Perceptions yako ya mafanikio ndo tunatofautiana kwani kuna ulazima wa watu kufa kwa wingi ule ndo ionekane nchi inakombolewa???
Unayoyaita mafanikio mie naona huo umwagaji damu unawahusu wote kwa hizo damu za wenzetu zilizo potea na hapa nawaingiza hawa waliochangia hili
Wanasiasa (Chama tawala chini ya Rais Samia na wapinzani hasa Chadema maana wao wapo tayari kuona damu za vijana wadogo na maisha yakipotea ili wafike ikulu)
Pili Wanaharakati kwa sababu halisi au zile wanazozijua wao (kama inavyosemekana wengine wamelipwa pesa kama kuna ukweli) nao hao wamechangia umwagaji wa damu kwa hamasa waliyoitoa na hili kundi pia wali wa mislead waandamanaji kwa kuwapa ujasiri wa kutoka kwa wingi kwamba kuna hakikisho la usalama wao kutoka idara nyingine ya ulinzi lkn wote tumeshuhudia kilichotokea na tunajifanya hatuoni hilo la wao kupotosha kwa taarifa zao , hapa wapo kina Mange, Maria sijui Sativa , Vazi nuru na wengineo
Baadhi ya viongozi wa dini nao kwa namna moja au nyingine wamechangia umwagaji damu huu kwa waraka na matumaini waliyo yatoa na kutumia neno haki haipo kwa sababu za wazi na zile wajuao wao ( sijasema hawakpaswa kusema ila wao nao ni sehemu ya kilichotufikisha hapa na yaliyotokea) hapa TEC na Gwajima unawaweka humu
Kwahiyo neno mafanikio ni mtizamo tu inategema unatizama kwa upande upi ila kwangu sijaona mafanikio mpaka sasa zaidi ya mparaganyiko na hofu na hizo damu zilizomwagika na wahusika ni hao kwa mtizamo wangu wenye dola ( chama tawala) na wanaotaka dola (wapinzani na hasa Chadema) na wapiga debe hao kina TEC na baadhi ya wachungaji kwa sababu zao dhahiri na zilizofichikana