Unachosema hapa ni sawa na kuyaambia mashirika ya bima yasikae magari makuukuu (mikweche) yenye namba kama T008AKS kukata bima kubwa (comprehensive). Utakubalije bima ya mtu ambae havai helmet, anaendesha gari/bodaboda bila leseni, analala na kuku wake uvunguni, hana chandarua, anajisaidia vichakani hana choo, hanawi mikono wakati wa kutoka haja kubwa, haogi, havui, hana chakula nyumbani, nyumbani kuna viroboto, anakunywa gongo, anatumia madawa, kila mwaka ya kulevya na kila mwaka mimba halafu upate faida?