NHC: Ujenzi wote wa Nyumba za makazi na Ofisi za Umma ziwe kazi za na mali za milele ya Tanzania National Housing Corporation

NHC: Ujenzi wote wa Nyumba za makazi na Ofisi za Umma ziwe kazi za na mali za milele ya Tanzania National Housing Corporation

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
U hali gani Tanzania !

Naomba niweke mchango wangu wa mawazo hapa Jamii Forums.

Napenda kuweka wazo rasmi kwa National Housing Corporation (NHC) kuwa ipewe umakini, umuhimu na umaanani katika ujenzi wa nyumba zote za Makazi na Majengo ya Umma hapa nchini yaani isitokee Raia yoyote afanye ujenzi wa Nyumba ya makazi ball shughuli hizo zote zinafanywe na huyu NHC.
(Nyumba zote za Wananchi zitaifishwe na kuwa Mali ya Shirika (NHC) na Majengo yote ya Umma yataifishwe na yawe Mali ya NHC)

1. Nyumba zitakazo jengwa za makazi ya Umma ziwe za kawaida zenye mahitaji muhimu ya kijamii mfano; maji, umeme, gesi na mawasiliano. Hii baada ya mtaifisho kufanyika. Nyumba zitakazo jengwa zifuate mfumo huo.

2. Nyumba na Majengo yote ya Umma ziwe za kupangwishwa. Yaani asiwepo mtu au watu au taasisi ya Umma wanaomiliki Nyumba za Makazi au Ofisi bali ziwe mali ya shirika.

3. Gharama za malipo kwa hizo nyumba zisizidi Tsh.100,000/= kwa maeneo ya Mjini (Manispaa & Jiji) na Tsh.20,000/= kwa kijijjni (Halmashauri). Hii ni kwa Nyumba za Makazi pekee.

3. Pasiwepo na mikopo ya Nyumba za makazi hapa nchini. Hii ni kwa Nyumba za makazi.

4. Mwananchi/ Raia / Shirika ataruhusiwa na NHC kubuni na kujenga jengo la biashara kwa gharama zake. Kwa upande wa makazi ni hapana. Hii itafaa kwa maslahi ya biashara pekee.

NB

1. Wananchi watakuwa na makazi bora yaliyopangilika vizuri.

2. Nchi itakuwa salama kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimazingira.

3. Wananchi watawaza zaidi kufanya kazi na kuliletea taifa maendeleo kuliko kuwaza upuuzi wa ujenzi wa makazi na uchafuzi wa mazingira.
 
Ingelikuwa vyema kama NHC wangekuwa na uwezo huo. Lakini Kwa bahati mbaya hawana huo uwezo.

Kabla ya kujenga nyumba za makazi, hebu tuwapime kama wanao hata uwezo wa kujenga hospital, zahanati na vyumba vya Madarasa nchi nzima na nyumba za watumishi. Wakiliweza hilo, pole pole tutaanza kuwapa jukumu la kutujengea makazi, Kwa kuanza na miji michache ya mfano.

Na siamini kama uwezo na dhamira ya kufanya hivyo vipo. Kama tu kupima viwanja vya makazi, kuplani miji na kusimamia ujenzi au kuzuia ujenzi holela wameshindwa sembuse, hilo la kujenga makazi ya watu nchi nzima!! Hilo tutabaki kulisikia huko kwingine duniani siyo hapa kwetu.

But all in all it's a good idea, which remains as sweet dream that one would not like to part from it, yet has to let it go.
 
Hodi hodi!

Kwenye hayo maboresho ya muswada wenu wa muswada wekeni na hii kitu tafadhali sio ufahari raia au wananchi kujenga nyumba kwa kigezo cha kipato hapana.

Tuchukue hatua maana tunapenda maendeleo ya kuwa na nyumba bora na makazi mazuri.

Shirika la Nyumba la Taifa nyie ndio kila kitu kwenye maendeleo ya Taifa.
 
Back
Top Bottom