Nguvu inawezaje kutengeneza object?

Nguvu inawezaje kutengeneza object?

Mfano wako ni batili kabisa ndugu, kwa madai yako ya kutojua ulimwengu umefanyikaje ni sawa na kutojua square root nini, ajabu ukaambiwa square root ya 2 ni 5 ukaanza kupinga wakati hujui square root ni nini.

Duuuuuh nakumbuka mwl wangu na hizo habari za Vipeo na Vipeuo, vilinisumbua sana kwa kweli.

Square root ya mbili ni
1.414213562373095 sawa na kusema haizidi 1.4
 
Unaposema Nguvu kwanza unamaanisha nini mkuu?

Pia naomba nikupe mwanga wa tafiti zinavyosema kuhusiana na hali ya kila kitu unachokiona.

Kwanza kabisa nature ya ilimwengu haipo kama wengi wanavyoelewa. Kila unachokiona hakipo kama kilivyo. Wengi waliobahatika kusoma na kufahamu mengi hii sio concept mpya kwao.

Kila kitu unachokiona (matter) vimeundwa au kujengwa na Atoms. Ukiweza kuchukua kitu na kutumia darubini kali saana 10,000 times utaona Atoms. Katika uchunguzi wa atom kuna mambo mengi ambayo mpaka sasa Quantum Physics inajaribu kufahamu zaidi kwa sababu Atoms zipo zina tabia tofauti na Matter. Atoms zimejengwa na Electrons ambazo zinazunguka kiini chake kinachoitea Nicleus. Ndani ya kiini kuna proton na neutron.

View attachment 396335

Ni kama vile sayari zinavyozunguka jua katika njia yake. Lakini tofauti ya mzunguko wa sayari na jua na mzunguko wa electrons ni kwamba kwenye atom electron zinaweza kuhama njia yake lakini hazibadiliki idadi. Ukichukua kila kitu unachokiona duniani ukaangalia particle zake hazijak size ya kiwanja cha mpira cha standard. Na hapo utaona ulimwengu na kila ukionacho ni ILLUSION.

Kiini cha atom ni umeme kuna positive na negative charge. Kama atom ina electron +3 lazima iwe na proton -3 kuweka balance.

Kila kitu kimeindwa na element mbalimbali. Kuna oxygen, hydrogen, helium, carbon na kadhalika. Kila element ina atom na kila atom ina umeme. Tofauti kati ya kitu kimoja na kingine ni mpangilio wa atoms, umeme wa atoms katika vibration yake na idadi ya protons.

Mfano Hydrogen ina atomic number 1 (nadhani mmesoma periodic table). View attachment 396339

Tofauti kati ya hudrogen na element zote ulimwenguni ni idadi ya protons. Hydrogen inayo 1 tu. Inayofuatia ni Helium ina proton mbili, inayofuatia ni Lithium na kuendelea.

Kila unachokiona mfano mti na jiwe vipo na tofauti kwenye atomic particles. Vibration na umeme wa mti na jiwe vinatofautiana na ndio maana unaona ni tofauti. Pia utofauti wake unapelekea utofauti mpaka wa elements. Mfano mti ina Carbon lakini jiwe linaweza kuwa ni Calcium. Kwahiyo utofauti wa kila chenga chenga za ulimwengu ni atomic number. Utofauti wa atomic number umetokana na utofauti wa aina za vibration.

Pia hata Rangi ni vibrations za waves katika hali mbalimbali. As same as sound. They are all energies katika frequency mbalimbali. View attachment 396342

Macho, pua, ubongo, ngozi, sikio na ulimi ni organs ambazo tunazitumia tangu evolution inaanza katika kila kiumbe ili kujua rates za vibration na kutumia ubongo kutafsi kuwa katika forms mbalimbali. Red unayoiona sio red colour ni tafsiri ya ubongo kupitia jicho likasense vibratory frequency na ubongo kutafsiri. Sikio lina sense rate ya vibration kwenye hewa na kukupa frequency kwenye ubongo ukatafsiri.

