NHC yanunua eneo la Urafiki lenye ekari 50 na majengo yaliyopo kwa Shilingi Bilioni Tatu

NHC yanunua eneo la Urafiki lenye ekari 50 na majengo yaliyopo kwa Shilingi Bilioni Tatu


Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limenunua rasmi eneo la Urafiki na majengo yaliyokuwa chini ya Kampuni ya Urafiki wa Tanzania na China (Tanzania - China Friendship Textile CO LTD) Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ambayo sasa yatakuwa chini ya miliki ya NHC na kufafanua kuwa eneo hili linajumuisha nyumba, maghala, viwanja vya wazi, viwanda na mali nyinginezo.

Katika ziara yake, Saguya alielezea furaha yake na matumaini makubwa kuhusu hatua hii, akibainisha kwamba itasaidia kuboresha miundombinu na kuinua uchumi wa maeneo hayo na kuboresha mandhari ya jiji.

Amesema kuwa NHC, imelinunua eneo hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 50 kutoka kwa mnada wa wazi kikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu.

Alisema kuwa, "Kupitia umiliki huu mpya, Shirika la Nyumba la Taifa limejipanga kuboresha maeneo haya ili kuendana na malengo yetu ya kutoa makazi bora na ya kisasa kwa wananchi. Tumeanza kwa kulipima eneo lote na kutambua mipaka yote inayolihusisha eneo hilo.

Eneo la Urafiki lina historia ndefu ya kuwa kituo muhimu cha viwanda na makazi, kikitoa mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania. Hivi sasa, NHC inapanga kufanyia maboresho makubwa eneo hili kwa kujenga miundombinu bora, nyumba za kisasa, na maeneo ya biashara ambayo yatavutia wawekezaji na wakazi wapya.

Shirika la Nyumba la Taifa linaamini kuwa mradi huu mpya utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa kwa ujumla, na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya makazi na maendeleo ya kiuchumi nchini. Katika mpango wa maendeleo ya NHC, eneo la Urafiki litawekewa mkazo maalum kwa ajili ya kuhakikisha kuwa linakuwa mfano bora wa maendeleo ya kisasa na endelevu.

Muungano alihitimisha kwa kusema, "Hii ni hatua muhimu kwa NHC na kwa taifa letu. Tunawaomba wananchi na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi zetu katika kuboresha na kuendeleza maeneo haya kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na kampuni Kampuni ya Urafiki wa Tanzania na China (Tanzania - China Friendship Textile CO LTD).
Mchakato ulianza siku nyingi wa hilo eneo kwa kuvunja baadhi ya majengo mfano Shule ya Msingi Urafiki ilianza kuvunjwa tokea mwaka juzi wanafunzi wakahamishiwa shule nyingine.

Mimi nataka kupata taarifa ya uhakika kuhusu kiwanda cha Urafiki, kitahamia eneo lingine au ndio mwisho?
 
Mchakato ulianza siku nyingi wa hilo eneo kwa kuvunja baadhi ya majengo mfano Shule ya Msingi Urafiki ilianza kuvunjwa tokea mwaka juzi wanafunzi wakahamishiwa shule nyingine.

Mimi nataka kupata taarifa ya uhakika kuhusu kiwanda cha Urafiki, kitahamia eneo lingine au ndio mwisho?
Kiwanda kilikufa zamani ilibaki kuwa godown tu.
 
Serikali ina pesa za kuchezea urafiki ya bonyokwa inatoa kitita chote hiko, hapo wachina wamelia sana ilibidi wapewe m54
Umeamua kuchangamsha genge au? Eneo hilo la urafiki 1acre sio chini ya $1.5m
 
Eneo ni mali ya serikali na NHC ni mali ya serikali.
Serikali imetoa eneo lake kwa shirika lake ili liweke makazi.
Wangeweza kuuza pesa nyingi kwa sekta binafs, lakini wafanyabiashara wangeweza kuweka bandari kavu, terminal za malori, na biashara nyingine kama hizo, hali hiyo ingeleta vurugu ya magari makubwa kwenye barabara zinazoingia eneo hilo.
NHC inatosha
Sawa kabisa. Ni kama NHC wamepewa tu.
 
Eneo ni la serikali. Na aliyeuziwa NHC na yeye pia ni mali ya serikali.

Mali yako mwenyewe kwa nini ujiuzie kwa bei ghali
Wamesema ulikuwa ni mnada wa wazi. Hii inaua mawazo yako kwa sababu kama ilikuwa ni mdada wa wazi, basi walishiriki watu wengi. (Upande wangu siamini ulikuwa mnada wa wazi kwa sababu bei ya kuuzia ingekuwa kubwa sana). Nadhani aliyeleta habari hakuelewa vizuri au kama wameuza kwa bei hiyo basi kuna mazingira y aupigaji yanaandaliwa, hasa huko kwenye shirika la nyumba. Otherwise kama habari ni sahihi na hakuna makandokando, basi big up, wamefanya vizuri.
 
Back
Top Bottom