PostGE2025 Nguvu ya Wananchi Kwenye Giza la Uchumi: Tumaini la Tanzania Mpya

PostGE2025 Nguvu ya Wananchi Kwenye Giza la Uchumi: Tumaini la Tanzania Mpya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Hali ya sasa imefika mahali ambapo moyo wa kawaida umeshindwa kubeba. Tumekuwa tukipambana, tukitafuta angalau mwanga mdogo ili tuendelee kuishi, lakini ukweli mchungu ni kwamba hatuoni huo mwanga tena. Kwa sisi tunaoishi kwa kutegemea utalii maisha yamekuwa kama kupita kwenye jangwa bila hata tone la maji. Kila siku unakaza roho lakini reality bado inakulazimisha kukubali kuwa huu ugumu hauna budi ila kuusukuma kimya kimya.

Kinachoumiza zaidi ni kuona kwamba mzigo huu mzito unaangukia kwa wananchi tu. Wale waliopewa dhamana ya kutuongoza wanaendelea kuishi kwenye comfort zone kana kwamba storm hii haipo. Ni kama sisi ndio tunahitajika kuwa survivors wa kila aina ya maumivu ilhali wao wanaendelea na maisha yao bila pressure. Sometimes unajiuliza kama kweli wanaona kinachoendelea au wanaamua kuzima macho tu. This thing hits different. Inakula ndani kabisa.

Lakini pamoja na hii dark cloud iliyotanda juu ya taifa letu bado tuna sababu moja ya kushikilia tumaini. Mungu. Yeye ndiye shahidi wa machozi tuliyoficha usiku, maombi tuliyopiga kimya kimya, na ndoto zilizoanza kufifia kwa sababu ya hali ya uchumi na jamii yetu. Mungu ndiye anayeona tofauti kati ya nguvu tulizonazo sisi na mamlaka walizonazo watawala. Atajua mwenye kusimama upande upi. Huo ndio ukweli ambao hakuna system inaweza kuufuta.

Ndugu zangu tuendelee kumuomba Mungu atujalie Tanzania mpya. Tanzania yenye haki na mshikamano Tanzania ambayo haina watu wanaotembea kwa hofu ya kesho. Tanzania ambayo huwezi kukosa usingizi kwa sababu ya njaa au kukosa ajira Tanzania ambayo heshima ya kila binadamu inahesabika. I believe deep down kwamba majibu yapo njiani. Labda si leo labda si kesho lakini yatakuja. Na yakija yatakuja kama nguvu ya light inayosambaratisha darkness bila huruma.

Tudumu katika imani hiyo. Hii siyo weakness. Hii ni resilience. Hii ni nguvu ya watu wanaog refuse kuzimwa hata pale wanapokuwa wamechoka kupita maelezo.
 
Back
Top Bottom