sasa kama hata hujui ulimwengu umefanyikaje, ni wazi hata msingi wa hoja zako ni batili. Hujui unachokisema ama unakana kwa makusudi ili kuendeleza ubishi.

Mungu ni Nguvu na Sheria zilizofanya Ulimwengu, sifa ya kwanza ya hiyo asili, ni yenyewe ndio The Creator, mengine yanafuata. Hii ni hatua ya kwanza ya kukuelewesha, jibu kama unatambua uwepo wa Asili iwe yenye upendo ama laa. Unachoogopa ni nini hasa? Dhamira yako ni ipi hasa, je kuongeza maarifa au kuendelea kubaki kuwa mpingaji tu siku zote?


Hakuna swali gumu utoalo, ila tu unapaswa kuelekezwa kwa hatua, nataka tuanze hapo kwanza, kumbuka mimi ndiye nitakaye kukuelekeza.
 
Sasa kama hata hujui ulimwengu umefanyikaje, ni wazi hata msingi wa hoja zako ni batili. Hujui unachokisema ama unakana kwa makusudi ili kuendeleza ubishi.

Mungu ni Nguvu na Sheria zilizofanya Ulimwengu, sifa ya kwanza ya hiyo asili, ni yenyewe ndio The Creator, mengine yanafuata. Hii ni hatua ya kwanza ya kukuelewesha, jibu kama unatambua uwepo wa Asili iwe yenye upendo ama laa. Unachoogopa ni nini hasa? Dhamira yako ni ipi hasa, je kuongeza maarifa au kuendelea kubaki kuwa mpingaji tu siku zote?


Hakuna swali gumu utoalo, ila tu unapaswa kuelekezwa kwa hatua, nataka tuanze hapo kwanza, kumbuka mimi ndiye nitakaye kukuelekeza.

Nitarudi kwenye hesabu, hesabu inafanya mambo yenye longolongo nyingi kuwa clear.

Umeema kama sijui ulimwengu umefanyikaje, msingi wa hoja zangu ni batili.


Kimsingi unachoniambia ni kwamba "kama hujui square root ya mbili ni nini, msingi wa kukataa kwamba square root ya mbili ni kumi ni batili".

Si kweli.

Sihitaji kujua jibu la swali ili kujua kwamba jibu fulani ni batili.

Naweza kuwa sijui square root ya mbili ni nini. Lakini nikajua kwamba square root ya mbili ni lazima iwe ndogo kuliko mbili, hivyo jibu lolote lililo kubwa kuliko mbili ni batili.

Naweza kulijua jibu batili bila hata ya kujua jibu ni nini.

By the way, unafahamu square root ni nini?

Nisije kuwa na assume tu unafahamu square root ni nini wakati hata hujui square root ni nini.
 
Nitarudi kwenye hesabu, hesabu inafanya mambo yenye longolongo nyingi kuwa clear.

Umeema kama sijui ulimwengu umefanyikaje, msingi wa hoja zangu ni batili.


Kimsingi unachoniambia ni kwamba "kama hujui square root ya mbili ni nini, msingi wa kukataa kwamba square root ya mbili ni kumi ni batili".

Si kweli.

Sihitaji kujua jibu la swali ili kujua kwamba jibu fulani ni batili.

Naweza kuwa sijui square root ya mbili ni nini. Lakini nikajua kwamba square root ya mbili ni lazima iwe ndogo kuliko mbili, hivyo jibu lolote lililo kubwa kuliko mbili ni batili.

Naweza kulijua jibu batili bila hata ya kujua jibu ni nini.

By the way, unafahamu square root ni nini?

Nisije kuwa na assume tu unafahamu square root ni nini wakati hata hujui square root ni nini.
Mfano wako ni batili kabisa ndugu, kwa madai yako ya kutojua ulimwengu umefanyikaje ni sawa na kutojua square root nini, ajabu ukaambiwa square root ya 2 ni 5 ukaanza kupinga wakati hujui square root ni nini.


Duuuuuh nakumbuka mwl wangu na hizo habari za Vipeo na Vipeuo, vilinisumbua sana kwa kweli.
 
Mfano wako ni batili kabisa ndugu, kwa madai yako ya kutojua ulimwengu umefanyikaje ni sawa na kutojua square root nini, ajabu ukaambiwa square root ya 2 ni 5 ukaanza kupinga wakati hujui square root ni nini.


Duuuuuh nakumbuka mwl wangu na hizo habari za Vipeo na Vipeuo, vilinisumbua sana kwa kweli.

Kwa hiyo mtu ambaye hajui square root ya mbili ni nini, lakini anajua kwamba square root ni lazima iwe ndogo zaidi ya hiyo namba inayotafutiwa square root, akiambiwa kwamba square root ya 2 ni 5, hawezi kuona kwamba 5 haiwezi kuwa square root ya 2 kwa sababu 5 ni kubwa kuliko 2?
 
