NHIF mje na mfumo mpya

NHIF mje na mfumo mpya

Wangwambo

Member
Joined
May 22, 2020
Posts
20
Reaction score
14
Kumekuwa na taarifa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ya kwamba mfuko wa bima ya afya kukumbwa na changamoto mbalimbali za ukwasi, na hii inadhihirishwa na NHIF wenyewe walivyokuja na mwongozo kwa wanufaika wa idadi ya siku za kwenda kupata matibabu kwa mwezi na baada ya siku chache wakasitisha.

Wanachama wengi wa NHIF wamekuwa wakilalamika na hata kugombana na baadhi ya wahudumu wa hospitali hususani za private kwenye kipengele kidogo cha kujaza gharama za matibabu. Wahudumu wengi wanajaza baada ya mgonjwa kuondoka na haijulikani wanajaza kiasi gani hii hali inapelekea NHIF kuyumba kipesa.

Nchi yetu ina watalamu wengi sana wa mifumo, ningeshauri zile sms wanazotuma mara baada ya mnufaika kupata huduma basi ziambatane na bei husika iliyotumika, hii angalau inaweze ikasaidia kunusuru NHIF kufirisika.
 
We need to go into the primary aim of NHIF ilianzishwa kwa lengo gani kipato chao kilikuwaje? matumizi yao? na Fedha zilizokopwa na serikali zilisha rudishwa? usikute Serikali kuu inahusika na kufilisika huko mnataka kuhamisha tatizo hili kwa wachangiaji.

Same as mifuko mingine ya jamii shida ni hiyo hiyo, awamu iliyopita walimerge hii mifuko shida ni hiyo hiyo kufilisika na uwekezaji usiona mashiko bila kuangalia return na demand za wenye mifuko husika.

Kwenye nchi zenye discipline ya fedha nifuko kama NHIF inapesa nyingi sana hata kufikia kununua hati fungani za kiserikali na sio kujiingiza kwenye miradi ya real estate kama hapa au serikali kuchukua fedha bila ahadi maalum za urejeshaji.

Na sasa serikali inaingilia jinsi ya kubadili sheria na kumbana mchangiaji ambae kimsingi ndio owner wa mifuko hii. Hii ni very bad.

Serikali irejeshe pesa yote ya mifuko hii ya jamii in full na kuachana na uwekezaji kwenye maendeleo bila kumjali wananchi wake. Primary issue kwa serikali ni watu wake sio vitu au madaraja tu.
 
Wakifuja pesa kutona na hasara huko kwenye uwekezaji uchwara na matumizi ya kifahari wanakuja kulalama.
 
Ukiwa mwongo lazima uwe na kumbukumbu nzuri sana laah utaadhirika sana.
 
Kumekuwa na taarifa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ya kwamba mfuko wa bima ya afya kukumbwa na changamoto mbalimbali za ukwasi, na hii inadhihirishwa na NHIF wenyewe walivyokuja na mwongozo kwa wanufaika wa idadi ya siku za kwenda kupata matibabu kwa mwezi na baada ya siku chache wakasitisha.

Wanachama wengi wa NHIF wamekuwa wakilalamika na hata kugombana na baadhi ya wahudumu wa hospitali hususani za private kwenye kipengele kidogo cha kujaza gharama za matibabu. Wahudumu wengi wanajaza baada ya mgonjwa kuondoka na haijulikani wanajaza kiasi gani hii hali inapelekea NHIF kuyumba kipesa.

Nchi yetu ina watalamu wengi sana wa mifumo, ningeshauri zile sms wanazotuma mara baada ya mnufaika kupata huduma basi ziambatane na bei husika iliyotumika, hii angalau inaweze ikasaidia kunusuru NHIF kufirisika.
NHIF wana mkataba na watoa huduma na sehemu ya mkataba unaainisha bei za dawa na vipimo pamoja na consultation. Hakuna mahali mtoa huduma anaweza kujiandikia tu bei ya dawa.
 
Hili jambo nadhani linahitajika kujadiliwa kwa ukweli na nia njema bila ya kuleta chembe chembe za ushabiki bila ya kulijua jambo. NHIF kuharibika kwake kunatokana na usimamizi hafifu na mbovu na wala si michango ya wanachama.

