VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kila uchao, viongozi wanapishana hadi kugongana kwenye kuwahi 'kuuchambua' na 'kuupambanua' mkataba wa ukodishwaji wa Bandari kati ya Tanzania na Emirati kupitia DP World. Mkataba ulishasainiwa na kuidhinishwa na Bunge. Umebaki utekelezaji tu. Lakini, kelele za wananchi juu ya mkataba huo haziishi.
Viongozi, wakiongozwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, wamekuwa wakipambania 'kueleweka' juu ya mkataba huo. Wanapojibanza ni faida tutakazozipata kama taifa. Hawagusi kabisa hatari na hasara za kimkataba tutakazozipata kama taifa.
Wanaelezwa viongozi wa dini; wanafafanuliwa watu wa chini; wanaandikiwa watu wa mtandaoni; wanaambiwa watu wa redioni; wanaoneshwa watu runingani lakini mambo bado ni magumu. Kila mtanzania anayejaribu kuuchambua mkataba huo (kupitia inayoitwa nakala ya mtandaoni), hakubaliani na mkataba huo.
Viongozi wa chama na Serikali wanaeleza lakini ni kama wanabezwa; wanasema kwa kuhema lakini ho0ja zao hazisikiki ipasavyo. Wanaonekana 'wamekatiwa' kitu kidogo. Wananchi na viongozi hadi wa dini hawatosheki na maelezo juu ya mkataba huo. Lakini, nguvu kubwa inatumika kuuelezea bila mafanikio.
Tunajua kuwa mkataba mtautekeleza. Tunajua kuwa mkataba ulishaanza kazi yake. Tunajua kuwa hata mikataba itakayozaliwa na huu wa sasa itakuwa na ukakasi halisi na mikali kama fisi. Tunajua kuwa maoni yetu hayatafua dafu kwenu wakuu wetu. Lakini, amini nawaambia, watanzania wameshasajili jambo hili mioyoni mwao.
Hakika, nguvu kubwa inayotumika kuuelezea mkataba huu wa DP World (ulioibuliwa bila idhini ya Serikali na baadaye kufanywa kama public document) ni kilelezo na ushahidi tosha kuwa mkataba huu una walakini mkubwa.
Sauti iliayo nyikani!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Chato, Geita)