Unaposema Nguvu kwanza unamaanisha nini mkuu?

Pia naomba nikupe mwanga wa tafiti zinavyosema kuhusiana na hali ya kila kitu unachokiona.

Kwanza kabisa nature ya ilimwengu haipo kama wengi wanavyoelewa. Kila unachokiona hakipo kama kilivyo. Wengi waliobahatika kusoma na kufahamu mengi hii sio concept mpya kwao.

Kila kitu unachokiona (matter) vimeundwa au kujengwa na Atoms. Ukiweza kuchukua kitu na kutumia darubini kali saana 10,000 times utaona Atoms. Mfano kama size ya dunia ndio matter atom zake zinaweza kuwa size ya mpira wa Golf ukisema uangalie mfano kwa ration utakayoielewa. Katika uchunguzi wa atom kuna mambo mengi ambayo mpaka sasa Quantum Physics inajaribu kufahamu zaidi kwa sababu Atoms zipo zina tabia tofauti na Matter. Atoms zimejengwa na Electrons ambazo zinazunguka kiini chake kinachoitea Nicleus. Ndani ya kiini kuna proton na neutron.

IMG_1473339484.532037.jpg


Ni kama vile sayari zinavyozunguka jua katika njia yake. Lakini tofauti ya mzunguko wa sayari na jua na mzunguko wa electrons ni kwamba kwenye atom electron zinaweza kuhama njia yake lakini hazibadiliki idadi. Quantum Physics inasema kuwa Ukichukua kila kitu duniani ukachukua atoms zake particle hazijai size ya kiwanja cha mpira cha standard. Na hapo utaona ulimwengu na kila ukionacho ni ILLUSION.

Kiini cha atom ni umeme kuna positive na negative charge. Kama atom ina electron +3 lazima iwe na proton -3 kuweka balance.

Kila kitu kimeindwa na element mbalimbali. Kuna oxygen, hydrogen, helium, carbon na kadhalika. Kila element ina atom na kila atom ina umeme. Tofauti kati ya kitu kimoja na kingine ni mpangilio wa atoms, umeme wa atoms katika vibration yake na idadi ya protons.

Mfano Hydrogen ina atomic number 1 (nadhani mmesoma periodic table).
IMG_1473339906.485178.jpg


Tofauti kati ya hudrogen na element zote ulimwenguni ni idadi ya protons. Hydrogen inayo 1 tu. Inayofuatia ni Helium ina proton mbili, inayofuatia ni Lithium na kuendelea.

Kila unachokiona mfano mti na jiwe vipo na tofauti kwenye atomic particles. Vibration na umeme wa mti na jiwe vinatofautiana na ndio maana unaona ni tofauti. Pia utofauti wake unapelekea utofauti mpaka wa elements. Mfano mti ina Carbon lakini jiwe linaweza kuwa ni Calcium. Kwahiyo utofauti wa kila chenga chenga za ulimwengu ni atomic number. Utofauti wa atomic number umetokana na utofauti wa aina za vibration.

Pia hata Rangi ni vibrations za waves katika hali mbalimbali. As same as sound. They are all energies katika frequency mbalimbali.
IMG_1473340282.103709.jpg


Macho, pua, ubongo, ngozi, sikio na ulimi ni organs ambazo tunazitumia tangu evolution inaanza katika kila kiumbe ili kujua rates za vibration na kutumia ubongo kutafsi kuwa katika forms mbalimbali. Red unayoiona sio red colour ni tafsiri ya ubongo kupitia jicho likasense vibratory frequency na ubongo kutafsiri. Sikio lina sense rate ya vibration kwenye hewa na kukupa frequency kwenye ubongo ukatafsiri.

Hivyo nature ya ulimwengu ni kama mazingaombwe. Imani za Asia zinasema ULIMWENGU HAUPO KAMA UNAVYOUONA. Kutoka katika Element ya kwanza Hydrogen imetengeneza elements zote unazoziona na kila siku nyota zinavyopasuka na kujijenga zinatengeneza elements. Oxygen unayotumia leo hii imetokana na hudrogen iliyokuwa fused na kubadilishwa atoms katika nyota na ndio kazi kuu ya nyota. Kutengeneza elements. Ndio maana wanasayansi wanaamini Hydrogen ndio element ya kwanza kwa sababu imeinda kila element.

Kila kitu ni energy. That energy ndio inayoshikilia ulimwengu na kila particle. Na tunavyotafsiri ulimwengu ulivyo sio kama. Ulivyo bali ni kutokana na mazoea ya kuuelewa ulimwengu tangu tulipozaliwa mpaka sasa.


KWA KUCHUNGUZA NATURE YA ULIMWENGU UTAGUNDUA KUWA MUUMBAJI, CHANZO CHA ULIMWENGU, KILICHOUMBWA, NA KINACHOONA UUMBAJI NI WAMOJA.
 
Back
Top Bottom