NHC yanunua eneo la Urafiki lenye ekari 50 na majengo yaliyopo kwa Shilingi Bilioni Tatu

AISEE MTACHOMWAAA MOTO KHAAA MAJENGO YOTEE YALEEE NA HK ZOTE AISEE NGOJA NKAKOJOE KWANZA
 
Ni Jambo jema serekali haijapigwa sana, kama watu wengi walivyoizoea! Ila Kuna la kujifunza Kwa NHC, wajijue wao Kwa sasa Ndio tegemeo kubwa katika taifa kupunguza makazi holela, ikumbukwe kwenye hili taifa hasa hasa kwenye wananchi wengi kama Dar es salaam makazi holela ni kero kubwa!! Wizara ya Ardhi imejitoa ufahamu, manispaa wamekuwa wakijiona kama sio jukumu lao!! Sasa ujenzi holela unazidi kushamiri. Jaribu kufikiria Jiji kama Dar es salaam 70% Gari la zimamoto haliwezi kufikia nyumba husika kama Kuna dharura ya Moto!!! Na pia 40% watu hawawezi kufika majumbani na magari Yao, au hata kufikisha mizigo majumbani!! Wenye dhamana wameona ni SAWA,
Mimi sikawii kuisifu NHC ila ningependa Hawa NHC wafanye zaidi!! Kununua maeneo yaliyopimwa tayari au yenye hifadhi nzuri hayatufanyi tukaanza kufurahia, wafanye zaidi kununua maeneo kama manzese, Kawe, mikocheni nyuma ya Tanesco, Sinza uzuri, Kwa mtogole, Vingunguti, Na maeneo mengine holela, na kuyafanyia planning na kuyauza Kwa watu binafsi, hii ingesaidia kupunguza makazi holela, tuchukulie mfano kama vingunguti wenye viwanda wameamua kununua maeneo holela na kugeuza viwanda, au Maghala ya viwanda, mfano kiwanda Cha pipe industry, hii ilitakiwa ipate full support ya manispaa na wizara ya Ardhi ila hadi yote haya yamefanyika, Wizara imekuwa haitoi msukumo, je tuelewe wanafurahia makazi holela!? hii imekuwa haina msukomo wowote wa kimkakati, jamani manispaa, Wizara chini ya Waziri Jerry Silaa fanyeni chochote wananchi tuone angalau tujue mnachukizwa na makazi holela, tupo nyuma yenu!!!
 
Eneo kubwa kama hilo tena katikati ya mji kiusalama serikali naona imeona bora ijipigie pande tuu
Eneo ni mali ya serikali na NHC ni mali ya serikali.
Serikali imetoa eneo lake kwa shirika lake ili liweke makazi.
Wangeweza kuuza pesa nyingi kwa sekta binafs, lakini wafanyabiashara wanaweza kuweka bandari kavu, terminal za malori, na biashara nyingine kama hizo, hali hiyo ingeleta vurugu na usumbufu wa magari makubwa kwenye barabara zinazoingia eneo hilo.
NHC inatosha
 

Huu ujumbe ungefanyiwa kazi tungekuwa mbali
 
CCM HAIWEZI KUTUTOA KWENYE UMASIKINI. Viwanda inaua kisha eneo wanagawana viongozi wa CCM! Wameua Tanganyika Packers wakageuza sehemu ya kuabudu! Tazara wameua wameuza nyumba walizokuwa wanaishi wafanyakazi na karakana imekua shule! Kwa kifupi vyote alivyoanzisha Nyerere wameua badala yake wamewazalisha chawa na viroboto akina Lucas Mwashambwa wawasifie kutwa nzima, huo ndio uchumi wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…