Yohana Charles-David Lymo
New Member
- Jul 23, 2021
- 1
- 1
NGUVU YANGU NI SERIKALI, NA MIMI NDIYO SERIKALI YENYEWE!
Nilipokuwa mdogo, sikuwa natambua umuhimu, ama kazi za koki ya bomba la maji kwasababu mara zote niliona mabomba hususani sehemu za umma yakitiririsha maji lakini maji hayo yalidhibitiwa kwa vitu vingine tofauti kabisa na koki, ambapo kama si “gunzi” la muhindi basi ni “kitindi” cha muwa, na kama si kitindi basi ni mfuko wa plastiki, pengine kama ungebahatika kuikuta koki bombani basi nayo ingefanya kazi kwa msaada wa egesho la tofali zima ama kipande chake.
Koki zilikuwa ziking'olewa na watu wenyewe
Hata nilipoingia elimu ya msingi, vivyohivyo, bomba la shule liliendelea kunionyesha taswira ileile niliyoizoea. Wanafunzi tulipenda kuona maji yakitiririka muda wote, koki ziliendelea kung'olewa na njia zilezile tulizoona zinatumika mitaani kwetu, ziliendelea kutumika hata shuleni pia. Hatukufahamu maji yanakotokea, hatukujua bei ya koki, wala hatukutambua kwamba maji hayo hulipiwa na mradi wowote ili ukue sharti uweze kujimudu wenyewe. Mwisho wa siku mabomba yale yalizibwa na hayajatoa maji hata leo.
Baada ya maarifa mengi kuongezeka kupitia nyanja mbali mbali za kielimu, ndipo nimefahamu kwamba, kumbe serikali ilikuwa inaingia gharama nyingi za lazima kufanya maboresho ya miundombinu ya maji iliyokuwa inaharibiwa kwa makusudi na raia wenyewe na kamwe hatukuacha kupaza sauti zetu tukisema;- “Tunacheleweshewa maendeleo!” ingali kitanzi tulikitengeneza na kujivisha wenyewe.
Hebu tujaribu kulipima hili katika mazingira haya, leo hii kijana yule aliyelelewa katika jamii ya watu hawa anapata wadhfa wa uongozi sekta fulani, ama anapewa usimamizi wa raslimali katika kuchochea maendeleo. Je, atakuwa thabiti ama anaweza kuwa na uchungu wa kuitunza miradi hiyo ya maendeleo kwa manufaa ya jamii nzima?
Je, ataweza vipi kuwaonyesha ama kuwafundisha uzalendo hao wanaomtazama kama dira ingali yeye mwenyewe uzalendo haujui?
Kumbe sasa sisi kama jamii ki-ujumla tunalo jukumu la kushirikiana kwa pamoja katika kukiandaa na kukijenga kizazi chenye misingi bora ya uzalendo ili kuepukana na wimbi la watu waliokosa weledi. “Mtoto wa mwenzio ni wako” akifanikiwa, taifa limefanikiwa kwa matunda yake, akiharibikiwa sote pia tumeharibikiwa kwa gharama za matunda ya uharibifu, “kwani nguvu yetu ni serikali na sisi ndiyo Serikali yenyewe!”
Hivyo basi, sisi kama raia tunao wajibu wa kutambua thamani ya rasilimali hata miundombinu tuliyojengewa katika kuilinda na kuitunza vema, pasipo kusubiri viongozi wetu ama makosa yao ndiyo yatukumbushe.
Yakizingatiwa haya ndipo tutashuhudia udhibiti katika uharibifu wa miundombinu, upotevu wa mali hata upungufu wa nguvu kazi unaoweza kusababishwa na ajali, machafuko mpaka mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira
Tutashuhudia nidhamu na weledi kwa watumishi wa umma ambapo vitendo vya unyanyasaji, unyonyaji, ukandamizaji, rushwa na vingine vingi vifananavyo na hivyo vitapungua kama si kumalizika kabisa
Haya ni kwa uchache tu pengine yapo mengi zaidi, lakini ni hakika ya kwamba, nyumba yoyote isipokuwa na msingi imara hata ikawa nzuri kama nini, HAIDUMU!
Misingi imara ya maendeleo ya jamii yoyote ile, hata taifa kiujumla inajengwa na kizazi thabiti chenye uzalendo wa kweli juu ya ardhi yake. Tofauti na hapo, jamii itaendelea kuzalisha nasaba za Mafisadi, Majasusi, na aina za watu wengi wenye karama za kutishia amani ndani ya mioyo ya wengine, ambapo mwisho wa yote hata ile nuru kidogo tuliyoanza ama tuliyokuwa tukiitazama, hatutaiona tena.

Upvote
1