Hivyo nature ya ulimwengu ni kama mazingaombwe. Imani za Asia zinasema ULIMWENGU HAUPO KAMA UNAVYOUONA. Kutoka katika Element ya kwanza Hydrogen imetengeneza elements zote unazoziona na kila siku nyota zinavyopasuka na kujijenga zinatengeneza elements. Oxygen unayotumia leo hii imetokana na hudrogen iliyokuwa fused na kubadilishwa atoms katika nyota na ndio kazi kuu ya nyota. Kutengeneza elements. Ndio maana wanasayansi wanaamini Hydrogen ndio element ya kwanza kwa sababu imeinda kila element.

Kila kitu ni energy. That energy ndio inayoshikilia ulimwengu na kila particle. Na tunavyotafsiri ulimwengu ulivyo sio kama. Ulivyo bali ni kutokana na mazoea ya kuuelewa ulimwengu tangu tulipozaliwa mpaka sasa.

KWA KUCHUNGUZA NATURE YA ULIMWENGU UTAGUNDUA KUWA MUUMBAJI, CHANZO CHA ULIMWENGU, KILICHOUMBWA, NA KINACHOONA UUMBAJI NI WAMOJA.

Finally at least someone with a scientific base.

Mtu kama wewe hata nikiamua kubishana nawe najua tutaweza kuulizana maswali deep.

Quantum physics is so fascinating, especially its counterintuitive nature.

Mara nyingine huwa napata tabu hata kuanza kuigusia.

Utaanzaje kuongea quantum physics na mtu ambaye haelewi kwamba unaweza kujua 5 si square root ya 2 bila kujua square root ya 2 ni nini, ikiwa unajua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2 na 5 ni kubwa kuliko 2 ?

Umeandika

Na hapo utaona ulimwengu na kila ukionacho ni ILLUSION.

Kisha ukaandika

KWA KUCHUNGUZA NATURE YA ULIMWENGU UTAGUNDUA KUWA MUUMBAJI, CHANZO CHA ULIMWENGU, KILICHOUMBWA, NA KINACHOONA UUMBAJI NI WAMOJA

Unajuaje hili ni kweli na si illusion tu pia? Huoni kwamba kuna contradiction kati ya habari ya kwanza na hii ya pili?

Utajuaje illusion inaishia wapi na reality inaanzia wapi?
 
Uwezo wa kutafakar yapaswa kabisa kuwa energy... na ikawa transformed kutoka hali moja kwenda nyingine...

Wewe kama hujiulizi kwanini kila kitu hapa ulimwenguni kina "purpose"

Dini hizi au imani zina mchango mkubwa katika maendeleo ya sayansi.. na naamini "MUNGU" "الله" huwa anapenda wanaotumia akili..anapenda watu watumie resources alizo ziandaa tayar kwa ajili ya utafiti ili aidha tuutambue ukuu wake au utafiti huo urahisishe hili game la maisha tulilo nalo..

Science ilivyo jimega na kujiondoa kwenye dini sasa imekuwa ni finyu maendeleo yake yanakuja polepole..

Kwa kiwango cha akili tulicho nacho walimwengu ni kikubwa mno hawa scientist waliofikiri mpaka wakagundua kuwa light ndo yenye speed kuliko chochote ulimwengua wametumia kijitheluthi tu cha akili zao.. kazi ipo kwetu ambao hata hio akili tu hatutumii..!
 
Kwa hiyo mtu ambaye hajui square root ya mbili ni nini, lakini anajua kwamba square root ni lazima iwe ndogo zaidi ya hiyo namba inayotafutiwa square root, akiambiwa kwamba square root ya 2 ni 5, hawezi kuona kwamba 5 haiwezi kuwa square root ya 2 kwa sababu 5 ni kubwa kuliko 2?
Hujanielewa bado, nimesema mfano wako ni batili. Unaposema hujui ulimwengu umefanyikaje, ni sawa na kusema hujui square root ni nini na inapatikana, sasa mtu akikuambia square root ya mbili ni kumi, unatumia msingi gani wa kukataa? Kama hujui ulimwengu umefanyikaje, kipi kinajenga msingi wa hoja zako? Unaogopa nini kuwa straight na unachokijua na kukiamini.
 
