Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Upendo ni asili ya mtu mweusi, hata wakoloni walipofika Afrika walishangaa kuona upendo mkubwa katika jamii yetu. Mjane wa kaka alitafutiwa mume katika ukoo ule wa mune wake ili watoto walelewe kwenye ukoo na wasipate shida. Mgonjwa aliyeshindwa kulima familia yake ilikula bila wasiwasi. Jamii ilimchangia chakula mpaka matokeo ya ugonjwa yafikie hatima yake.
Upendo ndiyo ulimfanya Mwalimu Nyerere kupigania kulikomboa bara la Afrika. Aliwalaza macho Makaburu pamoja na pesa na tekinolojia waliokuwa nayo. Heshima ya Nyerere katika Afrika haita kaa ipotee.
Baada ya uchaguzi 2015, idadi ya wabunge na madiwani wa upinzani ilikua kubwa. Mbinu kubwa ilitumika kuwanunua wanasiasa hawa. Kama tu angetokea mwenye hekima na kuwapatia madiwani milioni 50 za kubadilisha mazingira ya wazee, watoto yatima, walemavu na wajane katika mtaa wake na matokeo yaonekane. Hata kuwajengea nyumba Bora za gharama nafuu,
Hii ingekua silaha bora ya kuushinda upinzani kuliko kulipa madeni ya wanasiasa na kuwapa pesa kwaajili ya matumbo yao.