Nguvu ya mtandaoni ya #NRNE ni ya Soda tujikumbushe vilivyotamba na kubuma bila mafanikio

Mzuka Wana Jamvi..

Huu ni mwendelezo wa spana kwa Keyboard Warriors na wanaharakati uchwara wote Jf ndani na nje ya nchi.

Naanza kuflow sasa ; naona Kuna watu wameanza kujipa matumani baada ya kuona mitandaoni sasa Insta na kwengineko kwenye comments session #NoReformNoElection inatamba sana na imetawala sasa wameanza kujipa matumani kuwa Wabongo wameamka na huu ndio mwaka wa mabadiliko .

Sasa niwaweke wazi wengi wao wanafuata mkumbo tu hawajui hata maana ya wanachokisema kiuhalisia Wala hizo reforms zinazodaiwa ni za namna gani bali wao wanaweka tu kupata likes na kufuata upepo kwani ukiweka tu unapata likes nyingi za fasta na wabongo huwaambii kitu kwenye kupata likes na kwenda na upepo.

Sasa tujikukumbushe mengine ya nguvu ya Soda yaliyopita ;

1. Maandamano ya Mange Kimambi ; sikumbuki mwaka gani alipiga kampeni na ilibamba mitandaoni kote na kupata nguvu kubwa kuwa kutakuwa na maandamano nchi nzima na watu waliitika ila siku yenyewe polisi wachache tu walijitokeza kufanya usafi hapakuwepo hata mtu mmoja aliyetoka front Wala dalili ya watu kuandamana

2. Kampeni za Membe ; nakumbuka humu Jf , Jamuhuri ya Twitter na kwengineko Bernard Membe alionekana na nguvu na ushawishi mkubwa watu wakamuona kuwa ni Rais ayaje na mpaka ajaye , ikadhihirika wakati wa Kampeni hakuna watu kabisa hata 50 hawafiki mpaka Mzee wa watu akaamua kujitoa mapema kwenye mbio za urais.

3. Maandamano ya Chadema ; mapema sana siku ya tukio Raia walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida kama hakuna kinachoendelea .

4. Nk

My Take .

Wabongo kwenye kuongea na kusapoti mitandaoni, kwa kutype na hastag na kwenda na upepo wako vizuri sana ila kwenye ground mapema sana wanakuacha kwenye mataa na asilimia kubwa ya Wabongo hawana habari na mambo ya mtandaoni .

Hivyo kitu chochote ili kipate nguvu bongoland kampeni zianze chini kwa watu wa kawaida ambao ndio asilimia kubwa na ndio watu wa Maamuzi , kuliko Walamba lips 👄 👄 wa mitandaoni wao support Yao kubwa ni kutembeza hashtag nyuma ya Keyboard huku wakinywa Tungi.

Kama mnabisha naomba huu Uzi uwekwe kama kumbukumbu kwa Matumizi ya baadae kama rejea maana Mimi ni mtu wa maono .
WEWE UKO SERIOUS.KIASI GANI?
 
Vyama 17 na CCM ya 18 vimekubali kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Sasa vyovyote mtakavyohamasishana watakaosusia uchaguzi ni kundi la watu wachache kati ya wengi ambao wapo tayari kushiriki uchaguzi huu.
Halafu kuna kitu nikiwaangalia nashindwa kuwaelewa sababu kuu ya kugomea uchaguzi ni
A. Kwasababu mifumo ya uchaguzi inahitaji reforms au ni
B . Watu wanatekwa na kuuawa?!
Haya mambo naona yanachanganywa na kufanywa kuwa ni sababu za watu kususia uchaguzi.
Kwani no reforms no election na watu kutekwa na kuuawa vina uhusiano gani?!
Kuweni na sababu moja inayoeleweka ya kususia uchaguzi
Je tatizo ni reforms au ni watu kutekwa na kuuawa?!
Vyote vinaenda pamoja maana ni ndani ya misingi 11 ya demokrasia. Uhuru wa maoni unavurugwa kwa kutekwa, sasa kama uchaguzi bado watu wanatekwa ndio sembuse ukitangaza kugombea dhidi ya CCM. So kutekwa kuna affect pia ushiriki wa uchaguzi wenye demokrasia maana kunakua na hofu ya kuchagua chama mbadala.

Kingine hata tukishiriki bado CCM itapewa ushindi wa majimbo yote ya ubunge na urais atashinda kwa 90% so tutapoteza tu hela ya campaign na damu zitamwagika.