Hapana.

Unalazimisha.

Twende polepole.

Dhana ya msingi hapa ni kwamba, unaweza kujua jibu fulani ni batili hata kama hujui jibu sahihi ni lipi.

Kwamba huhitaji kukua jibu sahihi ili ujue jibu hili si sahihi.

Hilo unakubali au hukubali?
 
Duh!

Mazee huwa unaandika mambo mengi sana hadi unaishia kujichanganya mwenyewe tu [na pengine unakuwa hujui hata kama umejichanganya].

Sasa kama hujui jibu sahihi ni lipi utajuaje kwamba jibu hili au lile ni batili?
 
Mkuu Apollo, sayansi haipingani na Mungu ila tu kumdhihirisha. Mungu si nguvu tu, bali ni Nguvu na Sheria. Fikiria mti, kabla haujachanwa mbao huwezi sema hizi mbao, ukishachanwa mbao bado haitoshi kusema hili ni kabati, sheria ni vigezo nguvu ni kani ya kutimiza vigezo.
Bahati mbaya sina ujuzi na physics, lakini bado sijawahi ona kujidhihirisha kwake juu ya uumbaji nje na nikijuacho.
 
Hapana.

Unalazimisha.

Twende polepole.

Dhana ya msingi hapa ni kwamba, unaweza kujua jibu fulani ni batili hata kama hujui jibu sahihi ni lipi.

Kwamba huhitaji kukua jibu sahihi ili ujue jibu hili si sahihi.

Hilo unakubali au hukubali?
Ni kweli, ila tu kama unajua jibu sahihi linapatikanaje. Sasa wewe hujui ulimwengu umefanyikaje, unaanzaje kupinga jibu la kuwa kuna aliyeufanya? Mkuu huoni hapo kuwa wewe ndiye unayelazimisha?
 
Duh!

Mazee huwa unaandika mambo mengi sana hadi unaishia kujichanganya mwenyewe tu [na pengine unakuwa hujui hata kama umejichanganya].

Sasa kama hujui jibu sahihi ni lipi utajuaje kwamba jibu hili au lile ni batili?
Swali zuri sana.

Chukua mfano unajua kanuni za msingi za hesabu.

Unajua kuhesabu 1,2,3, 4,5,6 etc, unajua the basics of number theory.

Unajua kanuni za square root, kwamba 5x5 = 25, -5 x -5 = 25, therefore the square root of 25 is -5 or 5.

Unajua square root ya namba "a" haiwezi kuwa kubwa zaidi ya hiyo namba "a".

Sasa mtu akakuambia "square root ya mbili ni 5".

Kwa kweli mtu kuijua square root ya mbili bila kukokotoa si rahisi, maana si namba iliyo kamili. Hata Ramanujan ingempa shida (By the way, have you seen "The Man Who Knew Infinity", the movie?)

Lakini kutokujua hiyo namba ambayo ni square root ya mbili kwa ukamili wake, hakukuzuii kujua kwamba 5 si square root ya mbili.

Kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na 5 ni kubwa kuliko 2, hivyo 5 haiwezi kuwa square root ya 2.

Napenda kutumia hesabu kuonesha wazi mambo.

Kuna watu wanafikiri kwamba usipojua ulimwengu umeanzaje, basi maana yake hata ukiletewa hoja batili kuhusu ulimwengu ulivyoanza (kama vile kuumbwa na Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote) ni lazima uikubali tu, kwa sababu hujui ulimwengu ulianzaje.

Kusema hivyo ni sawa na kumwambia mtu asiyejua square root ya 2 kwamba akubali ni 5 tu, kwa maana hajui jibu.

Mimi huwauliza, mnaweza kuthibitisha na kuonesha kwamba Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu?

Mnaweza kuthibitisha na kuonesha kwamba 5 ni square root ya 2?

Wanaingia mitini wote.
 
