Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Mkuu umenena mazito na makubwa na siku zote chizi naye huwasema wenye akili zao njema eti nao hawana akili, sio ajabu mkuu, mambo haya yapo Tu

Vigeugeu Wapo na hawataisha
Hakika mkuu
 
naona umeandika mashahiri haha.
its simple nilicho hoji ni logic not ushabiki. and because sina interest na upande wowote ule. just a concerned citizen
Hata mm sina Chama chochote ila nazungumza ukwl mtupu.
 
Ningeenda lakini nina majukumu mengine sehem nyingine lakini nayo yanahusu msiba huohuo,, kwahiyo naamini nitapata nafasi ya kuwepo, usijali ndugu yangu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Judas Iscariot muda huo huna.

Usaliti wako umeshatimia basi ndy furaha kwako..

a traitor is always a traitor
 
Naam huo ndo ukweli japo umeeleza kwa ufupi muelewa kaelewa,
 
Yetu macho, kama hii leo tu tunaanza kuona wizi wa makontena bandarini!! Hii inaashilia nini
 
Unajua wala rushwa,wakwepaji kodi,n.k walikuwepo na watakuwepo.sababu kuu ya baadhi yetu kuamini kuwa wakati wa utawala wa hayati JPM vitu hivi havikuwepo ni kuwa vyama vya upinzani vilibanwa sana,(opposition parties),pili hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari.
 
Lakini hatujaona ule Uonevu mkubwa kama kipindi cha nyuma
 
Mapema mnoo.. Acheni uchuro..
 
Watu waliovunja mageti uwanja wa ndege JNA ndio watakaolia mara nyingine ikiwa yataachwa mambo yajiendee

..baada ya wapinzani kushughulikiwa na kuzimwa kabisa, kundi lililokuwa linafuata kushughulikiwa ni wananchi wa aina ya hao waliovunja mageti uwanja wa ndege.

..iko siku waTz waliovunja mageti uwanja wa ndege watachoka kuishi kwa matumaini na ahadi hewa za maisha bora. wataanza kuwazonga watawala na matatizo yataanzia hapo.
 
Wachovu mna wasiwasi kweli, muda wote mmepewa bado mnalalamika hii ndio shida ya kuendekeza watu wanaojiita wanyonge. Na mihela mlikuwa mnajichotea hakuna hata auditing wala bunge kuhoji lakini bado mnalalamika tu. Ndege zinanunuliwa kama mananasi tu , hakuna budget inajadiliwa zaidi ya kusema ndiooooo, na bado mnalalamika tu mwenzenu baar shit alijisemea katika watu wanaokula raha ni yeye sasa nyie wanyonge wengine mlikuwa wapi kula raha au mmesahau raha mlizopata labda niwakumbushe;
1. Mlifurahia sana watumishi kufukuzwa kazi kama mbwa.

2. Mlifurahia kuweka biashara kila sehemu hata mabarabarani bila utaratibu hata kukodi frame za biashara as long una kitambulisho mkaua biashara za wenye frame na walipakodi.

3. Mlishangilia sana manunuzi yasiyofuata utaratibu na kushangilia watu wazima wanapotukanwa hovyo kwa jambo hata dogo tu.

Sasa ni wakati wa waliolia nao kucheka, mbona wenzenu walikaa kimya na mkawa mnashangilia wakakaa kimya ni nini nyie mnapiga kelele nanyi mtulie sasa sindano ziwaingie . Maneno.liyoyatumia yanawarudi Mungu sio Athumani.
 
Hao wanyonge siku zote, miaka yote 6 wameshindwa kujiondoa unyonge baada ya kupata mtetezi ???
Wanasema alifanya mengi zaidi kushinda miaka yote ya wenzake sasa hawa wanyonge si watakuwa ndio matajiri maana alisema wanyonge wataishi kama malaika na matajiri wataishi kama mashetani. Tulishukudia matajiri wakiumizwa sana na tukakaa kimya he hawa wanyonge bado wanalalamikia tu? Tulishasema huwezi kunyanyua uchumi kwa kuwaendekeza wanaojiita wanyonge, wengi wao ni watu wavivu,, wanaopenda majungu na wanafiki wasiopenda kujishughulisha muda wote wao ninwalalamishi tu. Yani ulikosa barabara unalalamika badala ya kujichanga mjenge. Hizi ndio akili za wanyonge naona watupishe sasa tunataka kwenda kadi maana tumerudi nyuma miaka 30
 
Unataka kusema kutesa kwa zamu

Ova
 
Mkuu, walivunja si Kwa sabb nyingine, ni kumsindikiza kipenzi chao hadi kwenye ndege ilipokuwa imesimama
 
Unataka kusema kutesa kwa zamu

Ova
Ndio maana yake mkuu, wimbo waliouimba wa mitano tena sasa tunataka kumi kabisa tuone wanaitikia kibwagizo au tunawaacha mitaa ya kolomoje😃
 
Mkuu, walivunja si Kwa sabb nyingine, ni kumsindikiza kipenzi chao hadi kwenye ndege ilipokuwa imesimama

..Ni kipenzi chao kwasababu aliwapa MATUMAINI fulani.

..sasa wale ni watu wa kipato cha chini ktk nchi yetu.

..na ukichunguza serikali haina mpango wowote wa maana wa kuwainua wasogee ktk kipato cha kati, au juu.

..na kila miaka inavyozidi kwenda kundi hilo linazidi kuongezeka haswa maeneo ya mijini.

..hali hii isiporekebishwa tutajikuta tuna tatizo kubwa sana la kiuchumi, kijamii, na kisiasa, hapa Tanzania.

NB:

..Nimeliona kundi hilo likiongezeka toka utawala wa Raisi Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, na sasa Samia Suluhu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…