Nguvu ya mtandaoni ya #NRNE ni ya Soda tujikumbushe vilivyotamba na kubuma bila mafanikio

Kwani hawa wa mitandaoni si ndio wapo uraiani? Wakihamasishana hakuna kupiga kura hiyo siku ya uchaguzi utasema Kuna uchaguzi hapo?
 
Mbona wewe haujatekwa wala kuuwawa mpaka muda huu , unaweza kunipa sababu ?

Hii ichi ina Watanzania wangapi na waliotekwa wanavuka hata asilimia 0.5 ya Watanzania wote?
Usiangalie idadi ya waliohai mtu mwenye utu na maadili lazima uone hasara kumpoteza ata mmoja kwa sababu zinazoweza kuzuilika
 
Chukulia mzaha.Nguvu ya Hili Jambo Utaona October Kama Kuna Raia Wenye Akili Timamu Wataenda Kupiga Kura.
Katika Mwaka Ambao Uchaguzi Utadorora Kama Ukifanyika Ni Huu Mwaka.
Tunza Uzi Wako Vizuri.
 
hivi idadi kuwa ya hizo NRNE mtandaoni inazuiaje process inayoendelea ya uchaguzi?, vyama 18 wanaenda kupambana na CCM, ni mechanism gani hiyo NRNE itasimamisha/zuia uchaguzi October 2025??
 
No reform No Election
 

Attachments

  • 20250609_000141.jpg
    49.2 KB · Views: 20
Wakati wa kampeni ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Mrema alipendwa zaidi ya anavyopendwa Lissu muda huu, Mwalimu Nyerere akawaambia watu muacheni Mrema abebwe juu juu wala msitishwe na kampeni zao.

Uchaguzi ulipokuja RIP Mrema akaangukia pua.
 
Chukulia mzaha.Nguvu ya Hili Jambo Utaona October Kama Kuna Raia Wenye Akili Timamu Wataenda Kupiga Kura.
Katika Mwaka Ambao Uchaguzi Utadorora Kama Ukifanyika Ni Huu Mwaka.
Tunza Uzi Wako Vizuri.
turn up yoyote ile itaiweka serikali madarakani, huku vijijini ndyo kwenye kura nyingi za CCM na upinzani mko mijini zaidi, huku bush NRNE haina effect yoyote ile, hata uwepo wa vyama vya upinzani ni negligible
 
Hiyo mifano uliyo itoa naiona ni illogical tu,, je hicho kipindi yalitokea kama haya yanayo endelea hivi sasa???

Kipi kinaku aminisha kuwa wananchi hatuwezi kufanya kitu katika harakati za kudai mabadiliko mwaka huu?
 
Kwani hawa wa mitandaoni si ndio wapo uraiani? Wakihamasishana hakuna kupiga kura hiyo siku ya uchaguzi utasema Kuna uchaguzi hapo?
Vyama 17 na CCM ya 18 vimekubali kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Sasa vyovyote mtakavyohamasishana watakaosusia uchaguzi ni kundi la watu wachache kati ya wengi ambao wapo tayari kushiriki uchaguzi huu.
Halafu kuna kitu nikiwaangalia nashindwa kuwaelewa sababu kuu ya kugomea uchaguzi ni
A. Kwasababu mifumo ya uchaguzi inahitaji reforms au ni
B . Watu wanatekwa na kuuawa?!
Haya mambo naona yanachanganywa na kufanywa kuwa ni sababu za watu kususia uchaguzi.
Kwani no reforms no election na watu kutekwa na kuuawa vina uhusiano gani?!
Kuweni na sababu moja inayoeleweka ya kususia uchaguzi
Je tatizo ni reforms au ni watu kutekwa na kuuawa?!
 
turn up yoyote ile itiiweka serikali madarakani, huku vijijini ndyo kwenye kura nyingi za CCM na upinzani uko mijini zaidi, huku bush NRNE haina effect yoyote ile, hata uwepo wa vyama vya upinzani ni negligible
Vijijini ni wapi? Mbona heche kote alikopita wananchi kwa maelfu wamesupport NRNE. Acheni propaganda, mitandao ya kijamii imeshaenea mpaka vijijini huku, huku kwetu kalinzi hakuna kijiwe utapita usisikie watu wanajadili mikutano ya Heche licha ya kuwa wapo Bush sana.

Endeleeni kujidanganya tu
 
subiri kampeni ya CCM maeneo hayohayo, uataona NrNe inavyokuwa deleted, na mnaaminisha watu uchaguzi october haufanyiki, ila hamjasema hiyo mechanism ya kuzuia watu nchi nzima wasiende kwa ballot itafanyikaje
 
Andishi refu lakini pumba tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…