Precedence aliyo set JPM ndio inatutafuna na ndio itakua milele kila chaguzi ni kama 2020 mpaka hapo jeshi litakapoamua kupindua serikali otherwise tunapoteza muda tu.
 
subiri kampeni ya CCM maeneo hayohayo, uataona NrNe inavyokuwa deleted, na mnaaminisha watu uchaguzi october haufanyiki, ila hamjasema hiyo mechanism ya kuzuia watu nchi nzima wasiende kwa ballot itafanyikaje :420Pls:
CCM ipi itaweza zuia NRNE, kama wanajiamini si walete reforms alafu tuone wananchi wamekubali chadema au Ccm. Yaani mnaogopa kuweka uwanja sawa alafu muda huo huo mnajisifia mnapendwa?

Haupo serious, Tanzania vijana chini ya 35 ni 70% na hao wamezaliwa kipindi cha vyama vingi unadhani hao wanaweza ipigia kura CCM? mnakera sana wezi nyie, ila kila kitu kina mwisho wake. Kwani Mugabe au Nkuruzinza kiko wapi?.
 
Mimi yanayonihusu ni kula yangu na Familia yangu pamoja na kuhakikisha Mimi Nakuwa mtu Bora na Familia yangu mengine ni ziada tu.
Hata mimi niko hivohivo lakin najua dunian watu hatuwez kufanana.
Hata kipindi cha akina nyereee najua kuna waliomwita kiherehere, walimshangaa kwamba anajishughulishaje na watu wasio familia yake?
Mwaka 1900 chirf Mangi aliponyongwa na wajeruman kuna watu walimuona ni kiherehere.

Kifupi mkuu ujue tuu kwamba tabia yangu mimi nawewe sio SI-unit ya watu wote.
Hivyo kama kuna wanao tekwa tusiwaone majinga kwakuwa hawabehave kamasis.
Bali tuangalie ni kwa kosa gani wamestahili hukumu hiyo na hao wanaoteka ni majambaz au? Kama sio kwani polisi si ipo na mahakama je?
 
Ukiwa focous na mambo yasiyokuhusu lazima yakukute .

Wanaonihusu wako bize na mambo Yao wanapiga jembe hawataki uWanaharakati uchwara na kuinglia yasiyowahusu . Na ukiona wametekwa labda wajiteke wenyewe.
Kwahyo kufocus na yasiyo yako ndo kustahili kuuawa au hata humo safarini tunaposaidia au kusaidiwa na watu tusiofahamiana napo tupotezwe, kwakuwa ni mambo yasiyo tuhusu?
 
Mbona wewe haujatekwa wala kuuwawa mpaka muda huu , unaweza kunipa sababu ?

Hii ichi ina Watanzania wangapi na waliotekwa wanavuka hata asilimia 0.5 ya Watanzania wote?
Kwahyo mkuu mtu gari ikipata ajali mtu akafiwa na nzaz wake na wengine wote wakapona hapaswi kulia sio?
Au mbona hata vitani akifa askar mmoja tuu wanaona wapepata pigo, ila wew unataka wafe watu mpaka watu 3000 ndo uone kwamba ni jambi la kutisha asee akili ni nywele mkuu.
 
turn up yoyote ile itiiweka serikali madarakani, huku vijijini ndyo kwenye kura nyingi za CCM na upinzani uko mijini zaidi, huku bush NRNE haina effect yoyote ile, hata uwepo wa vyama vya upinzani ni negligible
CCM ina shughulika na matatizo ya msingi, maji, umeme, barabara, uwezeshaji wa biashara kubwa na ndogo na hayo ndio masuala yanayopigiwa kura siku ya uchaguzi.
 
Mzuka Wana Jamvi..

Huu ni mwendelezo wa spana kwa Keyboard Warriors na wanaharakati uchwara wote Jf ndani na nje ya nchi.

Naanza kuflow sasa ; naona Kuna watu wameanza kujipa matumani baada ya kuona mitandaoni sasa Insta na kwengineko kwenye comments session #NoReformNoElection inatamba sana na imetawala sasa wameanza kujipa matumani kuwa Wabongo wameamka na huu ndio mwaka wa mabadiliko .

Sasa niwaweke wazi wengi wao wanafuata mkumbo tu hawajui hata maana ya wanachokisema kiuhalisia Wala hizo reforms zinazodaiwa ni za namna gani bali wao wanaweka tu kupata likes na kufuata upepo kwani ukiweka tu unapata likes nyingi za fasta na wabongo huwaambii kitu kwenye kupata likes na kwenda na upepo.