Ni kweli, ila tu kama unajua jibu sahihi linapatikanaje. Sasa wewe hujui ulimwengu umefanyikaje, unaanzaje kupinga jibu la kuwa kuna aliyeufanya? Mkuu huoni hapo kuwa wewe ndiye unayelazimisha?
Ni lazima kujua square root ya 2 ni nini au inapatikanaje ili ujue kwamba 5 si square root ya 2?
 
Swali zuri sana.

Chukua mfano unajua kanuni za msingi za hesabu.

Unajua kuhesabu 1,2,3, 4,5,6 etc, unajua the basics of number theory.

Unajua kanuni za square root, kwamba 5x5 = 25, -5 x -5 = 25, therefore the square root of 25 is -5 or 5.

Unajua square root ya namba "a" haiwezi kuwa kubwa zaidi ya hiyo namba "a".

Sasa mtu akakuambia "square root ya mbili ni 5".

Kwa kweli mtu kuijua square root ya mbili bila kukokotoa si rahisi, maana si namba iliyo kamili. Hata Ramanujan ingempa shida (By the way, have you seen "The Man Who Knew Infinity", the movie?)

Lakini kutokujua hiyo namba ambayo ni square root ya mbili kwa ukamili wake, hakukuzuii kujua kwamba 5 si square root ya mbili.

Kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na 5 ni kubwa kuliko 2, hivyo 5 haiwezi kuwa square root ya 2.

Napenda kutumia hesabu kuonesha wazi mambo.

Kuna watu wanafikiri kwamba usipojua ulimwengu umeanzaje, basi maana yake hata ukiletewa hoja batili kuhusu ulimwengu ulivyoanza (kama vile kuumbwa na Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote) ni lazima uikubali tu, kwa sababu hujui ulimwengu ulianzaje.

Kusema hivyo ni sawa na kumwambia mtu asiyejua square root ya 2 kwamba akubali ni 5 tu, kwa maana hajui jibu.

Mimi huwauliza, mnaweza kuthibitisha na kuonesha kwamba Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu?

Mnaweza kuthibitisha na kuonesha kwamba 5 ni square root ya 2?

Wanaingia mitini wote.

Sawa, nakuelewa.

Lakini sidhani pia kwamba unaweza ukadismiss kabisa jibu fulani na kuliita batili ilhali jibu sahihi huna.

Kama jibu sahihi huna mamlaka ya kuliita jibu fulani ni batili unayatoa wapi?

Ni mpaka pale utapopata jibu sahihi ndo unaweza kusema kwamba jibu hili au lile ni batili na sahihi ni hili hapa.

Kwa sababu, hata hilo ambalo unaliona ni batili linaweza kuwa ni sahihi vilevile.

Na ndo maana sisi wengine ikija kwenye hayo mambo ya ulimwengu ulianza anzaje au sijui mambo ya uwepo wa mungu, tunakiri tu kuwa hatujui.

Hatujui kwa sababu yote yanayodaiwa na pande zote mbili [wakana mungu na wakubali mungu] yana mapungufu mengi tu.
 
Mamlaka ya kusema hili ni jibu batili wakati jibu sahihi huna unaweza kuyapata kutokana na principle inayoweza kukuonesha jibu sahihi linatakiwa liwe vipi, bila ya kulijua hilo jibu kamili lenyewe.

Kwa mfano, mtu anaweza kuniambia mji wa Los Angeles uko Marekani. Halafu akaniambia mji huo uko katika state ya Tabora huko Marekani, Wilaya ya Igunga. Hata kama sijui mji wa Los Angeles uko state gani, nitajua kwamba haupo katika state ya Tabora, kwa sababu nazijua states zote 50 za Marekani, Tabora si state ya Marekani.

Hivyo basi, bila hata kujua mji wa Los Angeles uko state gani, hili jibu la state ya Tabora nitajua ni batili.

Vivyo hivyo mtu akiniambia square root ya 2 ni 5, sihitaji hata kujua square root ya 2 ni nini, kwa sababu najua tu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.

Hii logic huwa inasaidia sana katika elimination method, hasa kwenye multiple choice questions.

