Nguvu tunayotumia "kushadadia" Vita visivyotuhusu tungeitumia kukemea maasi kwenye Taifa letu

Nguvu tunayotumia "kushadadia" Vita visivyotuhusu tungeitumia kukemea maasi kwenye Taifa letu

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Salam,
Nimekua najiuliza mara nyingi sana kuwa hizi nguvu zinazotumika kushabikia vita au maasi kwenye nchi ambazo wala hazituhusu, si tungezitumia hapa kwetu kukemea maovu? Mfano ni haya yafuatayo
1. Ndani ya kipindi kisichozidi siku 10 yaani kati ya November 25 - December 2 Polisi wetu,wanaolipwa kwa kodi zetu, wameua RAIA wawili wasio na hatia, Mlinzi wa Boardroom Sinza na Mama muuza Mboga huko Iringa, hakuna official statement imetolewa, hakuna chochote it is like walioliwa ni mbwa. ila tuko busy na waarabu/waisrael.
2. kuna wimbi kubwa la vijana wa kihuni kufanya vurugu, wamejeruhi, wameua, wamepora na huwezi kusikia kuna mtu anakemea hili, wote kimya, Vijana hawa kwa sasa wanazidi kuongezeka na mbaya zaidi vyombo vya habari viko kimya au pengine mamlaka husika hazitaki kutoa taarifa, makundi haya kwa sasa yapo Dar, Moro, Katavi (wamepora na kuua) na Arusha. wanaoporwa, kujeruhiwa na kuumizwa ni ndugu zetu.

3. wakati tunaumizwa na haya, anajitokeza Waziri anayejiita Profesa ambaye amekula amevimbiwa anasema VINGOZI wa Tanzania wanabana Matumizi kwa kununua magari ya 2023 ya million 500.

Nilitaka kuendelea kuandika, narudi kwanza........
 
Kuna watu wanaamini Israeli ni bora kuliko hata kwao walipotoka babu na bibi yake.
Kuna watu wanaamini waarabu ni bora kuliko ndugu zao weusi na Africa yao.

Hapa ndio kuna wapa watu upofu na ndio hawa waarabu na waisraeli walipotublackmail.

Kama wewe ni muumini wa dini za ukristo na uislamu baki kwenye mafundisho yanayosisitiza utu, kupendana na kuamini katika Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ma sio kuamini eti jamii hizo ni bora kuliko ndugu zako wamakonde wenzio.
 
Ukiwa ni mtu wa kupinga na kutokufurahia injustices (keyword ni kupinga na kutokufurahia sio kushabikia) basi utazipinga no matter zimetokea wapi; ukipinga za kule does not mean upingaji utakwisha hivyo kukosa nguvu za kupinga hapa....
 
Uncle focus yetu ni 2025 panga pangua za maana..... figisu za kutosha...mkituchagua tena nakuhakikishia panya road tunawapeleka kwenye scheme mbali mbali zilizopo nchini
 
Kuna watu wanaamini Israeli ni bora kuliko hata kwao walipotoka babu na bibi yake.
Kuna watu wanaamini waarabu ni bora kuliko ndugu zao weusi na Africa yao.

Hapa ndio kuna wapa watu upofu na ndio hawa waarabu na waisraeli walipotublackmail.

Kama wewe ni muumini wa dini za ukristo na uislamu baki kwenye mafundisho yanayosisitiza utu, kupendana na kuamini katika Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ma sio kuamini eti jamii hizo ni bora kuliko ndugu zako wamakonde wenzio.
Hakika kabisa
 
Back
Top Bottom