Nguvu ya wachache walioweza kufanikiwa sehemu ngumu inafanya wengi wawe masikini, epuka huo mkumbo !! fanya kitu cha uhakika vingine weka plan b

Nguvu ya wachache walioweza kufanikiwa sehemu ngumu inafanya wengi wawe masikini, epuka huo mkumbo !! fanya kitu cha uhakika vingine weka plan b

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Bakhresa, GSM, Mo Dewji na wafanyabiashara wachache hapa Tanzania wamechana msamba, ni ndoto za abunuwasi kudhani unaweza fika hapo kwa kuacha kitu cha uhakika unachoweza fanya bila backup plan, connections, resources, n.k. utashangaa mtu anaacha kazi na hajawahi kufanya biashara eti hakuna tajiri alieajiriwa, iga ufe

Diamond ni msanii aliefanikiwa lakini ni kundi la asimilia 0.01 ya wasanii wa Tanzania walioweza kufikia hapo, ukifanya maamuzi ya kuacha kitu cha uhakika au chenye nafuu ya uhakika uwe msanii una nafasi ndogo sana kufika stage za kina Mario achilia mbali kabisa kina Diamond, fikiri nje ya box fanya cha uhakika kilichokomboa wengi iwe ni kilimo, biashara, ajira, n.k. kama ni muziki weka plan b.

na kuna vitu vingi sana ambavyo wachache wamefikia levels hizo, nguvu ya wachache isije kukuharibia maisha
 
Kwa hio kwa kifupi unasema tuajiriwe tusijiajiri?
 
Bakhresa na mo dewj sijui huko waliko wanajionaje maana wabongo tunavyowaongelea haipiti siku bila kutolewa mifano
 
Watu hukurupuka tu, watu hutofautiana mazingira walipotoka, historia ya familia, mtazamo wa familia kuhusu maisha, msingi wa kiuchumi wa familia nk...Kila mmoja aangalie factors nyingi kama anaweza kutoboa, ww huna chochote zaidi ya mtaji tu hata instincts pia huna then ufike level hizo...hiyo mifano huko juu wazazi wao walianzia mbali na kuzunguka TZ nzima kufanya biashara then wakaamua kuwekeza Kwa watoto wao Leo hii wako hapo...lazima Kila mmoja afikirie Kwa kina kabla ya kuingia huko.
 
Back
Top Bottom