Mimi mara mbili nimewahi kuwa na bima za Afya na sikuwahi kuzitumia. Kwa maana nyingine michango ya bima hizo ilitumiwa na watu wengine. Hali hii iko kwa wachangiaji wengi sana wa NHIF na mifuko mingine ya bima ya Afya.

Mimi naona tatizo kubwa liko kwa waaandika matibabu wa Hospitali zote za umma na za binafsi. Aina za vipimo, madawa na hata siku za kulazwa Hospitalini, ndiyo tatizo kubwa sana la NHIF.
 
We need to go into the primary aim of NHIF ilianzishwa kwa lengo gani kipato chao kilikuwaje? matumizi yao? na Fedha zilizokopwa na serikali zilisha rudishwa? usikute Serikali kuu inahusika na kufilisika huko mnataka kuhamisha tatizo hili kwa wachangiaji.

Same as mifuko mingine ya jamii shida ni hiyo hiyo, awamu iliyopita walimerge hii mifuko shida ni hiyo hiyo kufilisika na uwekezaji usiona mashiko bila kuangalia return na demand za wenye mifuko husika.

Kwenye nchi zenye discipline ya fedha nifuko kama NHIF inapesa nyingi sana hata kufikia kununua hati fungani za kiserikali na sio kujiingiza kwenye miradi ya real estate kama hapa au serikali kuchukua fedha bila ahadi maalum za urejeshaji.

Na sasa serikali inaingilia jinsi ya kubadili sheria na kumbana mchangiaji ambae kimsingi ndio owner wa mifuko hii. Hii ni very bad.

Serikali irejeshe pesa yote ya mifuko hii ya jamii in full na kuachana na uwekezaji kwenye maendeleo bila kumjali wananchi wake. Primary issue kwa serikali ni watu wake sio vitu au madaraja tu.
Hii ndio point kubwa, serikali inachangia sana kufilisi hii mifuko ya uchangiaji halafu wanarudi kwa Gia ingine
Kuna Kampuni inaitwa Mkolazi Holding Limited, ilichukua mabilioni ya pesa kutoka NSSF ili Kuanzisha kiwanda cha sukari lakini matokeo yake hawakuzalisha hata robo kilo
Unaweza kuona kiasi gani cha pesa za wanachama wanaovuja jasho zimeliwa na Hawa watu halafu mwanachama akienda kufuatilia mafao yake wanamtungia sheria za ajabu kua asichukue pesa yake mpaka afikishe miaka 60 Sijui 50
Same applies to NHIF, Hua Wanakopesha hospital kujenga majengo au kununua vifaa, pesa inayotumika huko ni nyingi ila hawasemi badala yake wanajificha kwenye kivuli cha watoa Huduma kua wanawaibia
Nchi ya hovyo sana
 
NHIF wana mkataba na watoa huduma na sehemu ya mkataba unaainisha bei za dawa na vipimo pamoja na consultation. Hakuna mahali mtoa huduma anaweza kujiandikia tu bei ya dawa.
Je mtu akipimwa malaria baade ile form ikaongezwa amepimwa na typhoid nk nk nk? wapi inaonesha kuwa ile form sasa imefungwa/haiwezi kuongezwa chochote, baada ya mgonjwa kusaini. Najua wapo watoa huduma waaminifu sana ila kuna mianya mingi kila mahala ya kupiga dili. sasa badala ya kuthibiti mianya kwanza wanapambana na wenye mfuko

Kuna mambo mengi sana ya kuangalia (research) na sio kisiasa; Mfano; kwa nini watu wanapima hospitali mbili tofauti? Je matokeo yanatofautiana kwa asilimia ngapi? na kama asilimia ni kubwa, hapo ni kushuhulika kwanza na usahihi wa vipimo nk nk nk na kama tofauti ni ndogo sana ; Nguvu kubwa itumike kwenye Kuelimisha....

Waweke wazi gharama za uendeshaji wa mfuko kwa wanachama (wenye mfuko) waone kama zina uhalisia
 
Back
Top Bottom