Ukiweza kuielewa hii logic, kwenye habari kama mitihani ya multiple choice na IQ tests itakusaidia sana.

Utakuta mtu kapewa majibu A, B, C, D wakati clearly mawili yapo out of range, yeye anataka kuhakiki yote, anatumia muda mara mbili zaidi.

Wanaodai Mungu yupo, hususan huyu Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wameshindwa kuondoa contradictions za huyo Mungu.

Mungu huyo ni wa hadithi zaidi mpaka hapo watakapoweza kuondoa contradictions hizo.

Huwezi kuniambia Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu huu wenye vita, njaa, magonjwa, tsunami, matetemeko ya ardhi etc that is an inherent contradiction that needs resolving.

Nobody has resolved this.

If one believes this, one must believe that there is a triangular circle in Euclidean geometry.

It carries the same contradiction.
 
Sasa hapo umetumia mfano ulio rahisi sana kupata uthibitisho wake. Ni mfano mzuri lakini sidhani kama unawakilisha vizuri ubishi/utata wa uwepo wa mungu.

Kuyajua majimbo yote ya Marekani na kuthibitisha kama Tabora ni mojawapo ya majimbo ya huko ni kazi rahisi mno na isiyo na utata wowote ule.

Kwa suala la mungu na uwepo wake ni habari nyingine kabisa. Ulimwengu ni mkubwa mno. Sidhani kama kuna binadamu anayejua kila kitu kilichopo ndani yake.

Sidhani kama inawezekana kwa binadamu yeyote yule ku scour kila pembe na kona ya ulimwengu na kujua vyote vilivyopo.

Kwa hiyo, nakubali kwamba unaweza kuitumia hiyo kanuni katika kuengua mambo fulani fulani lakini sidhani kama unaweza kuitumia kwenye kila kitu na kupata majibu sahihi.

Kuna mambo majibu yake hupatikana kirahisi na mengine si kiurahisi na huenda mengine hayana majibu kabisa.

Hilo ni kweli. Kwamba, wanaodai uwepo wa mungu hawajatoa uthibitisho wa kuridhisha na kuhitimisha kuwa kweli yupo. Mapungufu ya majibu yao hata mimi nayaona na wala si vigumu kuyaona.

Na kwa kweli huhitaji hata akili kubwa kubaini kuwa kuna walakini.

Lakini kwa upande mwingine pia, inawezekana hata wao wamepotoka kupita maelezo. Kwamba, kile wanachokiamini [kikubali] sicho bali kipo kingine ambacho hawakijui.

Kwa hiyo nakubali kwamba unaweza kuukataa ushahidi wanaoutoa, lakini hiyo haimaanishi kwamba wanachokisema hakipo. Inawezekana kipo lakini wao hawajajua namna ya kuupata uthibitisho wake.

Na pia inawezekana kipo lakini pengine hakina sifa ambazo wanadhani kinacho.

Kwa mtaji huo ngoja tu niendelee kuwa open minded na kusubiri kuupata huo ukweli.

Agnostics oyeeeeeeeee
 
Sasa hapo umetumia mfano ulio rahisi sana kupata uthibitisho wake. Ni mfano mzuri lakini sidhani kama unawakilisha vizuri ubishi/utata wa uwepo wa mungu.

Kuyajua majimbo yote ya Marekani na kuthibitisha kama Tabora ni mojawapo ya majimbo ya huko ni kazi rahisi mno na isiyo na utata wowote ule.

Kwa suala la mungu na uwepo wake ni habari nyingine kabisa. Ulimwengu ni mkubwa mno. Sidhani kama kuna binadamu anayejua kila kitu kilichopo ndani yake.

Sidhani kama inawezekana kwa binadamu yeyote yule ku scour kila pembe na kona ya ulimwengu na kujua vyote vilivyopo.

Kwa hiyo, nakubali kwamba unaweza kuitumia hiyo kanuni katika kuengua mambo fulani fulani lakini sidhani kama unaweza kuitumia kwenye kila kitu na kupata majibu sahihi.

Kuna mambo majibu yake hupatikana kirahisi na mengine si kiurahisi na huenda mengine hayana majibu kabisa.

