Kwa upande wangu, Mr Kenzy kutokukata tamaa kumekuwa msingi wa mafanikio yangu. Nilipokuwa mdogo, niliishi katika mazingira yenye changamoto nyingi, lakini nilijifunza kwamba kila changamoto ni fursa ya kujifunza na kukua. Licha ya kukosa rasilimali nyingi, niliendelea kusoma kwa bidii na kufanya kazi za vibarua ili kujimudu na kufikia ndoto zangu.
Nikiwa chuo kikuu, nilikumbana na changamoto nyingi za kifedha, lakini sikukata tamaa. Nilitafuta msaada na fursa za kujifunza zaidi. Baada ya kuhitimu, nilianzisha Kampuni ambayo inafanya masuala ya Kilimo , lengo ni ili kusaidia wakulima vijana kama mimi kuboresha kilimo na maisha yao. Kwa kupitia Kampuni hii sasa tumefanikiwa kusaidia wakulima wengi kuongeza mavuno na kipato chao, na hivyo kuboresha maisha ya familia nyingi.
Kwa hiyo, kwa maoni yangu, kutokukata tamaa ni nguzo muhimu sana katika safari ya mafanikio. Ni nguvu inayotusaidia kusimama imara wakati wa changamoto na kuendelea kusonga mbele hadi tufikie malengo yetu.
Ningependa kusikia maoni yenu na uzoefu wenu pia kuhusu jambo hili.