Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Watu wengi hawafuatilii takwimu na hawa ndio wanapiga kelele kuwa Tanzania sii nchi maskini inayohitaji misaada na mikopo. Je unajua kati ya watanzania Milion 65, ni watanzania milion 25.7 pekee ndio wenye uwezo wa kufanya kazi ya kujiingizia kipato? Nikiwa na maana hao wengine wanaobaki hawawezi kutumika kama nguvu kazi. Kwenye hiyo milion 25 toa hapo vijana wavivu na wale wasio na kazi maalumu(job less) pia toa hapo baadhi ya wanawake wanaoamini kufanya kazi sio jukumu lao (ukizingatia wanawake wametuzidi kidogo kwa idadi)
Katika hiyo nguvu kazi ya milion 25, ni watanzania milioni 4 pekee waliosajiliwa kama walipa kodi wa moja kwa moja.
Kwa ufupi Tanzania tunahitaji nguvu ya ziada kuondoka katika utegemezi
Katika hiyo nguvu kazi ya milion 25, ni watanzania milioni 4 pekee waliosajiliwa kama walipa kodi wa moja kwa moja.
Kwa ufupi Tanzania tunahitaji nguvu ya ziada kuondoka katika utegemezi