Hilo ni kweli. Kwamba, wanaodai uwepo wa mungu hawajatoa uthibitisho wa kuridhisha na kuhitimisha kuwa kweli yupo. Mapungufu ya majibu yao hata mimi nayaona na wala si vigumu kuyaona.

Na kwa kweli huhitaji hata akili kubwa kubaini kuwa kuna walakini.

Lakini kwa upande mwingine pia, inawezekana hata wamepotoka kupita maelezo. Kwamba, kile wanachokiamini [kikubali] sicho bali kipo kingine ambacho hawakijui.

Kwa hiyo nakubali kwamba unaweza kuukataa ushahidi wanaoutoa, lakini hiyo haimaanishi kwamba wanachokisema hakipo. Inawezekana kipo lakini wao hawajajua namna ya kuupata uthibitisho wake.

Na pia inawezekana kipo lakini pengine hakina sifa ambazo wanadhani kinacho.

Kwa mtaji huo ngoja tu niendelee kuwa open minded na kusubiri kuupata huo ukweli.

Agnostics oyeeeeeeeee
Kwa mtaji huo huwezi kuamka kutika kitandani siku yoyote ile.

Utakapotaka kuutoa mguu kitandani ukanyage sakafu utakumbwa na maswali alfu moja na moja. Itabidi ubpostpone judgement. Wakati hakuna 100% certainty. Not if Heisenberg stands.

Utajiuliza, sakafu inaweza kuhimili uzito wangu? Vipi ikipasuka nikianguka na kufa?

Vipi ikipasuka, nikadondoka, halafu Superman akaja kunidaka, halafu wakati ananidaka mkono wake ukatoboa tumbo langu nikafa?

Vipi ikipasuka, nikadondoka, halafu Superman akaja kunidaka, halafu wakati ananidaka, mkono wake usitoboe tumbi langu lakini anichanje kwa pete yake yenye sumu?

Vipi ikipasuka, nikadondoka, halafu Superman akaja kunidaka, halafu wakati ananidaka, dari ikapasuka na kryptonite ikamuingia machoni na yeye akafa pale pale?

Vipi kama mtu anachimba kutoka uoande wa piki wa dunia halafu drill lake la moto linakuja kutokea hapo nitakapokanyaga?

You gotta be suicidal just to wake up in that world.

At some point one has to use logic and weed out the logical fallacies and contradictions, and choose a practical framework to work with.

Ndiyo maana mimi sikatai imani. Naam, zaidi ya hapo nasema hakuna mtu anayeweza kuishi bila imani.

Ukishapanga ya kesho tu ushapanga kwa imani kwamba kesho itakuwepo.

Inawezekana isiwepo.

Nakataa imani mbovu.
 
Mpo salama waungwana?

Swali hili ningependa haswa kulipeleka katika pande mbili (2) kwenye sayansi na wanaoamini uwepo wa Mungu.

Katika sayansi ningependa kuhoji hivi je, ni kivipi nguvu inaweza kutengeneza/kutokeza object?

Katika upande wa Waumini wa Mungu naomba kuhoji hivi
kama ilivyoandika na vitabu vyake kwamba kwa kutumia uweza wake ama nguvu zake Mungu aliumba kila kitu. Swali hapa ni je, ni kivipi nguvu hiyo ya Mungu iliweza kuumba/kutokeza/kuunda objects kama dunia,nyota n.k?

Ni hivyo tu wakuu mnakaribishwa.
Uliza kwa kiingereza kiswahili kina utata kidogo[emoji120][emoji120]
 
Kwa mtaji huo huwezi kuamka kutika kitandani siku yoyote ile.

Utakapotaka kuutoa mguu kitandani ukanyage sakafu utakumbwa na maswali alfu moja na moja.

Sakafu inaweza kuhimili uzito wangu? Vipi ikipasuka nikianguka na kufa?

Vipi ikipasuka, nikadondoka, halafu Superman akaja kunidaka, halafu wakati ananidaka mkono wake ukatoboa tumbo langu nikafa?

