Ni sawa mkuu na umechambua vyema tu, napingana na wewe kusema hakuna wajasiramali walio poteza mali zao hili si kweli kwa mfano kuna jamaa alichomewa mbao zake pale buguruni kama sikosei, achia mbali duka la Sharo au Jux au kibanda cha chakula cha shishi bila kusahau baadhi ya mikoa kuna wajasiliamali wamepata hasara au wewe kwako mjasiriamali ni mtu wa aina ipi?
Hujaelewa hoja yangu, labda umesoma kwa pupa... Anyway Kama wewe vitu vyako vilichomwa au vya wengine basi hao watu/wajasiriamali wana uhusiano na mafisadi/ufisadi, ndiyo maana watu wameamua kushusha hasira zao hapo.
Mfano Sheri nyingi zilizo chomwa zilikua ni lake oil, kwanini zichomww tu hizo na si zingine?
Shida nyingine maandamano ya natakiwa hata yawe na kiongozi kama hii mradi tutoke tu inaweza kuja tena kama ya 29 na ikiwa watatoka wengi kama unavyosema na kumbuka nimesema kuna watu wanaweza toka kwa sababu za mwanzo kabla ya tarehe 29 na wengine baada ya matukio ya 29 wanaweza toka lkn kuna wengine wanaweza wasitoke pia kwa hizo shift za matukio yanavyojitokeza
Pengine hufuatilii saivi kinacho endelea, utakua umesikia tu Kuna maandamano 9D basi ukaja na direct judgement.
Uliyo yaona Oct 29 hayatorudi saivi watu wamekuja systematically and strategically, naamini kabisa haya yanayo kuja yatakuwa bora kuzidi yaliyo pita na yeyote atakaye jaribu kuwagusa wandamanaji anajichimbia kaburi.
Suala la kina TEC ni mtizamo wangu binafsi na wala sio suala la leo lkn kwa jicho la ndani kuna kuangalia fursa kutokana na mgogoro huu pia japokuwa neno haki kuna muda wana misuse hasa kukiwa kuna faida au hakuna faida kwa upande wao
Ok nakubaliana na hiye perception yako but sorry Unaweza onesha angalau kidogo madhaifu ya TEC hasa pale panapo tokea Kuna faida upande wao kama unavyo dai?
Hitimisho, mie sipingi watu kuandamana ni njia pekee ya kuonyesha matamanio na mabadiliko ya watu kwa wanachokitaka na kukataa ukandamizaji na kukandamiza uhuru wa mtu wa maoni na mitizamo yao
Safi, lakini ni vizuri zaidi kuwaunga mkono.. sauti au maneno yako yatakuwa ni motisha kwa wapambanaji kueleke ushindi.
Ninacho pinga ni aina ya kuandamana na hila za baadhi ya wanao push kuandamana kwa mgongo wa damu za vijana wengine wa kimasikini na uchache wa elimu na exposure
Mkuu, kuandamana siyo kosa kisheria, Katiba yetu imeribariki hilo.. ni haki kila mwananchi pale anapo ona kero zake hazitatuliki ni haki yake kuandamana kushinikiza serikari kutimiza wajibu wake.
Anaye ua wandamanaji ndiyo mwenye kosa anavunja katiba ya nchi lakini pia anavunja Sheria za kulinda haki za Binadamu (International human right law) huyo ndiye anatakiwa kuadhibiwa.
Kusema Kuwa watu wanatoa vijana sadaka Huku wao wakiwa nje, labda tu inaweza Kuwa ni ufinyu wako wa kufikiri.
Kitu kama hichi inabidi serikari pamoja na nyie wadau mjiulize kwanini vijana wanafuata na kusikiliza wanaharkati wa nje? Kwanini vijana wamekosa Imani kwa serikari yao?
Kama ndivyo kwambia awali Saivi vijana ni wasomi na smart wanaelewa wanacho kifanya siyo rahisi kudanganyika hivyo.