NHC kutumia Tsh. Bilioni 466 mradi wa Samia Housing Scheme

Vipi yale majengo yaliyotelekezwa kule kawe, hadi yamepigwa ukungu......hakuna mwendelezo yaani, ni mwendo wa kutafuta kiki kwa mama.
Mama ameamua kila kitu kilichokua kimesimama atakifanikisha
 


Bei nafuu ni kiasi gani? Je serikali inaendelea na utaratibu wa kuweka 18% kwenye ununuzi wa nyumba?
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Subiri bei zake ndio utajua walengwa ni kina nani
Hivi wakatii mwingine mie huwa najiuliza, eti watz wenye mahitaji kama hayo huwa ni wa Dar es salam tu, na wale wa mikoani huwa ni kutoka Burundi'???? Kaazi kwelikweli......
 
Sasa hawa nao, mradi wa 7Eleven pale Kawe Beach uliishia wapi, kwa nini wasiendeleze huo na kufungua zile za Morocco Square?
 
Kwa hesabu za haraka hapo kila nyumba ni 100m. Kwa bei ya jumla, na jinsi wabongo wanavyojenga hapo zilitakiwa zitoke nyumba 15,000. Waache longolongo, hiyo pesa wapeleke wakawatengenezee vijana ajira, huko wanaenda kupiga na kutupa pesa. bashe kaanzisha ekari 8,000 za vijana kulima. waongeze pesa huko kwenye tija.
 
Kwa haraka tu given the investment sums and number of units projected. On average kila nyumba itajengwa kwa 93.2 million + inflation adjustment + mark up profit + bank interest maana hiyo hela watakuwa wamekopa tu; kwa haraka haraka sioni hizo nyumba kuuzwa chini ya tsh 120 million.

Sasa zikiisha kuna watu wanaweza jenga individual units privately kubwa zaidi with more rooms and back yards at lower price. Bear in mind mradi kama huo kwa NHS wana economies of scale na kama wana team nzuri ya procurement wanaweza pata deal nzuri ya components kama saruji, nondo etc at cheaper price than the retail ambazo individuals wananunulia so in essence nyumba zao on similar size na mtu anaejenga private zinatakiwa kuwa cheap.

What you see from these bozzos is beyond me.
 
" Nyumba za Bei nafuu ambazo MTANZANIA wa kawaida anamudu kununua😯😯😯😯😯"

Kauli inaudhi hii!!!!!
 
Mradi usio na tija pesa za umma ndio zinaenda kutumbukizwa hapo matokeo yake biashara itadoda hivyo kutoa mwanya wenye fedha kuzimiliki. Mradi ulianzishwa na JK lakini ulipigwa chini na JPM kwa kuzingatia hapakuwa na tija kipindi hicho kuingiliana na serikali kuhamia rasmi Dodoma. Inawezekana mstaafu mmoja anayeishi kando ya bahari ya hindi akitizamana na eneo la Tanganyika packers ndiye mwenye maslahi mradi ufufuliwe ila kwa sura tofauti kwa maslahi ya kisiasa.
 

Kwa taarifa tu ni kua mastermind wa mradi amehamishiwa hazina.
 
Hivi wakatii mwingine mie huwa najiuliza, eti watz wenye mahitaji kama hayo huwa ni wa Dar es salam tu, na wale wa mikoani huwa ni kutoka Burundi'???? Kaazi kwelikweli......
Yaani hata mimi nawaza hivyo hivyo, kwa nini kila kitu Tanzania ni Dar es Salaam tu? Akili za viongozi wote zimeishia Dar.
Nchi mbalimbali duniani uwa zinapanua huduma kwa wananchi na hata ujenzi wa nyumba sehemu mbalimbali. Lakini Tanzania sielewi kabisa nini kinaendelea. Sasa itakuwa Dar na Dodoma pekee! Ha ha ha!

Katika nchi zingine kila eneo la mji unaendelezwa na kuwekewa umuhimu wake. Sasa Bongo sijui ni ushamba hata sielewi! Kila kiongozi anababaikia Dar es Salaam! Nadhani hata vyoo vya Taifa vinajengwa Dar es Salaam. Ha ha ha!
 
Kwa Nini hawakuenda kununua zile za NSSF kule sijui wanaita Mji mwema/mpya au Kigamboni.
Zinaozea hapo kutafuta mnunuzi au mvua!
Kweli mchezo mchafu bado tutahangaika sana.
 
Appartment moja inauzwa bei karibu na bure 138 million only kuwezesha Wanyonge nao waweze kumiliki Makazi
Huyo mnyonge mnyongeni mwenye ako na Mil. 140 ako wapi?!
Hao hao walioko Nyuma yake ndio wanunuzi wakubwa Tena Kwa hela ile ile anayowapa ya Maendeleo wakiendelea kuzipigaa! Tanzania buanah!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…