Vipi ikipasuka, nikadondoka, halafu Superman akaja kunidaka, halafu wakati ananidaka, mkono wake usitoboe tumbi langu lakini anichanje kwa pete yake yenye sumu?

Vipi ikipasuka, nikadondoka, halafu Superman akaja kunidaka, halafu wakati ananidaka, dari ikapasuka na kryptonite ikamuingia machoni na yeye akafa pale pale?

Vipi kama mtu anachimba kutoka uoande wa piki wa dunia halafu drill lake la moto linakuja kutokea hapo nitakapokanyaga?

At some point one has to use logic and weed out the logical fallacies contradictions.

Hahahaaa mazee bana. Sometimes you take things to extremes.

Hapana, haiko hivyo hata kidogo maana ingekuwa hivyo nisingekuwa naishi.

You can't live in fear of the unknown. What kinda life would that be?

Maisha yana rangi mbalimbali, si nyeusi na nyeupe tu.

Kuna kijivu, hudhurungi, waridi, na kadhalika.
 
Unaposema Nguvu kwanza unamaanisha nini mkuu?

Pia naomba nikupe mwanga wa tafiti zinavyosema kuhusiana na hali ya kila kitu unachokiona.

Kwanza kabisa nature ya ilimwengu haipo kama wengi wanavyoelewa. Kila unachokiona hakipo kama kilivyo. Wengi waliobahatika kusoma na kufahamu mengi hii sio concept mpya kwao.

Kila kitu unachokiona (matter) vimeundwa au kujengwa na Atoms. Ukiweza kuchukua kitu na kutumia darubini kali saana 10,000 times utaona Atoms. Mfano kama size ya dunia ndio matter atom zake zinaweza kuwa size ya mpira wa Golf ukisema uangalie mfano kwa ration utakayoielewa. Katika uchunguzi wa atom kuna mambo mengi ambayo mpaka sasa Quantum Physics inajaribu kufahamu zaidi kwa sababu Atoms zipo zina tabia tofauti na Matter. Atoms zimejengwa na Electrons ambazo zinazunguka kiini chake kinachoitea Nicleus. Ndani ya kiini kuna proton na neutron.

View attachment 396335

Ni kama vile sayari zinavyozunguka jua katika njia yake. Lakini tofauti ya mzunguko wa sayari na jua na mzunguko wa electrons ni kwamba kwenye atom electron zinaweza kuhama njia yake lakini hazibadiliki idadi. Quantum Physics inasema kuwa Ukichukua kila kitu duniani ukachukua atoms zake particle hazijai size ya kiwanja cha mpira cha standard. Na hapo utaona ulimwengu na kila ukionacho ni ILLUSION.

Kiini cha atom ni umeme kuna positive na negative charge. Kama atom ina electron +3 lazima iwe na proton -3 kuweka balance.

Kila kitu kimeindwa na element mbalimbali. Kuna oxygen, hydrogen, helium, carbon na kadhalika. Kila element ina atom na kila atom ina umeme. Tofauti kati ya kitu kimoja na kingine ni mpangilio wa atoms, umeme wa atoms katika vibration yake na idadi ya protons.

Mfano Hydrogen ina atomic number 1 (nadhani mmesoma periodic table). View attachment 396339

Tofauti kati ya hudrogen na element zote ulimwenguni ni idadi ya protons. Hydrogen inayo 1 tu. Inayofuatia ni Helium ina proton mbili, inayofuatia ni Lithium na kuendelea.

Kila unachokiona mfano mti na jiwe vipo na tofauti kwenye atomic particles. Vibration na umeme wa mti na jiwe vinatofautiana na ndio maana unaona ni tofauti. Pia utofauti wake unapelekea utofauti mpaka wa elements. Mfano mti ina Carbon lakini jiwe linaweza kuwa ni Calcium. Kwahiyo utofauti wa kila chenga chenga za ulimwengu ni atomic number. Utofauti wa atomic number umetokana na utofauti wa aina za vibration.

