Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

Brother salute kwako.

Kuna kijiswali kidogo hapa .ulienda kituoni na furana ya navy ulipofika kituoni ukavaa sweta la polisi jambo ambalo raia wa kawaida hawezi thubutu,
Kwanini hukufikiria kunyag'anywa na kuachwa kifua wazi pamoja na kupigishwa kwata bila kupenda
Ile fulana na Navy nilienda nayo kwa bahati mbaya. Nilipofika pale ndio nikagundua kwamba nilivyo vaa its inappropriate kwa mahala nilipo.
Uzuri yule askari niliyemkuta getini namfahamu.
 
Short, sweet and powerful.

Hua nakubali sana nguvu ya kalamu yako chief. Lkn niwe tu muwazi, hii kitu umekosea sana kutupa vipande kama movie za Kinaijeria. I am really waiting for part 2, 3, 4 and 5. Thanks again for sharing ur talent with us. Stay blessed!!
Pamoja sana chief...

Nitajitahidi kudondosha 'episodes' mfululizo ili uhondo usikatike.

Salute!
 
The bold,
Shukrani kwa makala zako za simulizi za kipekee ktk lugha ya Kiswahili zinazoelezea matukio muhimu ulimwenguni kama hili la "Black Wednesday".

Maana Jamiiforums inabidi liwe jukwaa linalotoa mwanga kuelewa matukio makubwa kama haya na kuelimisha pia kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
Well said chief...
Pamoja sana!
 
The bold
Vizuri kaka.
Ingawa mi si muumini wa biashara za aina hii, lakini nitafurahi sana kama utakuwa muwazi kuelezea hii biashara.
Nasema hivi kwasababu kuna mtu ananilalamikia kwamba anajuta kuijua biashara hii, alikopa mkopo benk kwaajili ya kumalizia nyumba yake lkn alipo ona thread ya Ndugu Ontario ikabidi ajiunge kusaka mahela mengi.
Lkn lilichotokea ni kulalamika kila saa kuwa pesa zake zimepotea huko.

Nilichogundua kwa jamaa ni kutojua undani wa biashara hii, alifanya biashara ambayo haijui,.

Hivyo nitapenda sana mnapo washawishi watu humu waelezeni ukweli, nje ndani ili kuendelea kuaminika kwenu.

Nashukuru kwa makala hii, mimi ni msomaji mzuri wa makala zako
 
Is this a well choreographed 'movie' ?
Cc The bold
Hahah! Nah... haya ninayoandika na yale nitakayoandika ni maoni yangu 100% na nataka niandike maoni yangu binafsi kwa 100% ili kulinda credibility yangu.

Kama nilivyoeleza haya matukio ni halisi kabisa... nadhani baadhi ya wanafunzi wa kwanza kabisa kusoma pale kwa Onatario wanaweza kutoa ushuhuda namna ambavyo walivamiwa na mitutu ya bunduki na ofisi nzima kuwekwa chini ya ulinzi.

Labda tu kitu ambacho wengi watakuwa hawajui ni role ambayo nilihusika behind the scenes.

Hata nilivyofika pale Oysterbay Police kulikuwa na wasaidizi wa ofisi wa Ontario kama wanne hivi lakini sidhani hata kama walinitambua mimi ni nani.

Nimeanza na kisa hiki na baadae kuoanisha na tukio la George Soros kwa sababu huko mbeleni kuna kitu nitakuja kukiongelea kuhusu hii biashara hapa Tanzania na kitu ambacho hata wanaoifanya naamini hawakijui.
Sitaki kwenda direct, nimeanzia huko mbali ili kujenga msingi mzuri tuelewane na nisionekane kwamba namuaharibia Ontario. Nitaandika ule ukweli ambao nimeujua binafsi baada ya upekenyuzi wangu.


Stay tuned chief...
 
Back
Top Bottom