Hoja ya square root imekufa vipi?
Hojailikuwa kwamba, huhitaji kujua jibu halisi ili kujua kwamba jibu Fulani ni batili.
Nikatoa mfano mtu hajui square root ni nini, hajui square root ya mbili ni nini, lakini kaambiwa na mwalimu wake square root ni lazima iwe ndogo kuliko hiyo namba inayotafutiwa square root.
Huyu mtu si mdadisi, anasikia anachoambiwa na kukikubali tu, anaheshimu authority ya mwalimu wake.
Kwa hiyo hajui square root ni nini, hajui square root ya mbili ni nini. Lakini anajua kwamba square root ya namba yoyote ni lazima iwe ndogo kuliko namba yenyewe.
Ukimwambia mtu huyu square root ya 2 ni 5 atakwambia haiwezi kuwa hivyo, kwa sababu square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa kuliko 2.
Bila hata kujua square root ni nini na square root ya mbili ni nini.
Hahitaji kujua jibu sahihi ili kujua kwamba jibu fulani ni batili.
Kwa nini unasema hoja yangu ya kwamba unaweza kujua jibu fulani ni batili hata kama hujui jibu sahihi imekufa?