Pia hata Rangi ni vibrations za waves katika hali mbalimbali. As same as sound. They are all energies katika frequency mbalimbali. View attachment 396342

Macho, pua, ubongo, ngozi, sikio na ulimi ni organs ambazo tunazitumia tangu evolution inaanza katika kila kiumbe ili kujua rates za vibration na kutumia ubongo kutafsi kuwa katika forms mbalimbali. Red unayoiona sio red colour ni tafsiri ya ubongo kupitia jicho likasense vibratory frequency na ubongo kutafsiri. Sikio lina sense rate ya vibration kwenye hewa na kukupa frequency kwenye ubongo ukatafsiri.

Hivyo nature ya ulimwengu ni kama mazingaombwe. Imani za Asia zinasema ULIMWENGU HAUPO KAMA UNAVYOUONA. Kutoka katika Element ya kwanza Hydrogen imetengeneza elements zote unazoziona na kila siku nyota zinavyopasuka na kujijenga zinatengeneza elements. Oxygen unayotumia leo hii imetokana na hudrogen iliyokuwa fused na kubadilishwa atoms katika nyota na ndio kazi kuu ya nyota. Kutengeneza elements. Ndio maana wanasayansi wanaamini Hydrogen ndio element ya kwanza kwa sababu imeinda kila element.

Kila kitu ni energy. That energy ndio inayoshikilia ulimwengu na kila particle. Na tunavyotafsiri ulimwengu ulivyo sio kama. Ulivyo bali ni kutokana na mazoea ya kuuelewa ulimwengu tangu tulipozaliwa mpaka sasa.

KWA KUCHUNGUZA NATURE YA ULIMWENGU UTAGUNDUA KUWA MUUMBAJI, CHANZO CHA ULIMWENGU, KILICHOUMBWA, NA KINACHOONA UUMBAJI NI WAMOJA.

Ilihali nakubaliana na wewe katika baadhi Ya mambo unayosema kuna Mengine sikubaliani nawe

1. Sayansi na Ulimwengu si mazingaombwe ...kila kitu kipo mathematically arranged.Hakuna ajali, ndio maana leo unaweza kuelezea ulimwengu na matter kama ulivyoeleza hapo juu...suala la mazingaombwe linakuja tu pale tunaposhindwa kueleza jambo kwa wakati huo. imagine kumuelezea mtu hayo uliyosema hapo juu miaka 200 iliyopita!.

2. Kama kila kitu ni "nguvu" moja Ya muumbaji, nini basi kilileta "nguvu" Ya uhai?...kwa nini nguvu hii haiwezi kuhamishwa kwa maada zisizohai? Ilhali mifumo mingine Ya nguvu inawezekana? Mfano joto, n.k
 
Hahahaaa mazee bana. Sometimes you take things to extremes.

Hapana, haiko hivyo hata kidogo maana ingekuwa hivyo nisingekuwa naishi.

You can't live in fear of the unknown. What kinda life would that be?

Maisha yana rangi mbalimbali, si nyeusi na nyeupe tu.

Kuna kijivu, hudhurungi, waridi, na kadhalika.
Wewe umechagua kijivu kama Fifty Shades of Grey zote. Maana nyeupe hutaki, nyeusi hutaki. 🙂
 
Ni lazima kujua square root ya 2 ni nini au inapatikanaje ili ujue kwamba 5 si square root ya 2?
Je, unaweza ukawa hujui square root ni nini na ukawa unajua 5 haiwezi kuwa square root ya mbili?
 
Ndiyo.

Unaweza ukawa hujui square root ni nini.

Unaweza kuambiwa tu "square root ya namba ni lazima iwe ndogo zaidi ya hiyo namba". Usijue chochote kingine kuhusu square root.

Ukaambiwa 5 ni square root ya 2.

Ukasema kwa kufuata kanuni ya "square root ya namba ni lazima iwe ndogo zaidi ya hiyo namba" ukajua kwamba 5 haiwezi kuwa square root ya 2.

Hujui square root ni nini. Hujui square root ya 2 ni nini. Lakini unajua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.

Hilo tu linatosha kukujuza kwamba 5 si square root ya 2.
 
Back
Top Bottom