Sasa tujikukumbushe mengine ya nguvu ya Soda yaliyopita ;

1. Maandamano ya Mange Kimambi ; sikumbuki mwaka gani alipiga kampeni na ilibamba mitandaoni kote na kupata nguvu kubwa kuwa kutakuwa na maandamano nchi nzima na watu waliitika ila siku yenyewe polisi wachache tu walijitokeza kufanya usafi hapakuwepo hata mtu mmoja aliyetoka front Wala dalili ya watu kuandamana

2. Kampeni za Membe ; nakumbuka humu Jf , Jamuhuri ya Twitter na kwengineko Bernard Membe alionekana na nguvu na ushawishi mkubwa watu wakamuona kuwa ni Rais ayaje na mpaka ajaye , ikadhihirika wakati wa Kampeni hakuna watu kabisa hata 50 hawafiki mpaka Mzee wa watu akaamua kujitoa mapema kwenye mbio za urais.

3. Maandamano ya Chadema ; mapema sana siku ya tukio Raia walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida kama hakuna kinachoendelea .

4. Nk

My Take .

Wabongo kwenye kuongea na kusapoti mitandaoni, kwa kutype na hastag na kwenda na upepo wako vizuri sana ila kwenye ground mapema sana wanakuacha kwenye mataa na asilimia kubwa ya Wabongo hawana habari na mambo ya mtandaoni .

Hivyo kitu chochote ili kipate nguvu bongoland kampeni zianze chini kwa watu wa kawaida ambao ndio asilimia kubwa na ndio watu wa Maamuzi , kuliko Walamba lips 👄 👄 wa mitandaoni wao support Yao kubwa ni kutembeza hashtag nyuma ya Keyboard huku wakinywa Tungi.

Kama mnabisha naomba huu Uzi uwekwe kama kumbukumbu kwa Matumizi ya baadae kama rejea maana Mimi ni mtu wa maono .
No reforms no election
 
Vyama 17 na CCM ya 18 vimekubali kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Sasa vyovyote mtakavyohamasishana watakaosusia uchaguzi ni kundi la watu wachache kati ya wengi ambao wapo tayari kushiriki uchaguzi huu.
Halafu kuna kitu nikiwaangalia nashindwa kuwaelewa sababu kuu ya kugomea uchaguzi ni
A. Kwasababu mifumo ya uchaguzi inahitaji reforms au ni
B . Watu wanatekwa na kuuawa?!
Haya mambo naona yanachanganywa na kufanywa kuwa ni sababu za watu kususia uchaguzi.
Kwani no reforms no election na watu kutekwa na kuuawa vina uhusiano gani?!
Kuweni na sababu moja inayoeleweka ya kususia uchaguzi
Je tatizo ni reforms au ni watu kutekwa na kuuawa?!
Hivyo vyama 17 ukiondoa ACT Tena kwa Zanzibar waliobaki hawana wanachama.
 
Nakumbuka 2017 hivi yalitangazwa maandamo makubwa nchi nzima ya UKUTA basi bana walipromotiwa mwezi mzima nikasema haya hapo kweli sasa inafika siku ya siku dadeki kimya kama hakuna kitu😁😁😁
 
CCM ipi itaweza zuia NRNE, kama wanajiamini si walete reforms alafu tuone wananchi wamekubali chadema au Ccm. Yaani mnaogopa kuweka uwanja sawa alafu muda huo huo mnajisifia mnapendwa?

Haupo serious, Tanzania vijana chini ya 35 ni 70% na hao wamezaliwa kipindi cha vyama vingi unadhani hao wanaweza ipigia kura CCM? mnakera sana wezi nyie, ila kila kitu kina mwisho wake. Kwani Mugabe au Nkuruzinza kiko wapi?.
Hizi ni kauli za mtu aliyekata tamaa na hajui nini chakufanya.Unatakiwa ujue uchaguzi na madaraka sio mambo utakayoletewa kama ubwabwa kwenye sahani.Hakuna nchi yenye uchaguzi huru wa asilimia 100 duniani unaohusisha vyama vingi.Kupata madaraka lazima kuwe na mipango mikakati itakayowafanya wenye maamuzi kuona huyu kweli anafaa na huyu hafai.Ukisema tu watu watachagua wanaweza wakachagua ata kichaa aongoze nchi.Je ndio lengo la demokrasia na uhuru wa uchaguzi?.
 
hafai.Ukisema tu watu watachagua wanaweza wakachagua ata kichaa aongoze nchi.Je ndio lengo la demokrasia na uhuru wa uchaguzi?.
Yes mbona "kichaa" Trump alichaguliwa licha ya kuonekana kutopendwa na wengi? That's democracy
 
Back
Top Bottom